Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,502
- 4,408
Ningekuwa ni mpinzani wa kweli ningesema kweli daima kwamba wananchi hawahitaji katiba mpya sasa zaidi ya wanavyohitaji maji, umeme na huduma bora za afya na elimu.
Nikiwa kama mpigakura sihitaji mgombea anipe ahadi ya katiba mpya sasa, nitahitaji aniambie ni namna gani atapambana na hali yangu ya ukosefu wa ajira, nitahitaji aniambie ni fursa zipi nitazipata kutokana na bomba la mafuta au mradi wa gesi ya mtwara.
Umefika wakati muafaka wanasiasa kuangalia vipaumbele vya wananchi wao kuliko matumbo yao. Katiba mpya ni muhimu lakini sio sasa ambapo nchi inahitaji kujenga uchumi ulioathiriwa na Corona. Nchi inahitaji kutatua tatizo la ajira.
Licha ya mengi wananchi wanayopitia, Je suala la katiba mpya sasa si ni dhihaka? Kwa sasa hekima ya hali ya juu inahitajika hususani kwa mambo yanayohusu maisha ya watu ambayo hata wanaodai katiba mpya hawawezi kusema katiba mpya ni miongoni kama wakihitajika kufanya hivyo.