Je, wanaohama CCM na kujiunga na CHADEMA wataing'oa CCM madarakani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, wanaohama CCM na kujiunga na CHADEMA wataing'oa CCM madarakani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Jul 21, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Huko nyuma tumefananisha chama na nchi. Je,
  ni jambo jema wewe kuikimbia nchi yako kwa
  sababu ina matatizo badala ya wewe kushiriki
  katika kupambana na matatizo hayo?
  Tujifunze kutoka kwa wananchi wa Msumbiji na
  wa Angola na wa Afrika Kusini. Kama
  wangezikimbia kabisa nchi zao wangefanikiwa
  kuzikomboa nchi zao?
  Kwa hivyo wanachama wa CCM wanaoendelea
  kupambana na maovu ndani ya chama chao bila
  kukikimbia hao ni wanachama halisi wa CCM na
  wapenzi wa kweli na wa chama chao.
  Fikiria, kwa mfano, nyumba yako ni chafu.
  Badala ya kuisafisha unaamua kuikimbia.
  Atasafisha nani?
  Sababu nyingine ya wanachama wa CCM
  kukikimbia chama chao hapana shaka ni
  kutoridhishwa na uamuzi fulani uliopitishwa na
  chama.
  Kwa mfano, kuna wanachama wa CCM
  wanaoenguliwa bila haki kwenye kinyang’anyiro
  cha kugombea udiwani au ubunge au hata urais.
  Baadhi yao huamini kwamba wakigombea
  nafasi hizo kwenye chama kingine watafanikiwa.
  Na hufanikiwa.
  Basi sababu mojawapo inayofanya baadhi ya
  wanachama kukimbia vyama vyao (na hii si
  katika CCM tu) ni kukosekana demokrasia ndani
  ya vyama. Hii inaleta hoja kwa kila chama
  kuendesha chaguzi zake kidemokrasia.
  Lakini ukitaka kusema kweli kitendo cha
  wanachama kukimbia chama chao cha zamani
  huleta madhara makubwa zaidi kwenye chama
  wanachokimbilia.
  Maana kwa sababu tu ya mwanachama kutafuta
  maslahi yake binafsi anaamua kwenda kujiunga
  na chama ambacho haamini masharti yake wala
  siasa yake wala sera zake. Mtu kama huyo
  hubaki na mapenzi ya chama chake cha
  zamani. Ndivyo anavyoonekana John Shibuda,
  Mbunge wa Chadema wa Maswa Magharibi,
  aliyehamia Chadema ili agombee ubunge.
  Hapana shaka kuna viongozi wengi wa CCM
  waliokimbia chama chao na kujiunga na
  Chadema wakiamini kwamba mwaka 2015
  wagombea uchaguzi wote watakaowekwa na
  CCM watashindwa uchaguzi! Kama hiyo si ndoto
  ya mchana mimi sijui ni kitu gani.
  Basi katika suala zima la uchaguzi ni muhimu
  viongozi wa vyama waepushe mtafaruku ndani
  ya vyama vyao kwa kuweka mbele matakwa ya
  wanachama badala ya kuweka mbele matakwa
  yao na maslahi yao kwa kuweka wagombea
  wasiokubalika.
  Wakati mwingine mwanachama anaweza
  kufikiri kwamba chama chake kimekosea
  kupitisha uamuzi fulani ambao ni sahihi.
  Akakikimbia chama chake. Mwishoni akajikuta
  anajuta.
  Turudi nyuma mpaka wakati Tanganyika
  ilipokuwa ikipigania uhuru. Mwaka 1957 serikali
  ya Mwingereza Tanganyika iliyoongozwa na
  Gavana Edward Twining, mwana wa Padre,
  ilitangaza kuwa mwaka 1958 Tanganyika
  ingefanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Baraza
  la Kutunga Sheria (Lejiko). Uchaguzi huo
  ulipangwa mpiga kura apige kura tatu kwa
  mpigo. Alitakiwa amchague mjumbe Mwafrika,
  Mwaasia na Mzungu katika karatasi moja ya
  kupigia kura.
  Katika utaratibu huo wa kura tatu Gavana
  Twining alikuwa anatekeleza matakwa ya chama
  cha siasa cha Wazungu cha United Tanganyika
  Party (UTP).
  UTP kilikuwa chama cha pili cha siasa
  kuanzishwa Tanganyika baada ya TANU. Lengo
  la UTP lilikuwa kupigania Tanganyika iwe na
  serikali ya mseto (mchanganyiko wa mataifa
  yote).
  Baadhi ya wanachama wa TANU hawakutaka
  TANU ishiriki uchaguzi huo. Lakini Rais wa
  TANU, Mwalimu Nyerere, alipendelea TANU
  ishiriki uchaguzi huo ili ikiingia ndani ya Lejiko
  ipate nafasi nzuri ya kupambana na serikali ya
  Mwingereza.
  Basi kwa lengo la kufikia mwafaka TANU iliitisha
  Mkutano Mkuu maalumu Tabora mwezi Januari
  1958. Wajumbe walio wengi wa mkutano huo
  walikubaliana na wazo la Mwalimu Nyerere la
  kushiriki uchaguzi huo.
  Ndipo baadhi ya wanachama wa TANU
  wakiongozwa na Katibu Mwenezi wa TANU,
  Zuberi Mtemvu, walijiengua kutoka chama
  hicho wakipinga TANU kushiriki uchaguzi huo.
  Wakaanzisha chama cha African National
  Congress (ANC) ambacho kauli mbiu yake
  ilikuwa “Afrika kwa Waafrika.”
  Uchaguzi Mkuu ulipofanyika Septemba 8, 1958
  yalishindaniwa majimbo kumi ya uchaguzi. Kila
  jimbo lilitakiwa litoe wajumbe watatu
  (Mwafrika, Mwaasia na Mzungu).
  Kwa kuwa mpaka wakati ule TANU haikuwa na
  wanachama Waasia na Wazungu iliamua
  kuwapigia kampeni Waasia na Wazungu
  waliokuwa karibu na wananchi. Uchaguzi
  ulipofanyika TANU ilizoa viti vyote thelathini.
  Ikaingia kwenye Baraza la Kutunga Sheria kwa
  kishindo. Ikabadilisha mambo mbalimbali
  mpaka uhuru ulipopatikana.
  Wale wanachama waliojitenga na TANU chama
  chao hakikupata kitu. Mwishoni kiongozi wa
  ANC, Zuberi Mtemvu, alikikimbia chama chake.
  Akaajiriwa Ikulu na serikali ya Mwalimu
  Nyerere.
  Basi si kila uamuzi unaofanywa na chama
  unakuwa si sahihi. Cha muhimu ni
  mwanachama kuwa makini.
  Wakati huo huo kuna wanachama wa CCM
  wanaokikimbia chama chao kwa kufuata
  mkumbo tu. Labda kuikomoa CCM. Na kufuata
  nyuma yao wanachama hao wanaitwa “oili
  chafu” ambayo haifai kuendelea kutumiwa na
  CCM!
  Kuna wanachama wengine wa CCM
  wanaoaminiwa kuwa wanakikimbia chama chao.
  Kumbe kule waendako wanakwenda kulinda
  maslahi ya CCM! Huwezi kuepusha uwezekano
  huo. Waingereza wamesema, “Politics is a dirty
  game” (siasa ni mchezo mchafu).
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  ADDITION:

