Je wanasiasa kuwapinga wataalamu (maprofesa) tunaipeleka wapi nchi yetu ya tz? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wanasiasa kuwapinga wataalamu (maprofesa) tunaipeleka wapi nchi yetu ya tz?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Nov 14, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Ni jambo lisilo la kawaida nchi yoyote ile wanasiasa kupingana na wataalamu katika dunia hii ambayo inahitaji mawazo ya wataalamu ili kuleta maendeleo.
  Nchi ya TZ inaongozwa na viongozi wanasiasa katika sekta/wizara mbalimbali ambazo hawana taaluma ya hiyo sekta anayoiongoza lakini inafikia wanasiasa wanapinga mawazo ya wataalamu(maprofesa) waliobobea, waliosomea huo utaalamu zaidi ya miaka 10, siyo jambo la kushangaa sana kuona sekta/wizara fulani ambayo inaongozwa na mtu ambaye hana taaluma ya hiyo sekta ila cha msingi ni kwanini mtu kafikia form 4/form 6 na ikibidi kafikia darasa la saba anaamua kupingana na dokta aliyesomea afya ya binadamu zaidi ya miaka 10 na kuitwa prof, Engineer , mwanasheria aliyebobea na kuitwa prof lakini mwanasiasa anampinga na kumuita muongo, je hii nchi yetu ina viongozi walio makini au???

  Nasema hivyo kwa maana leo asubuhi nimeshuhudia Wasira kama waziri anawapinga akina Profesa Shivji kuwa hawaelewi huu mswaada unaitwaje na unamaanisha nini ndoo maana wanawapotosha wananchi, Wasira amejaribu kuwakejeli Maprofesa na wataalamu wa sheria waliokipaumbele na jukwa la katiba kuwa hawaujui mswaada huu wa marekebisho ya katiba,
  hii inamaanisha kuwa wanasiasa ndoo wanajiona kuwa wanajua kila kitu kuliko wataalamu ambao wamesomea huo utaalamu zaidi ya miaka 10 au ni udogo wa mawazo ya wanasiasa wetu wa TZ???
   
 2. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Mhhh hatutafika!!!
   
 3. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa CCM woote ni vilaza,na wanafanya kazi kimagumashi hakuna hata mmoja mwenye uafadhali,wengi wana vyeti vya kufoji wengine ni wavuvi wa samaki lakini kwa kujuana na mkulu wamepewa sekta,katika serikali ya Tanzania kuna kiongozi mmoja tu ndani ya magamba ambaye ni msomi na muelewa MAGUFULI pekee,wengine wooote ni magalasha tu elimu za kuunga na super glue.
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hopeless
   
 5. m

  mbwago2007 Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila shaka wanavuna walichopanda. Sasa hivi wahadhiri wengi wakiwemo maprofu wamejtumbukiza kwenye chama cha magamba ambacho hufikiria kwa masaburi na kina historia ya kusema uwongo, ufisadi, unafiki wizi wa kura n.k. Katika hali kama hiyo unatarajia nini. Kama wasomi haou wanaingia kwa mfano katika kugombea ubunge na anafahamu ameingia bungeni kwa kuchakachaua kura na dhamira yake haiwezi kumsuta. Je unatarajia kuheshimiwa. Tulizoea kuwaona wasomi hao wakitoa mada nzito za kuleta maendeleo lakini kwa sasa hivi tumeshuhudia akina Bana and company wakijipendekeza kwa watawala. Hali kama hii inashusha hadhi ya wasomi hao ktika jamii makini.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  masaburi kazini!
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  mtumikie kafiri upate mali, ndo mwendo wa magamba siku hizi
   
 8. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ukishanunuliwa na magamba haa uwe na tuzo ya nobel utakuwa kilaza kwa kuswma ndiyo kwa mzee wa bagamioyo
   
 9. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wataalamu wamenunuliwa!
   
