je! Wananchi kupinga serikali kandamizi bila kuumiza raia ni uvunjifu wa amani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je! Wananchi kupinga serikali kandamizi bila kuumiza raia ni uvunjifu wa amani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by majata, Nov 13, 2011.

 1. majata

  majata JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  wajumbe hivi wananchi wanapoamua kukinzana na maamuzi kandamizi ya serikali na kuamua kuandamana kudai haki yao pasipo mapigano ya raia kwa raia je! Inaweza kusemwa ni uvunjifu wa amani?

  Katiba ambayo ndio msimamo wa wananchi imeruhusu wananchi kuandamana kwa amani kupinga mambo ambayo yana wakandamiza, iweje leo ionekane kuandamana ni dhambi?

  Kilichojitokeza mbeya, kilijitokeza mwanza na sasa kinanukia kutokea dar na kwenye majiji mengine kwani huko pia bado wafanyabiashara wadogo wananyanyaswa vilevile, nivema wakasikilizwa kwa amani kuliko nguvu ya dola ikatumika na hatimae kusabisha vurugu kubwa kama mbeya.

  Ni aibu kwa serikali kushindana na nguvu ya umma wake na kamwe serikali haita shinda umma.

  Mimi naona uvunjifu wa amani ni ugomvi kati ya raia na raia, na si raia kupinga udhalimu wa serikali unao endelea.
   
 2. m

  mbwago2007 Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala linalofanyika hapa ni kulinda mfumo wa kidhalimu. Hali iliyopo ni kama vile mwizi akimwona polisi kuanza kujishuku na kutafuta mbinu ya kujihami. Serikali yetu imeshindwa kabisa kutimiza wajibu wake, imebaki kama baba mlevi ambaye watoto na mke wake wakidai chakula huwashushia kipigo na matusi. Historia inaonyesha nchi zinazokumbatia mifumo ya kidhalimu kama ya Tanzania aghalabu ni vigumu kuendelea licha ya kuwa na vigezo vyote na viashiria vyote vya kuleta maendeleo. Kwa kawaida mfumo huo ulindwa kwa gharama yoyote ile. Hata hivyo historia inatuonyesha kuwa mwishowe nguvu ya umma hushinda, angalia Ujerumani, Kenya, Rwanda. Na mara baada ya nguvu ya umma kupata ushindi mambo yanabadilika na maendeleo huja kwa kasi kama ilivyotokea kwenye mataifa niliyoyataja hapo juu. Kwa hali hiyo hayo yanayotokea sasa hivi hapa nchini ni mchakato wa kuelekea kwenye taifa huru na lenye maendeleo
   
Loading...