Je wanadamu tuna FREE WILL??

Ndo maana me naonaga kuish ni kupoteza muda tu
Vipindi vya furaha ni vichache kuliko vya shida afu kumbe ni ramani ilishapangwa siku nyingi,WTF?
Si bora kufa tu ukaishi hayo maisha mengine tu ya kudumu kama kweli yapo
 
Hapa ndipo huwa naungana na Kiranga. Ishu ya Mungu kuandaa moto kwa ajili ya watakaotenda maovu naona inamuondolea sifa ya yeye kuwa na uwezo wote, upendo wote na huruma yote. Kwanini aumbe kiumbe dhaifu chenye kujidhibiti ili kisifanye dhambi. Kama ana uwezo wote si angetuumba wakamilifu tusio weza kutenda dhambi?

Halafu kuna logic gani ya yeye kumuachia shetani ataghiribu halafu tukiingia mtego wa shetani anatuchoma moto? Kwanini kamuachia huru shetani. Hata kitendo tu cha shetani kuasi maana yake aliumbwa na mapungufu maana laiti angekuwa mkamilifu asingeasi.

Hii ishu ya kuwa kuna moto umeandaliwa tayari inatufanya tusiwe huru. Wengi wanasema ni bora waamini mungu yupo ili wakienda wakimkuta isiwepo shida yoyote maana tayari waliamini, sasa hii sio imani huu ni woga! Je Mungu anapenda kuogopwa? Na kwanini anataka sisi tuwe tunamsifu tu kwani ana hofu gani? Uwezo wake si unafahamika? Endapo tusipomsifu uwezo wake utaadhirika na nini?

Kwanini tusali? Yaan tunasali ili iweje? Tunasali ili kiwe nini? Halafu mtu anakuambia tuna free will, kweli? Nisiposali nachomwa, duuh!!! Sasa hapo free will inatoka wapi?

Wanasema mungu ni mjuzi wa yote! Ikitokea ishu labda msiba wanasema ni mipango ya mungu sasa kwanini nikitenda dhambi isiwe mipango ya mungu? Kumbe mungu aliishapanga kila kitu, sasa free will hiyo inatoka wapi?

Yule Petro aliambiwa na yesu mwenyewe kuwa atamkana mara tatu na kweli Petro alishindwa kuruka hicho kiunzi na akamkana yesu mara tatu!! Yuda hakuwa free! Matendo yake yalikuwa yameishapangwa kitambo tena bila hata kushirikishwa...

BINAADAMU HATUNA FREE WILL
 
Benedict de Spinoza katika kitabu chake cha Tractatus; Theologico-Politicus anasema Deus sive Natura akimaanisha God or Nature chapter three nanukuu "Whether we say...that all things happen according to the laws of nature, or are ordered by the decree and direction of God, we say the same thing.".
Katika chapter 3 na 4 anachotaka kutueleza ni kwamba Mungu na "Nature" acha niite asili (nimekosa kiswahili chake) ni kitu kimoja kwamba kila amuzi unalofanya na unalopitia sio kwamba umeamua kulifanya eti kisa unalipenda bali ni sababu mazingira(nature) yanakushawish ulifanye!
the infant believes that it is by free will that it seeks the breast; the angry boy believes that by free will he wishes vengeance; the timid man thinks it is with free will he seeks flight; the drunkard believes that by a free command of his mind he speaks the things which when sober he wishes he had left unsaid. … All believe that they speak by a free command of the mind, whilst, in truth, they have no power to restrain the impulse which they have to speak.″. kila unachofanya kina ushawish na mazingira uliyopo lasivyo jiulize;
  • unaweza zuia kasirika, lia, cheka?
  • Unaweza zuia kuamua, mawazo?
  • Unaweza zuia hisia zako/ zikaact tofauti na unavyoishi siku zote?
Binadamu hatuna FREE WILL

Maoni yako mkuu yananiwazisha. Moja ya jambo muhimu ninaloona tunahitaji kuliweka sawa, je tuna mipaka ya ubinadamu? Hapa kuna maswali mengi, tukihusisha free will ya mwanadamu na mazingira. Hivi kama hakuna wanyama waliwao, mimea iliwayo na mwanadamu, au kwa ujumla tujiulize kusingekuwa na dunia inayosupport uhai, maisha yangekuwaje?

Hakika majibu yake ni mepesi sana. Moja ya majibu rahisi ni kuwa, lazima kungekuwa na namna ya kuishi, kama siyo duniani, basi kwingine na ni lazima kungekuwa na supportive mechanisms za kuishi.

