Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Jamani watanzania wenzangu sidhani kuna asiyefahamu kwamba katiba hii tunayoendelea kuitumia si mali ya serikali au ya bunge au ya mahakam au ya wanasheria au wanasiasa, au ya wanaharakati au ya vitu mfano wa hivyo, hapana!
Katiba hii ya mwka 1977 ni mali ya wananchi wanaounda jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mantiki hii wao ndio wenye mali hiyo (katiba) japokuwa wametapakaa sehemu mbalimbali, mjini na mavueni. Wakulima, wafanyakazi, wafanyabiasha, wajasiliamali, wavuvi. wachimbaji wadogo wadogo nk.
Leo narudia kuwakumbusha kuwa; nyinyi wananchi ndiyo wenye katiba hii, japo iwe nzuri au mbaya.
Ni kwa sababu hiyo sasa, naomba mrejee pamoja nami katika sura ya kwanza, ibara ya 8 ibara ndogo ya (1) kipengere (b) cha katiba yetu hii ambacho kinasema hivi, nanukuu.
"Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wanachi kwa mujibu wa katiba hii"
Hebu tujaribu kutafakari polepole.
Kwamba wananchi sisi ndio msingi wa mamlaka yote! Na tena eti kwamba serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hiyo.
Yaani kwa rugha nyepesi ni kwamba; sisi wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu mamlaka, kwamba yupi tunampa mamlaka na yupi hatumpi mamlaka.
Ni hii inabainisha wazi kuwa ni sisi wananchi wenye maamuzi juu ya chama kipi kiunde serikali na kipi kiwe cha upinzani.
Ni sisi laia na wala si taasisi yoyote yenye mamlaka hiyo!
Vyombo vyote vya ulinzi na usalama, vilivyopokea mamlaka yao kutoka kwa wananchi, kwa mujibu wa katiba hii, vinapaswa kulisimamia, kulinda, na kutetea mamlaka ya wananchi.
SASA SWALI LANGU NI HILI.
Je kwa hali ilivyo hapa kwetu, wananchi wanayo mamlaka haya kweli?
Kwa mfano.
Mwaka 2020 endapo wananchi, kwa mamlaka waliyonayo kwa mujibu wa kifungu hicho juu watataka kukiondoa chama tawala madarakani; wakati huo huo bila kusahau mazingira ya chaguzi zilizopita, je wanayo hayo mamlaka ya kukinyang'anya chama hicho mamlaka waliyokipa?
Je katiba kweli katiba hii imeweka mazingira ya kutumika mamlaka na uwezo huu wa wananchi? au hili ni bado ni changa la macho tu!
Karibuni