  TANU ya Mwalimu Nyerere ilijua hilo mapema. Kwa hiyo haikumpokea kwenye TANU Mwaasia wala Mzungu kabla ya kupatikana uhuru.
  Kwanza TANU iliona kwamba katikati ya
  mapambano ya kutafuta uhuru ilikuwa vigumu
  kumjua Mwaasia au Mzungu aliyekuwa na
  mapenzi ya kweli na TANU. Pili, TANU ilihofia
  kuwa baada ya kupatikana uhuru Waasia na
  Wazungu wangeweza kujitapa kuwa bila wao
  uhuru usingeweza kupatikana. Tatu, TANU
  ilihofia kuingiza kwenye chama watu ambao
  wangejiunga na chama hicho kwa lengo la
  kupeleleza na kukivuruga.
  Kwa hiyo milango ya TANU ilifunguliwa kwa
  Waasia na Wazungu mwezi Januari, 1963 baada
  ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.
  Tofauti na TANU iliyokuwa macho na watu
  ambao wangeweza kuivuruga leo Chadema
  inapigana vita inayodai kuwa ni ya kuwakomboa
  Watanzania kutoka ukandamizaji wa CCM, huku
  ikiwaingiza ndani ya chama mamia (kama si
  maelfu) ya wanachama wa CCM. Wanachama
  wote hawa wa CCM wanatakiwa washiriki vita ya
  kuking’oa chama chao cha CCM!
  Je, itawezekana? Tusubiri.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Irrelevant analysis! Labda nisaidie maana ya political democracy
   
 4. mwimomo

  mwimomo Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wimbi laweza fanya mabadiliko yasiyotarajiwa. Time Will Tell.

  Dalili zilizopo zaonesha hili lawezekana, Late JKN alisema Upinzani utakaoizamisha ccm utatoka ndani yake.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kanu ilipigwa chini ndo itakua ccm only time will tell
   
 6. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema si lolote si chochote.tanzania itajengwa na watanzania
   
 7. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao ni wasaliti wa taifa hawana jeuri hyo,wanahangaikia matumbo yao tu
   
 8. b

  beyanga Senior Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​mbona hamchoki kuijadili chadela mmeliwa mwaka huu bye bye ccm hizi ni rasha rasha masika inaaza 2014 madiwani patamu hapo
   
 9. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,740
  Likes Received: 6,016
  Trophy Points: 280
  Was Kanu stronger than CCM?
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kanu ilimegeka coz powerful members walitoka na kuanzisha chama kingine, dont c that happenin here in bongo bt the way things are goin ikifika 2015 cdm wengi watakua either wamekufa or jela ccm wud do all they can to stay in power for whatever cost
   
Loading...