Je wapi wanajua kazi zaid na Tanzania inaweza kuiga au kujifunza ni CIA, MOSAD, KGB,

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Kwa karibu wiki 2 hivi zimepita shirika la ujajusi la Israel MOSAD inatuhumiwa kwa kuhusika na kifo cha kiongozi wa Hamas huko Dubai, Katika hali ya ajabu sana moja ya watu walihusika wametumia passport za mataifa ya Magharibi, Je katika Tanzania ya leo ni nani anaweza kufaa au kwa watu wa usalama kwenda kujifunza toka kwao, Je ni KGB,CIA,MOSAD au shirika la ujajusi la China??
 
Kujifunza nini mkuu? Hakuna tofauti kubwa baina ya hao na sisi isipokuwa utajiri. Umezungumzia mauaji yaliyofanywa na Mosad huko Dubai unafikiri hii mission ni ya kujifunza sisi waTz? Hawa watu wamepora identity za raia wao, wametumia pasi za nchi za magharibi ambazo zinakata cheki kila mwezi kuendesha Israel. Wametumia millions za $ kuwa-train makomandoo wao alafu wamewapeleka Dubai kwenda kupigwa picha ambazo zimezagaa kwenye mtandao. Sasa hawawezi kuwatumia tena for the most part. Hii mission ni complete failure. CIA wala usimeme uzembe wao. Waliziona vile zile WMD kule Irak. Bajeti ya CIA ni zaidi ya billion $50 kwa mwaka na nusu ya hizo hela ninatiwa ndani for bogus intelligence. Mkuu hiyo hela nyingi mno. Inaweza kuwalisha watanzania wote pilau bure kila siku kwa miaka mitano. Kwani sie Tz adui yetu nani?

¬K
 
ni vizuri kupeleka watu kujifunza katika mashirika yote, kwani katika usalama hakuna uniformity, inafikia kipindi mbinu za MOSAD ndio itahitajika au KGB au CIA nk, kwa hiyo ni muhimu kuwa na varayati ya wanausalama wenye skillz za kutoka mashirika mbalimbali
 
Cha kujifunza ni jinsi gani ujasusi unaweza kuwa na faida katika Taifa, ujasusi katika uchumi, elimu na kila idara katika taifa
 
Thread haieleweki mkuu, irekebishe tumwage sumu
Kitu cha kujifunza hapa ni suala la ujasusi katika usalama wa Nchi, Uchumi na hata idara zote katika taifa letu Tanzania, Je ni wakinani wanafaa ili twende kwao kujifunza usalama na mbinu zote kwa ajili ya taifa
 
Kuna msemaji mmoja wa Ikulu ya Marekani aliwahi kusema " SECURITY IS NOT A PERFECT SCIENCE" kwa hiyo naungana na waliotangulia-tujifunze toka kwa wote na hata nje ya hao waliotajwa, kwani kuna siku tutapambana nao !
 
Kuna msemaji mmoja wa Ikulu ya Marekani aliwahi kusema “ SECURITY IS NOT A PERFECT SCIENCE” kwa hiyo naungana na waliotangulia-tujifunze toka kwa wote na hata nje ya hao waliotajwa, kwani kuna siku tutapambana nao !
Mimi nashangaa sana kuona kwa jinsi gani Taifa linabaki kwenye usalama wa mtu na siyo Taifa na kuchuguza hata rasimili za Taifa letu na na ni kweli ulivyosema ila cha msingi inabadilika sana
 
Kwa karibu wiki 2 hivi zimepita shirika la ujajusi la Israel MOSAD inatuhumiwa kwa kuhusika na kifo cha kiongozi wa Hamas huko Dubai, Katika hali ya ajabu sana moja ya watu walihusika wametumia passport za mataifa ya Magharibi, Je katika Tanzania ya leo ni nani anaweza kufaa au kwa watu wa usalama kwenda kujifunza toka kwao, Je ni KGB,CIA,MOSAD au shirika la ujajusi la China??

Naona mnachangia kama vile vyombo vilivyotajwa hapo ni vyuo vikuu.