Kwa hiyo?

Binadamu = Uhai + Mazingira, labda mie ninaona hivi. Yaani, unapomtazama binadamu hai, tambua anaundwa na components mbili, uhai na mazingira. Na labda tukitazama existance ya mtu kwa namna hii, pengine kwa maoni yangu, ninaweza sasa kusema, binadamu ana free will. Utashi upo kati ya uhai na mazingira. Kuna wakati utashi unahitaji kubadili mazingira ili kumaintain uhai. Nafikiri teknolojia ni mfano mzuri, tunaitumia kuboresha mazingira (kwa upande mmoja) ili kufanya ubinadamu kuwa bora zaidi. Ninafahamu matumizi mabaya ya teknolojia yanaweza kupelekea kupotea kwa uhai na hivyo kupotea kwa mazingira na mwisho kupotea kwa ubinadamu. Utashi wetu huweza kutupelekea mazingira kutuadhibu kutegemea na namna utashi unavyotafsiri mazingira.

Yanaweza kuwepo mazingira ya kucheka na mtu asicheke, kulia naye asilie, kukaa asikae, kuamua yeye asiamue, kutokuamua, yeye akaamua n.k

Tukumbuke, hakuna mazingira bila kuwepo kwa uhai na hakuna uhai bila mazingira. Kukiwepo na uhai na mazingira, ili mambo haya yaende barabara, ili kukamilisha ubinadamu, tunahitaji utashi.

Kwa hiyo, ikiwa tutatazama ubinadamu kwa components hizi tatu, ninaweza kusema kuwa, tuna Free will na hususani ukizingatia kuwa, utashi ambao ni kungo muhimu, hakipatikani kwenye mazingira, kipo zaidi kwenye ubinadamu. Kumbuka wanyama wengine wana uhai lakini hawana utashi, mimea ina uhai lakini haina utashi.

Asante mkuu kwa tafakari yako.
 
kama unasoma bible vizuri,sisi hatuna adhabu tena,Yesu katuokoa,,Kuna mstari unasema kwaajili ya mtu mmoja ulimwengu wote,umetenda dhambi,na kwa mtu mmoja wote tumeokolewa
Yesu alituokoa dhidi ya nani? Kwanini mungu aliumba mtu dhaifu ambaye anaweza kurubuniwa na shetani ambaye ameumbwa na huyo huyo mungu?

Yaani Eva ni kiumbe dhaifu na kama asingekuwa dhaifu basi asingeweza kurubuniwa, namaanisha Eva hakurubuniwa kwa utashi binafs bali ni kutokana na udhaifu wake na ndio aliumbwa hivyo. Sasa kosa la Eva likakipata kizazi chote kilichofuata! Halafu akaja yesu kufanya ukombozi, heeeh!!!! Suala la sisi kuadhibiwa kwa kosa la Eva yalikuwa ni matakwa ya mungu sasa yesu alikuja kutukomboa dhidi ya nani? Yesu alikuja kutukomboa kutoka kwenye adhabu iliyowekwa na mungu? Halafu eti yesu alitoka kwa mungu mwenyewe!!! Illogical kabisa!!! okay ina maana pale bustanini wakati mungu anaweka hiyo adhabu hakuona kuwa sio busara ila akaja akabaini hilo baadae sana ndio akamtuma yesu kuja kufuta hiyo adhabu, hii concept inapingana na sifa za mungu tunazopewa kuwa anajua lililopita, lililopo na hata lijalo.

NAAMINI MUNGU YUPO ILA HIVI VITABU VINATUPOTOSHA MAANA VINAJIPINGA VYENYEWE KUHUSIANA NA MUNGU.
 
Zimeisha ukisimama kwenye mstari wako wala huwezi kuzitumikia izo adhabu...
Siku hizi watu hawafi, hawazai kwa uchungu na wala wanaume hawali kwa jasho?

Adhabu hizi bado zipo sasa yesu alikuja kufanya nini?
 
Hapa ndipo huwa naungana na Kiranga. Ishu ya Mungu kuandaa moto kwa ajili ya watakaotenda maovu naona inamuondolea sifa ya yeye kuwa na uwezo wote, upendo wote na huruma yote. Kwanini aumbe kiumbe dhaifu chenye kujidhibiti ili kisifanye dhambi. Kama ana uwezo wote si angetuumba wakamilifu tusio weza kutenda dhambi?

