Je Wanafunzi wa Elimu ya Juu ni Wawekezaji au La?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Baanda ya kuanza sera ya uchangiaji gharama za masomo ya Elimu ya Juu, wanafunzi wa Elimu ya juu wamekuwa wakikopeshwa fedha kwa ajili ya gharamia masomo yao. Mkopo huo hutakiwa kuanza kurajeshwa mara baada ya mwanafunzi kuhitimu masomo na kuanza kutumia cheti alichopata kutokana na mkopo huo. Bodi ya mikopo ip mbioni kutaka kuwa inatoza riba kwenye mikopo hiyo ya masomo.

Kabla ya kwenda kwenye pointi yangu, ngoja nikosoe kwanza kidogo. Utaratibu huu haumwezeshi mwanafunzi ambaye amekopeshwa fedha lakini hakufanikiwa kuhitimu masomo yake kwa vile kigezo kikuu cha kumtambua kwamba huyu alikopeshwa, ni cheti cha kuhitimu masomo.

Hoja yangu y msingi ni kutaka tujadiliane iwapo wanafunzi wanaokopeshwa fedha za kugharamia masomo yao ya elimu ya juu wanaweza kujumuishwa kwenye kundi la wawekezaji au la. Na kama wanakidhi kuwemo kwenye kundi la wawekezaji, je wanastahili msamaha wa kodi katika mishahara yao kabla hawajamaliza marejesho ya mkopo huo kama ambavyo wawekezaji wa kwenye madini wanasamehewa kodi hadi pale wameanza kupata faida. Laiti kama fedha hizo wanafunzi wangekopa na kununulia hisa ni dhahiri kwamba wangetakiwa kukata kodi kutokana na gawiwo ambalo wangepata baada ya kampuni walikonunua hisa kupata faida.
 
Back
Top Bottom