Kwanza mkae mkijua kila kimoja kipo 100% kwa maslahi ya nchi zao. Pili Wenzetu hata bila ya kuwa majasusi hawatuamini hata kidogo.

Tatu wamejifunza kututumia kwa maslahi yao.....kwa hiyo hata mafunzo ya kijeshi wanayotusaidia mara nyingi ni kwa ajili ya wao kujinufaisha kwenye Resource Explorations na Business Relationships. Hawawezi kukupa wewe siri nzito halafu ukaziendeleza na kuja kuwaletea tabu baadaye.

Na ukiwapelekea kifaa wakajua kitaleta faida kwa Afrika wanakipiga sumu tu hawataki ''another Osama Bin Laden''

Kwa kifupi mtoa mada hana ujuzi na mambo ya kijasusi na inaonekana anafikiri Ujasusi ni Cinema, Sifa na kujiburudisha. Hao Guonbu wenyewe wa China wako kibao Kariakoo, nyinyi mnafikiri wanauza maua!!!!!!! Achana na Mossad wazee wa by way of deception we shall do war, au MI5 wazee wa secretive...au CIA...thou shall know the truth au FSB( Siyo KGB wewe...hiyo ni zilipendwa haipo)...sasa hivi wachina na GUONBU...ni balaa...na huna cha kujifunza kwao!!!!!

Mnajua kwa nini kwenye tenda za barabara wanashinda wao. Bei yao chee sana na ukiangalia kwa bei yao ni kama wanapata hasara sana, mnajua ni kwa nini wanakubali hasara????? kwamba quality ni ndogo???? Ujasusi ni ishu...shauri yenu!!!!!!!!
 
Wote hawa wanafaa,Tanzania inaweza kujifunza kwao. Lakini nadhani CIA ndio wanafaa zaidi,kwa sababu MOSAD NA KGB[FSB siku hizi],wana historia ndefu,historia ndefu sana ya ukiukaji wa haki za binadamu,historia ya kutoheshimu binadamu.
 
intelligence inahitaji some inborn traits ambazo wengi wa intelligence officers wetu wanaotokana na ama kuwa houseboy au watoto wa wanasiasa hawana,tunahitaji an intelligence unit in its real sense ambao watatusaidia sana kwa kuwa mbele kimtazamo katika nyanja mbalimbali kuanzia kwenye ulinzi na usalama wa taifa letu,uchumi na maendeleo ya taifa letu kwa ujumla wake,haisadii sana kuwapeleka watz kujifunza mossad au CIA kwani vitngi ya vitu watavyofundishwa hawatapewa nafasi ya kuvidemstrate hapa Tz,majukumu ya wanausalama wa tz kwa kiasi kikubwa si kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya watawala wetu.
 
]
Cha kujifunza ni jinsi gani ujasusi unaweza kuwa na faida katika Taifa, ujasusi katika uchumi, elimu na kila idara katika taifa
[/COLOR][/QUOTE]
huo ndio ujasusi na ndio tunapaswa kuiga.
sio hawa UWT wetu, ni vimeo, ni tawi la chama cha mapinduzi.
wanafanya kazi za uajenti wa chama, wanawatisha wanaotishia uhai na usalama wa chama hicho, wanalinda wezi wa mali za umma, wetu ni genge la wajinga na vibaka.
 
Naona mnachangia kama vile vyombo vilivyotajwa hapo ni vyuo vikuu.

Kwanza mkae mkijua kila kimoja kipo 100% kwa maslahi ya nchi zao. Pili Wenzetu hata bila ya kuwa majasusi hawatuamini hata kidogo.

Tatu wamejifunza kututumia kwa maslahi yao.....kwa hiyo hata mafunzo ya kijeshi wanayotusaidia mara nyingi ni kwa ajili ya wao kujinufaisha kwenye Resource Explorations na Business Relationships. Hawawezi kukupa wewe siri nzito halafu ukaziendeleza na kuja kuwaletea tabu baadaye.

