Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Ndani ya wiki hii kumekuwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa agizo la Magufuli juu ya Uanzishwaji wa Pharmacy katika Hospitali za Mikoa na Rufaa kupitia Medical Store Department (MSD). Huduma hii inatarajiwa kuanza January, 2016. Hili litaifanya MSD kujihusisha moja kwa moja na uuzaji wa dawa katika hospitali na pia kuendelea na kazi yake ya kisheria ya kusambaza dawa nchi nzima. Katika maelezo yao MSD wanadai katika pharmacy zao watauza dawa aina 450 ili kuhakikisha dawa zote zinapatikana hospitali. Ni pigo kwa masikini, watoto chini ya miaka mitano, wamama wajawazito na wazee kwamba watatakiwa kununua dawa hizi na si BURE. Utaratibu ni kwamba ukikosa dawa katika pharmacy ya Hospitali unakwenda kununua pharmacy ya MSD. Najiuliza Je, Kama MSD inaweza kuwa na dawa zaidi ya 450 kwa nini ikose uwezo wa ku supply dawa Hizo katika hospitali za mikoa?, Je MSD itakuwa fair kuona Pharmacy za Hospitali zinakuwa bora kuliko zao ikizingatia kuwa wao msd wanafanya biashara wakati yale ya Hospital yanatoa huduma?.