Halafu kuna logic gani ya yeye kumuachia shetani ataghiribu halafu tukiingia mtego wa shetani anatuchoma moto? Kwanini kamuachia huru shetani. Hata kitendo tu cha shetani kuasi maana yake aliumbwa na mapungufu maana laiti angekuwa mkamilifu asingeasi.

Hii ishu ya kuwa kuna moto umeandaliwa tayari inatufanya tusiwe huru. Wengi wanasema ni bora waamini mungu yupo ili wakienda wakimkuta isiwepo shida yoyote maana tayari waliamini, sasa hii sio imani huu ni woga! Je Mungu anapenda kuogopwa? Na kwanini anataka sisi tuwe tunamsifu tu kwani ana hofu gani? Uwezo wake si unafahamika? Endapo tusipomsifu uwezo wake utaadhirika na nini?

Kwanini tusali? Yaan tunasali ili iweje? Tunasali ili kiwe nini? Halafu mtu anakuambia tuna free will, kweli? Nisiposali nachomwa, duuh!!! Sasa hapo free will inatoka wapi?

Wanasema mungu ni mjuzi wa yote! Ikitokea ishu labda msiba wanasema ni mipango ya mungu sasa kwanini nikitenda dhambi isiwe mipango ya mungu? Kumbe mungu aliishapanga kila kitu, sasa free will hiyo inatoka wapi?

Yule Petro aliambiwa na yesu mwenyewe kuwa atamkana mara tatu na kweli Petro alishindwa kuruka hicho kiunzi na akamkana yesu mara tatu!! Yuda hakuwa free! Matendo yake yalikuwa yameishapangwa kitambo tena bila hata kushirikishwa...

BINAADAMU HATUNA FREE WILL
Mkuu, Mungu ni mpaka tuliojiwekea sisi wenyewe na kisha tukaweka pia vigezo fulani ili watu waheshimu mpaka huo. Tumejijengea ukomo wa kufikiri. Yaani sawa na kujenga ukuta kuzungusha nyumba yako. Halafu ukaweka imani kuwa ukuta ule unaweza kila kitu. Yani kwa ulinzi, hapo ndio mwanzo na mwisho. Ukarelax, unapovamiwa (pata mateso, anguka kiuchumi, kuachwa na mpenzi, kushindwa mitihani n.k) unauuliza ukuta, kulikoni, na kisha unaanza kuuomba ukusaidie kuzuia wahalifu. Ni utumwa mbaya sana kuwahi kuushuhudia katika ulimwengu..

Kwa hiyo, Mungu ni dhana tuliyoijenga sisi wenyewe ili itupe ukomo wa kutenda na kufikiri. Ni sawa na Kizio, labda "Tesla" , meter, "Newton" n.k. Hivi vizio havipo mahali fulani kiasi kwamba ukihitaji Kani, basi uombe "Newton" ikusaidie na ijibu maombi yako. Ukiachilia mbali kuwa Newton ni jina la mwanasansi, je, unaweza kujibidisha kutafuta origin ya kizio "newton", kinaonekanaje, kinafanyaje kazi, kinaishi wapi, mbinguni labda, ardhini, kinawezaje kufanya Kani, n.k Tunapokosa majibu ya mwaswali haya tunasema, kweli "Newton" ni "uncreated creater". Utumwa mkubwa sana.

Mungu anachorwa kama kizio cha kueleza mabaya na mazuri, ni kipimo na haswa ni ukamilifu kama ilivyo, Newton. Hakuna namna kizio cha "Newton" kikawa na upungufu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na uhuru wa maisha. Hakuna mbingu nyingine zaidi ya kufurahia uhusiano wako mzuri na mazingira. uhusiano mzuri na watu, wanyama, mimea n,k. Tunahitaji uhuru huu. Hizi imani ni Mungu wa mbinguni ni utumwa mtakatifu.
 
Yesu alituokoa dhidi ya nani? Kwanini mungu aliumba mtu dhaifu ambaye anaweza kurubuniwa na shetani ambaye ameumbwa na huyo huyo mungu?