Na ukiwapelekea kifaa wakajua kitaleta faida kwa Afrika wanakipiga sumu tu hawataki ''another Osama Bin Laden''

Kwa kifupi mtoa mada hana ujuzi na mambo ya kijasusi na inaonekana anafikiri Ujasusi ni Cinema, Sifa na kujiburudisha. Hao Guonbu wenyewe wa China wako kibao Kariakoo, nyinyi mnafikiri wanauza maua!!!!!!! Achana na Mossad wazee wa by way of deception we shall do war, au MI5 wazee wa secretive...au CIA...thou shall know the truth au FSB( Siyo KGB wewe...hiyo ni zilipendwa haipo)...sasa hivi wachina na GUONBU...ni balaa...na huna cha kujifunza kwao!!!!!

Mnajua kwa nini kwenye tenda za barabara wanashinda wao. Bei yao chee sana na ukiangalia kwa bei yao ni kama wanapata hasara sana, mnajua ni kwa nini wanakubali hasara????? kwamba quality ni ndogo???? Ujasusi ni ishu...shauri yenu!!!!!!!!
Inaonekana wewe ndio unajua kuwa ujasusi ni wa cinema tu, ila hata kulinda, kutoa Economic intelligence katika idara mbalimbali katika Taifa ni jambo nzuri vitu vyote vinakwenda sambamba, na Mimi sikusema kuwa ni M15 hata kidogo ila ni mfumo wa kupata, habari kwa haraka sana na kuchuguza kijasusi, Jiulize kuwa ni kwanini mpaka leo mambo mengi hatujui, masuala ya EPA, Richmond, na uozo mwingine na hata kuna umuhimu sana wa restructure usalama wa Taifa wa Tanzania. Je ni nini kazi ya usalama wa Taifa katika Taifa letu?? jiulize maswali haya ndio unaweza kusema na kutoa jibu nzuri mkuu
 
intelligence inahitaji some inborn traits ambazo wengi wa intelligence officers wetu wanaotokana na ama kuwa houseboy au watoto wa wanasiasa hawana,tunahitaji an intelligence unit in its real sense ambao watatusaidia sana kwa kuwa mbele kimtazamo katika nyanja mbalimbali kuanzia kwenye ulinzi na usalama wa taifa letu,uchumi na maendeleo ya taifa letu kwa ujumla wake,haisadii sana kuwapeleka watz kujifunza mossad au CIA kwani vitngi ya vitu watavyofundishwa hawatapewa nafasi ya kuvidemstrate hapa Tz,majukumu ya wanausalama wa tz kwa kiasi kikubwa si kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya watawala wetu.
Umesema ukweli kabisa katika mambo haya yote mkuu wangu, Asante sana kwa mchango wako
 
Mleta mada asante.

Kuanza kwa kunukuu tukio ambalo Israel (MOSSAD) inayotuhumiwa kuuwa Kiongozi ndani ya nchi nyingine kwa kufoji / kuiba na kutumia hati za kusafiria za Mataifa mengine kisha ndipo tunaulizwa ni nani ambaye kwaye tunapaswa kujifunza; ni kuongeza utata usio wa lazima katika mjadala au kusudio la thread! Maana mwingine atafikiri kuwa unaongelea kujifunza kutekeleza hiyo skandali ambayo sasa inaendelea kuwa katika uchunguzi na mataifa mengi ya Ulaya & Australia wamelaani vikali. Na kwa hakika hii italigharimu Taifa lililohusika kama alivyoonya mzungumzaji wa Australia.

Tunapojadili juu ya idara hii, katika karne hii dunia inaongelea dhima ya Ulinzi, Usalama, Tafiti & Maendeleo na sio kuishia kuongelea tu 'Ujasusi'! jina ambalo linakuwa na negative connotation. Ndio maana huwezi kutoka tu na kuiba passport ya raia wa Mataifa mengine uzazitumia kufanya maasi ukadhani utabaki watu wakusifie eti wewe ni babu kubwa au eti unaamua tu kuwateka raia wako na kuwasurubu na kuwaondoa uhai bila hata jamaa zao kujua pasipo kufuata utawala wa sheria na kujali haki za binadamu (ingawa hii nayo haitakiwi kuzidi sana).

