Je, wanao badili ID kila siku nao wanakwepa kodi?

Faru fausta

JF-Expert Member
Apr 29, 2017
218
143
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya makampuni makubwa kubadili majina ya umiliki mara kwa mara mfano humu jf kuna bingwa 1 anaitwa HALICHACHI. Halafu kuna kampuni maarufu ya simu Tanzania inaitwa airtel ilianza kwa jina la zain ikaja airtel na sasa wanataka kujiita zone. Je, vodacom hawaogopi kodi?
 
Wanakwepa mtego wa kujulikana maana kuna watu humu ni wafuatiliaji wa mambo kwa kina wanaweza kuunganisha nukta na wakakupata
 
Wanakwepa mtego wa kujulikana maana kuna watu humu ni wafuatiliaji wa mambo kwa kina wanaweza kuunganisha nukta na wakakupata
Kubadili sana ID Si kigezo cha kutofahamika kama wanaume wakiamua kufanya kazi yao haswa!!!
 
Kubadili sana ID Si kigezo cha kutofahamika kama wanaume wakiamua kufanya kazi yao haswa!!!
Inatakiwa pia ujiulze huyo anayebadili sana anafikiria/anajua nini hadi anaamua kubadili??
 
Wengine wakiwatongoza mademu wa MMU wakitoswa basi wanabadili ID kuuwa soo.
 
Ni kweli hata mimi nilishawahi uliza swali hili baada ya kuona mahoteli mengi yanabadili nikapata fahamishwa kuwa kama kampuni ikiuzwa madeni yake yanatakiwa yalipwe sasa ni makubaliano ya muuzaji na mnunuzi na pia kuna kodi inaitwa capital gain.siyo kweli kila jina linapobadilika kuwa na utawala yaani management inakuwa imebadilika kwani wao management ndiyo wanakuwa na jukumu la kulipa kutokana na TIN zao kama wakurugenzi.hivo kubadili jina siyo tatizo ni sawa na wewe kuamua fanya biashara toka Temeke kwenda Ilala au biashara ya nguo badala ya vinjwaji.ila ni vizuri kushirikiana na serikali kama kuna ushahidi wa wakwepaji kwani tukiwaachia hawa sijui TRA peke yao inakuwa siyo uzalendo.sidhani kama kuna ubaya labda wenyewe TRA wakiona wanaweza tusaidia majibu
 
Back
Top Bottom