Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Do African Political Activists sincerely fight for Democratic Change or they simply keep alive a well-known old saying "It's Our Turn to Eat"?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu wa Tanzania;

Katika msimu wa joto wa mnamo mwaka 2009, aliyekuwa Rais wa Marekani bwana Barack Hussein Obama alisafiri kwenda nchini Ghana, kama kituo chake cha mwisho wa safari yake ya kwanza ya kimataifa kama Rais, na kutoa hotuba yake katika bunge la nchi hiyo katika jiji la Accra.

Katika hotuba yake, alijadili uhusiano wa taifa lake na Afrika, na ushirikiano uliohitajika kuhakikisha mabadiliko katika bara zima.

images (2).jpg


Alipokuwa jijini Accra, Rais alizungumzia juu ya mada (maudhui) nne ambazo alisema ni muhimu kwa mustakabali mwema wa bara hili la Afrika - demokrasia, fursa, afya, na utatuzi wa migogoro kwa njia za amani.

Rais Obama alitoa hotuba yake ya kwanza ya sera za USA juu ya bara la Afrika akiwa katika taifa mwenyeji ambalo linanafasi ndogo sana kiuchumi au kisiasa kulinganisha na mataifa yenye nguvu zaidi kama Afrika Kusini na Misri.

images (3).jpg


Hata miongoni mwa watu wa Ghana, uchaguzi wa nchi sahihi kwa Obama ulisababisha ukakasi Kwanini aende Ghana?

Baadhi ya Wachambuzi wa msauala ya kisiasa walisema mpangilio wa mazignira wenyewe unasaidia kukiri mafanikio ya kisiasa na kidemokrasia ya Ghana. Inaonekana alichagua Ghana kwa alama yake ya kisiasa.

Alifanya ziara yake ya kwanza kwa nchi ambayo imekuwa na mabadiliko ya kidemokrasia ambayo kiongozi wa upinzani bwana John Atta Mills kutoka chama cha National Democratic Congress alishinda dhidi ya a Rais wa wakati huo ndugu John Kufuor wa chama cha New Patriotic Party.

Huo ni ujumbe wenye nguvu sana kwa jamii zingine za Kiafrika, na kwa viongozi wengine wa Kiafrika.

images (4).jpg


HAYA NI MANENO MACHACHE YA RAIS OBAMA ALIPOKUWA ANALIHUTUBIA BUNGE LA GHANA:
================
"Here in Ghana, you show us a face of Africa that is too often overlooked by a world that sees only tragedy or a need for charity. The people of Ghana have worked hard to put democracy on a firmer footing, with repeated peaceful transfers of power even in the wake of closely contested elections."

Ninaomba nisimuongelee ndugu John Atta Mills kwa maana yeye ni marehemu na kwa mila na desturi za kiafrika marehemu huwa hapaswi kusemwa vibaya.

Sasa juzi wakati ninasoma makala kadhaa hapa mtandaoni ndio nikakutana na hii scandal kubwa sana ya Airbus ya Rais John Mahama aliyechukua nafasi ya hayati John Atta Mills ambao wote walitokea chama kimoja cha kisiasa cha National Democratic Congress, ya wizi wa pesa kiasi cha £5million.

cdfgrfgfrfgbvf.jpg


Sasa kuanzia hapa nikajawa na maswali mengi sana kuliko majibu kwamba;

Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Do African Political Activists sincerely fight for Democratic Change or they simply keep alive a well-known old saying "It's Our Turn to Eat"?

NB
: Hii mada inalenga katika kuangazia mustakabali mzima wa demokrasia katika bara la Afrika, hivyo ninaomba tuepuke kabisa matusi, mabishano na malumbano ya CCM, CHADEMA, ACT-WAZALENDO, NCCR, CUF.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Demokrasia ya nchi zetu ilianzishwa ili kujipatia pesa kutoka kwa wahisani Kama ilivyokuwa kupata pesa za wahisani kwa njia ya kuweka watu lockdown kipindi Cha korona.

Huwa nawashangaa watu wanashabikia kwa kufuata mkumbo tangu nilivyogundua kuwa democracy ni fursa kwa watu Sina ushabiki wa kijinga kwenye masuala ya vyma vya siasa.​
 
Demokrasia ni muhimu lakini twaambiwa kwenye safari ya mamba kuna uweekano wa kuwa na kenge pia. Cha muhimu ni kuwa na katiba bora zinazo wezesha hawa jamaa kupelekwa mbele ya pilato ikibidi. Ni vizuri pia kuwa na wananchi wenye ufahamu na uwezo wa kudai haki zao.

Dunia nzima wapigaji wapo tofauti ni kwenye demokrasia halisi, institutions hufanya kazi yake kwingineko wanalindana. China kuna tofauti lakini wako wngi wanao jihisi hawako huru bali wahanga wa ukondoo wa uMao zeDong.
 
Safi sana kaka mkubwa.
Wanasiasa wanatakiwa kupigania katiba kwanza Mimi naamini katiba ikiwa vizuri ndiyo tutapata demokrasia ya kweli.

Sasa wao wanahubiri demokrasia wakati katiba zetu zimejaa makandokando mengi.

Hivyo wengi wao wanatimiza wajibu tu ili wapate ruzuku hakuna mwenye nia ya dhati ya kusaidia raia.

Ukitaka kujua pia hawa viongozi wapo kimasilahi jaribu kufuatilia katiba za vyama vyao vya siasa.

Katiba zao hazina tofauti na katiba ya nchi zimempa mamlaka makubwa mwenyekiti.

Ukionekana kwenda kinyume unaondolewa uanachama kama ulikuwa mbunge automatically unapoteza nafasi yako ya Ubunge.

Itoshe kusema ni ngumu sana kudefine African leadership. Kijana mwenzangu Infantry soldier tuendelee tu kuwa wazalendo na tuipende Nchi yetu.​
 
Demokrasia katika Afrika ni fursa za kupokezana ulaji au kuuza utu wa wengine kwa maslahi binafsi ya wachache.

Ili Afrika tuendelee tunahitaji kuondoa kabisa mirija ya ukoloni mamboleo. Hii itawezekana tu iwapo baadhi ya vifungu vya katiba za nchi wanachama wa AU vitabadilishwa ili kutoa nafasi kwa wapinzani kuwa sehemu ya tawala.
 
Aise Ghana ni nchi ya tofauti mno. Wale watu wamepiga hatua sana kwenye swala la demokrasia. Kule huruhusiwi kuvaa tishet la chama utembee barabarani kama siyo wakati wa uchaguzi. Mahakama ni huru kweli.
 
Ukitaka kujua pia hawa viongozi wapo kimasilahi jaribu kufuatilia katiba za vyama vyao vya siasa.
Sawa kabisa mkuu. Nitajaribu kufuatilia nizisome walau katiba za CHADEMA, CUF pamoja na ACT-WAZALENDO.

Katiba ya CCM ninayo hapa kwangu tangia zamani sana.
 
Back
Top Bottom