Je wanasiasa walioshabikia lolondo kwa babu tuwasulubu vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wanasiasa walioshabikia lolondo kwa babu tuwasulubu vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EstoJ, Nov 1, 2011.

 1. E

  EstoJ Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [HR][/HR]Wapo wengi walio chochea watu kuziacha hosipitali na kukimbilia kwa mganga wa kienyeji tena wkionywa kwa nguvu kubwa na viongozi wa kilokle na kiisilam. Wengine tulifikia mahali pa kuwatukana kuwa wanahofu ya kupoteza waumini na sadaka. Sasa ukweli umekuwa wazi kuwa walikuwa sahihi kabisa. Moja ya nukuu nilizowahi kuzisoma ni zile zilizomshambulia waziwazi mtume mwingira aliposema kupitia television yake kuwa muda si mrefu babu atapoteza umaarufu na kufa na wale waliokunywa watakufa. Sasa watu wengi wamepoteza maisha kw kukimbia hosipitali. Juzi nilisoma juu ya babu kupoteza umaarufu na nikakumbuka kuwa yaliyosemwa yanatimia bado la kufa tu kwa mganga huyu.

  Tena kwa masikitiko zaidi yupo mtumishi marufu kama mzee wa upoko yeye alienda mbali zaidi kwa kuwashawishi waumini wake waende loliondo, pia lipo kanisa lilijiingiza kichwa kichwa na kubwa zaidi ni hawa viongozi wa taifa waliopnga foleni na kuaminiwa kwao kukawaponza wengi. Sasa issue imechina wamekaa kimya hata hawaombi radhi huku bado mamia wanendelea kuangamia. Tuliowapuuza sasa wanapata ushidi. N i hiv karibuni nilimsikia mwingira akisema wako wapi waliompinga na akasisitiza siku za babu zinahesabika na kuwaambia walikimbilia huko warudi kwa wchungaji wao wakatubu sivyo hawaponi.

  Sasa swali langu: TUTAWAFANYAJE HAWA WALIOTUPONZA BILA KUFANYA UTAFITI WA KISAYANSI WAHALI WAO NI VIONGOZI?
   
Loading...