Yaani Eva ni kiumbe dhaifu na kama asingekuwa dhaifu basi asingeweza kurubuniwa, namaanisha Eva hakurubuniwa kwa utashi binafs bali ni kutokana na udhaifu wake na ndio aliumbwa hivyo. Sasa kosa la Eva likakipata kizazi chote kilichofuata! Halafu akaja yesu kufanya ukombozi, heeeh!!!! Suala la sisi kuadhibiwa kwa kosa la Eva yalikuwa ni matakwa ya mungu sasa yesu alikuja kutukomboa dhidi ya nani? Yesu alikuja kutukomboa kutoka kwenye adhabu iliyowekwa na mungu? Halafu eti yesu alitoka kwa mungu mwenyewe!!! Illogical kabisa!!! okay ina maana pale bustanini wakati mungu anaweka hiyo adhabu hakuona kuwa sio busara ila akaja akabaini hilo baadae sana ndio akamtuma yesu kuja kufuta hiyo adhabu, hii concept inapingana na sifa za mungu tunazopewa kuwa anajua lililopita, lililopo na hata lijalo.

NAAMINI MUNGU YUPO ILA HIVI VITABU VINATUPOTOSHA MAANA VINAJIPINGA VYENYEWE KUHUSIANA NA MUNGU.

Hahahaha, mkuu haya yote ukiangalia, kukosekana kwa logic ni makosa ya kawaida kabisa ya mwanadamu. Alishindwa kutengeneza flow nzuri ya mawazo ndio tumekuwa kwenye mkanyiko wa namna hii. Mungu ambaye tunamjua sifa zake ni mkamilifu, hana doa, nadhifu kabisa, ni upendo, n.k hawezi kufanya vitu vya kijinga hivi.
 
Ila bwana
Adhabu alizopewa adam na hawa juu ya uasi wao zimeisha?
Kula kwa taabu
Kuzaa kwa uchungu
Kifo....na mengine....
Ila haya mambo yanachanganya sana.

1. Mbona viumbe wote hawapati chakula kiurahisi!!

2. Je suala la kuzaa kwa uchungu ni binadamu tu au!!?

3. Je, ni binaadam tu anayekufa au!!?.
 
haya maswali nayoo
 
haya maswali nayoo
w
Ila bwana
Ila haya mambo yanachanganya sana.

1. Mbona viumbe wote hawapati chakula kiurahisi!!

2. Je suala la kuzaa kwa uchungu ni binadamu tu au!!?

3. Je, ni binaadam tu anayekufa au!!?.
wanasema simba zamani alikua sio mkali,Adam Alicheza na simba,ukiuliza zaidi wanasema kisichowezekana kwa mwanadamu,kwa mungu kinawezekana
 
Utana free will kwa sababu ata ujui kesho yetu ana ata ukifanya kosa ni dhambi wakati wewe umeamua na unaona sawa kwa upande wako
 
Mkuu, Mungu ni mpaka tuliojiwekea sisi wenyewe na kisha tukaweka pia vigezo fulani ili watu waheshimu mpaka huo. Tumejijengea ukomo wa kufikiri. Yaani sawa na kujenga ukuta kuzungusha nyumba yako. Halafu ukaweka imani kuwa ukuta ule unaweza kila kitu. Yani kwa ulinzi, hapo ndio mwanzo na mwisho. Ukarelax, unapovamiwa (pata mateso, anguka kiuchumi, kuachwa na mpenzi, kushindwa mitihani n.k) unauuliza ukuta, kulikoni, na kisha unaanza kuuomba ukusaidie kuzuia wahalifu. Ni utumwa mbaya sana kuwahi kuushuhudia katika ulimwengu..

Kwa hiyo, Mungu ni dhana tuliyoijenga sisi wenyewe ili itupe ukomo wa kutenda na kufikiri. Ni sawa na Kizio, labda "Tesla" , meter, "Newton" n.k. Hivi vizio havipo mahali fulani kiasi kwamba ukihitaji Kani, basi uombe "Newton" ikusaidie na ijibu maombi yako. Ukiachilia mbali kuwa Newton ni jina la mwanasansi, je, unaweza kujibidisha kutafuta origin ya kizio "newton", kinaonekanaje, kinafanyaje kazi, kinaishi wapi, mbinguni labda, ardhini, kinawezaje kufanya Kani, n.k Tunapokosa majibu ya mwaswali haya tunasema, kweli "Newton" ni "uncreated creater". Utumwa mkubwa sana.

Mungu anachorwa kama kizio cha kueleza mabaya na mazuri, ni kipimo na haswa ni ukamilifu kama ilivyo, Newton. Hakuna namna kizio cha "Newton" kikawa na upungufu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na uhuru wa maisha. Hakuna mbingu nyingine zaidi ya kufurahia uhusiano wako mzuri na mazingira. uhusiano mzuri na watu, wanyama, mimea n,k. Tunahitaji uhuru huu. Hizi imani ni Mungu wa mbinguni ni utumwa mtakatifu.
Mbaya zaidi kuna watu wameweka tabaka lao wengine wanajiita manabii, wengine wachungaji, mashekh na wengineo yaani hawa ndio wanajua kila kitu kuhusu mungu sasa hata wakiongea pumba hakuna wa kubisha maana wenyewe wanasema mungu anasema nasi kupitia wao.
 