 10. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Wasira ana elimu gani ya kuwapinga maprofu??/
   
 11. A

  Ame JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Tutafikaje na wewe bado unapepea bendera ya chama cha mafisadi? Mm hadi hizo rangi zao nimezipiga marufuku sehemu yeyote niliyo na authority nayo kwasababu hizo rangi ndo zimeloga akili za watanzania wengi...
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yote haya yanatokana na ulevi wa madaraka walio nao ccm pia na thinking capacity yao imefika mwisho they have to retire
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Samaki mmoja akioza wote wanaoza nae magufuli hamna kitu ktk bunge lililopita alitudanganya baraba za juu zimeanza kujengwa dar na mpaka leo hatujaona kitu au alizijengea kwenye ndoto?
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkono mtupu haulambwi
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kilichopo hapa ni kama mafisi(watawala) wapo na mzoga(wameshika utamu wa kula kodi na misaada ya wafadhili) wakiona kiumbe yeyote anataka kuwaondolea mzoga huo huwa hawangalii kuwa mnyama huyo ni Simba au bweha, kwa ujumla mbele ya mzoga fisi huwa hana busara na wakati mwingine kujikuta wana challenge hata simba huku wakijua fika kawazidi uwezo wa kila kitu zaidi ya simba kutokuwa na mzoga.

  Katiba ni last breath of CCM, Katiba yoyote inyowapatia wananchi uwezo wa kuamua hatma yao ni one way ticket ya CCM.
   
 16. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Werema na Wasira wanaishi Tanzania ya zamani,TZ ya ndiyo mzee
  ambayo wasomi walikuwa wakiimba na kuitukuza serikali.

  Hawajui na hawasomi alama za nyakati zama za mwamko mpya
  ambapo wasomi wanatakiwa kuishi katika kweli,hawaoni kina dr bana
  walivyotia aibu na REDET?Hizi ni zama nyingine.
   
 17. U

  UNIQUE Senior Member

  #17
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAWA WAKINA WASIRA WANA AKILI NZURI ILA LAZIMA WATETEE MAATUMBO YAO. Utakuwa kichaa aliyepitiliza kumpinga MZEE WETU Pfof SHIVJI , BAREGU. HAWA WAZEE WAKO VEMA. CCM LAZIMA TUWADUNDE SAFARI HII. WANAFIKIRI TUMELALA? TUKO MACHO. MHESH TUNDU LISU BIG UP. HAYO ULIYOSEMA NDIYO TUNATAA
   
 18. N

  N series Senior Member

  #18
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hko umagambani majembe yapo bt ndo hvo tena huyo kilaza wa ukwereni anawakandamiza sana,kama mh.samwel sitta,mwakyembe,na hiyo power tiller magufuli,yeye ni zaidi ya jembe . . . . .
  Kuwapinga wasomi ni kutokana na kwamba wanasiasa wa umagambani wapo after their own feed na chama chao cha mafisadi . . .
  Wanajua wakiwaskiliza wasomi mlo hakuna,
  Na kuhakikisha uswahiba uliopo,kiongozi akiharibu area A,utaskia kahamishiwa area B,kwanin wasifukuzwe kazi?
  Wizi mtupuu. . .
   
 19. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Sera ya ccm ni kuwanyonya watanzania ndio maana hata hao akina magufuli mda mwingine wanajilimbikizia mali kwa mgongo wa chupa
   
 20. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nafikiri Wasira yuko sahihi.
  Kazi ya siasa ni ya wao akina wasira kusema lolote kwa maslahi yao. Kwa upande wa wataalam, walipaswa kutoa ujuzi kulingana na elimu waliyonayo, au kama inavyodaiwa wamesoma nakubobea.
  Inapofika wakati maprofesa wanaongea kwa niaba ya wanasiasa au kwa lengo la kuwafurahisha wanasiasa, nachelewa kusema sioni umuhimu wao kama wataalam. Kwa msingi huo hawafai kwa lolote.
   
Loading...