Kama mwingine alivyosema mimi naona mafunzo tunaweza kujifunza toka sehemu mbalimbali so long as kweli tunaongeza ujuzi. Kwa mazingira na matatizo yetu yapo mengi yanaweza kufanyika hata bila kuhitaji msaada wa nje.

Ni vyema tusilaumu tu idara ilivyo bali tutoe maoni ya nini kifanyike. Nawaheshimu sana wale wanao weza kuchambua tatizo tulilo nalo na pili wakatoa mapendekezo nini kifanyike.

Ebu bonyeza hapa kama ulikuwa hujaona:

https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/51349-nini-kibadilishwe-au-kuboreshwa-uwt.html
 
Asante sana kwa michango yako yote na pia natumaini watu na wahusika watakuwa katika hali ya kufanya mambo ya muhimu katika Taifa letu na pia katika kujua ni jambo gani lina manufaa katika Tanzania
 
Kujifunza nini mkuu? Hakuna tofauti kubwa baina ya hao na sisi isipokuwa utajiri. Umezungumzia mauaji yaliyofanywa na Mosad huko Dubai unafikiri hii mission ni ya kujifunza sisi waTz? Hawa watu wamepora identity za raia wao, wametumia pasi za nchi za magharibi ambazo zinakata cheki kila mwezi kuendesha Israel. Wametumia millions za $ kuwa-train makomandoo wao alafu wamewapeleka Dubai kwenda kupigwa picha ambazo zimezagaa kwenye mtandao. Sasa hawawezi kuwatumia tena for the most part. Hii mission ni complete failure. CIA wala usimeme uzembe wao. Waliziona vile zile WMD kule Irak. Bajeti ya CIA ni zaidi ya billion $50 kwa mwaka na nusu ya hizo hela ninatiwa ndani for bogus intelligence. Mkuu hiyo hela nyingi mno. Inaweza kuwalisha watanzania wote pilau bure kila siku kwa miaka mitano. Kwani sie Tz adui yetu nani?

¬K

Sina uhakika kama ni failure kama unavyodhani, sometimes failure may be part of the mission !!!,
 
Ni kweli kabisa failure inaweza kuwa part of mission na kurudi kujifunza na mbinu upya na kutazama makosa yamefanyika wapi ila sisi kama Watanzania kuna umuhimu sana wa kuboresha usalama wa taifa na kuona unaendana na changamoto zilizopo kwa ajili ya kizazi chetu
 
Wote hawa wanafaa,Tanzania inaweza kujifunza kwao. Lakini nadhani CIA ndio wanafaa zaidi,kwa sababu MOSAD NA KGB[FSB siku hizi],wana historia ndefu,historia ndefu sana ya ukiukaji wa haki za binadamu,historia ya kutoheshimu binadamu.

Mkuu, kama ni kufuru ya kukiuka haki za binadamu CIA wanaongoza. Angalia baadhi ya matukio yao:

-CIA ndio waliomuua Patrice Lumumba wa Congo baada ya kuona anamwelekeo wa kijamaa
-CIA kwa kutumia biologicaL weapons (futuristic weather modification technology), waliharibu mashamba ya miwa nchini CUBA wakati wa vita baridi, miwa ilikuwa ndio chanzo cha uchumi wa CUBA. Pia walipandikiza virusi vya african swine fever na kuua mifungo mingi sana
-CIA wamehusika moja kwa moja kupindua serikali za Nicaragua, Guetimala, El salvador

Kama ni suala la kujifunza bado twaweza kujifunza kwa wote, hizi covert operations hakuna kuangalia suala la haki za binadamu (almost and always quick wins achieved through ilegal means). Lakini Idara za usalama kwa sasa zinalenga pamoja na usalama kuhujumu nchi nyingine resources zao ili kujenga uchumi wa nchi husika
 
[/B]

Ni kweli kabisa USA na mashirika yake ni Taifa namba moja kwa kuingilia mataifa mengine soma Kitabu cha Chomosky anasema vizuri san na pia wame meddling katika sehemu zote ila walifanya hivyo kwa ajili ya nini??? hapa ndio nasema kuwa ni kwa ajili ya interest za taifa lao na idara zao
 
Back
Top Bottom