Je, wanaosifia sakata la mchanga ni werevu mno au wajinga mno?

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kutokana na Mikataba Mibovu iliyofungwa na Serikali ya ccm kwa wawekezaji wanachukua Asilimia 97 sisi kama Nchi tunachukua Asilimia 3 kwa hiyo Kwenye ule Mchanga sisi kama nchi tunatakiwa kulipwa na Wawekezaji Asilimia 3 tu, wabunge Wa upinzani kila siku wamepiga kelele bungeni hiyo mikataba iwekwe wazi mfano Mhe, John Mnyika.

sasa hayo matrioni yaliyokuwa tunaambiwa na Rais kuwa tumeibiwa baada ya mchanga kwenda nchi ya nje kumbe ni Porojo tu kama porojo za Serikali ya Viwanda, Buzwagi, Nyamongo na Geita Gold Mine tunalipwa Asilimia 3 tu yaani hata kama huo mchanga ungechakatwa hapa hicho ndicho tungelipwa.

Yaani hayo matrioni yashindwe kupatikana kwenye migodi yote inayochakata Dhahabu nchini yapatikane kwenye Mchanga unaenda nje huu ni uzuzu Wa PhD, kuna watu wamelogwa sio Bure mnachoambiwa mnalipuka kushangilia tu.

MalcomX alipokuwa akiongea na vijana Wapigania haki zao huko Mississippi (1965) alisema "Moja ya vitu ambavyo ningependa vijana wajifunze siku hivi, ni kuona wewe mwenywe, kusikiliza wewe mwenyewe, na kufikiri wewe Mwenyewe. Na hapo ndio utaweza kuja katika uamuzi Wa Busara kwa ajili yako Mwenyewe.

Ninashangaa kuna watu wanaacha watu wengine wafikiri badala yao tena nachoka kabisa ninakuta Asilimia kubwa ni Vijana, utawasikia wanasema ni Mzalendo kuzuia Mchanga je vipi kuhusu uuzwaji holela Wa Nyumba za umma, nani alikuwa Waziri Wa makazi, sometime tuwe tunafiri tukishirikisha Akili zetu jamani, Wakenya wanatucheka.

Ngoja Tuone wanaweza kutupeleka mahakamani tukalipa kama alivyokurupa kukamata samaki sasa tunadaiwa mabilioni.

Mhere Mwita
2017
 
Mbona unafikili kama darasa la pili C, au una vyeti fake?Nyumba aliuziwa mzungu au ziliuzwa Ulaya?hakuna mtu anayeshangilia hapa tunasema hatua imepigwa kupunguza wizi
 
Wewe sidhani kama ni Mtanzania,kama ni Mtanzania huwezi pinga kile mheshimiwa anachokifanya labda kichwani ndio uwe na matatizo.Kwa mtazamo wako unakubaliana na wizi unaofanyika Wa madini, hujaona kuwa hii ya mchanga ni hatua ya kwanza ya kuzui wizi huu na urasimu unaofanywa na hawa Accasia,ungekuwa wa maana ungeona juhudi za serikali nzuri na vile vile ni harakati ya kutatua na kufumua hiyo mikataba uchwara...je wew hizo data umeambiwa?
Huyu sio ndioooooooooooooooooooooooooooooooooo kama nyinyi Lumumba. We have to think!
 
Mbona unafikili kama darasa la pili C, au una vyeti fake?Nyumba aliuziwa mzungu au ziliuzwa Ulaya?hakuna mtu anayeshangilia hapa tunasema hatua imepigwa kupunguza wizi

hatua ipi na kupunguzwa wizi upi? na nani anaibiwa? mnajifanya mmesahau jinsi nyumba zilivyouzwa kimagumashi? mpaka kuna mrembo mmoja hakua mtumishi wa umma na yeye alipata mjengo chini ya maelekezo ya mkulu.
 
Hapa kuna mambo kama matatu hivi moja wapo lazima litakuwa linakuhusu
1.Ulikuwa muuza ngada au MLA ngada sasa Ngosha amezibiti
2.Ulikuwa na vyeti fake na kwa mwezi huu umekosa mshahara mambo yako yapo tite.
3.Ulikuwa kwa mzungu mgodini sasa unawasiwasi na mgodi kupunguza watumishi baada ya sakata hili,au no mfanyakazi wa TMAA mambo hadharani sasa
 
hakuna hata moja ulilopatia bila shaka hiyo ni dalili za uganga wa kienyeji na ramli chonganishi
 
Wewe sidhani kama ni Mtanzania,kama ni Mtanzania huwezi pinga kile mheshimiwa anachokifanya labda kichwani ndio uwe na matatizo.Kwa mtazamo wako unakubaliana na wizi unaofanyika Wa madini, hujaona kuwa hii ya mchanga ni hatua ya kwanza ya kuzui wizi huu na urasimu unaofanywa na hawa Accasia,ungekuwa wa maana ungeona juhudi za serikali nzuri na vile vile ni harakati ya kutatua na kufumua hiyo mikataba uchwara...je wew hizo data umeambiwa?
Kipindi mikataba inaingiwa Magufuri alikua diwani? Na kama alikua mbunge alitoa ushauri gani kwa Serikali kama mzalendo? Kama alipinga uhuni huu ambao unatutesa sasa weka clip ili tumuunge mkono kwa nguvu zote na kama sio kwanini anatumia siasa kutaka kulitatua hili tatizo au ana mgao na hayo mabilioni ambayo kama Serikali itagharamia endapo hawa wezi watashinda kesi kwa mikataba ambayo waliipitisha ccm? Tumieni wanasheria ktk kulitatua jambo hili huu ni muda wa kuumiza vichwa ktk kuifumua mikataba ya hovyo kama hii kuliko mihemuko
 
Tehe tehe tehe nimekusoma maana stress zipo juu sana na kwa taarifa huyu Mwanaume atatusukuma miaka yote kumi

Mimi mwenyewe ni mwnaume na wala sijawahi na kamwe sintofikiria kufanya au kuajiriwa na wadhalim na chama kilicha saini mikataba ya kuwaibia wa tz na leo wanakuja kivingine na kujifanya wazalendo waliotukuka na majuha kama wewe unakuja na upupu wako huku mkitaka sapoti yetu.... mtajijua wenyewe hata kama nchi ni yetu sote kwenye huu ujinga wengi wetu hatutowaunga mkono mlilikoroga na sasa ni wakati wa kulinywa wenyewe
 
Kuna mtu kaja inbox anakujua naona nikuache umebanwa tayari tutakutana Mahakama ya Kisutu
 
hahahahahaaaaaa acheni uongo wa mchana kweupe nyie ndio mmesema mkulu alipelekewa bilion 300 akazikataa na pia hajawachukulia hatua waliompelekea hizo hela jinsi anavyopenda kiki? wengi wanajitambua siku hizi acheni utaahira.....
eti tutakutana kisutu kufanya nini? hata huko dar hua nikija naishia kufanya mambo yangu na bata zangu za hapa na pale then back to the flight....
acha ujinga wewe mtu mzima hovyo
 
Wawekezaji wanachukua alimia 97% Tanzania inachukua asilimia 3%,,,,kuna msemo wa kiswahili unaosema "wajinga ndio waliwao"

Watanzania na Afrika tutaendelea kuwa maskini maisha yetu yote kwa vile hatuwezi kujitawala,waafrika hatuna uwezo wa kujitawala angalia Nigeria,Nigeria inazalisha mafuta lakini haina hata kiwanda kimoja cha kusafishia mafuta,mafuta yanasafishwa nje ya nchi halafu yananunua na kurejeshwa tena Nigeria..

Ni waafrika tu ndio tunatunga katiba halafu anakuja raisi anaipinga hiyohiyo katiba waliyoinandika......
 
Vita huanza kwa kufyatua risasi moja au kurusha bomu moja au kombora moja.

Na mengine ndio hufuata.

Magufuli amelianzisha. Anaweza kuwa amechemka hapa au pale lakini kalianzisha. Kupinga kitu kunaweza kufanywa kwa namna nyingi kwa mfano kwa kususia tu

Alichokifanya magufuli dunia nzima imesikia. Hili ni onyo kwa wengine. Huenda hatutafaidi maana tumekosea hapa na pale lakini dunia ya tatu kuna nchi zitanufaika. Zitajifunza kutokana na nia na makosa yetu

Cha muhimu ni nia ya dhati ya kuondoa huu unyonyaji
 
Hayo makampuni ya kinyonyaji yanayo honga na ku-blackmail viongozi wa nchi masikini wenye tamaa na wasiojiamini yamepata somo. Dunia nzima inashuhudia hili sekeseke. Historia inaandikwa

Na kuna mikataba mingi tu ya madini tutasainishana na makampuni mengine kama acacia. Hili ni somo zuri kwa watakao kuwa wanatengeneza mikataba na kuisaini

Nimefurahi kuwa kuna kitu tumekianzisha. Safari ya kuzunguka dunia nzima huanza kwa kupiga hatua moja

Viva magufuli, viva Tanzania
 
Back
Top Bottom