Free will ipo mkuu na kila binaadamu anayo

Utakachoamua/kufikiria ndio matokeo ya baadae it's FREE WILL you gain what u deserve
 
Free will inakutuma uchague ubaya kweli!! Basi kama ni kweli kuna Pre - destination, Mungu alishapanga watu wake na wa shetani. Lakini angepanga watu wengi hivo wa shetani? Robo tatu ya dunia inaendeshwa na shetani, kila penye uzuri wa ajabu au utajiri shetani kakikita pale. Ngoja niwasogelee Atheists kwani wana jambo muhimu
 
Yesu alituokoa dhidi ya nani? Kwanini mungu aliumba mtu dhaifu ambaye anaweza kurubuniwa na shetani ambaye ameumbwa na huyo huyo mungu?

Yaani Eva ni kiumbe dhaifu na kama asingekuwa dhaifu basi asingeweza kurubuniwa, namaanisha Eva hakurubuniwa kwa utashi binafs bali ni kutokana na udhaifu wake na ndio aliumbwa hivyo. Sasa kosa la Eva likakipata kizazi chote kilichofuata! Halafu akaja yesu kufanya ukombozi, heeeh!!!! Suala la sisi kuadhibiwa kwa kosa la Eva yalikuwa ni matakwa ya mungu sasa yesu alikuja kutukomboa dhidi ya nani? Yesu alikuja kutukomboa kutoka kwenye adhabu iliyowekwa na mungu? Halafu eti yesu alitoka kwa mungu mwenyewe!!! Illogical kabisa!!! okay ina maana pale bustanini wakati mungu anaweka hiyo adhabu hakuona kuwa sio busara ila akaja akabaini hilo baadae sana ndio akamtuma yesu kuja kufuta hiyo adhabu, hii concept inapingana na sifa za mungu tunazopewa kuwa anajua lililopita, lililopo na hata lijalo.

NAAMINI MUNGU YUPO ILA HIVI VITABU VINATUPOTOSHA MAANA VINAJIPINGA VYENYEWE KUHUSIANA NA MUNGU.
Mkuu ukisoma Mwanzo 3 yote utaona ni tamaa na uzembe wa binadamu wenyewe tuu kwani Adamu alishaambiwa asile hilo tunda hata kabla ya Hawa kuumbwa toka ubavuni mwake. Soma Mwanzo 2:16-17 "Mwenyezi-Mungu alimwamuru mwanaume huyo, waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa"
Kwa hiyo kwa mujibu wa huo mstari hapo Adamu alikua keshaonywa hata kabla ya kuumbwa kwa Hawa.

Sasa mkuu nani mjinga? nani mwenye makosa? Mungu au Adamu?
...Adamu ndie mwenye makosa kwa sababu hakutii amri ya Mungu badala yake alisikiliza alichoambiwa na Hawa. Soma Mwanzo 3:11-12 "Mwenyezi-Mungu akamwuliza nani aliyekuambia uko uchi? Je umekula tunda la mti nililokuamuru usile? Huyo mwanaume akajibu mwanamke uliyenipa akae pamoja nami ndiye aliyenipa tunda la mti huo nami nikala"

Sasa mkuu unaanzaje kumlaumu Mungu wakati ni makosa ya Adamu? Tena Adamu ndie mpuuzi kwa sababu alimsikiliza mwanamke badala ya kumsikiliza Mungu wake, so mwanamke kwake alikua ni zaidi ya Mungu! dharau ilioje????

Na uzuri Hawa nae alikua anajua matunda ya mti fulani Mungu kakataza yasiliwe soma Mwanzo 3:2-3

Sasa mkuu kwa kifupi tuko hapa tulipo sababu ya uasi wa binadamu toka mwanzo!
Haya yote yanayotokea hayana budi kutokea. Mungu ni mwema siku zote, binadamu sababu ya tamaa zetu na kutoshika maandiko ndivyo vinatuponza. Ni lazima tujue uwepo wa Mungu, watu wengi wasiposhuhudia matendo makuu ya Mungu huwa hawaamini kwamba Mungu yupo.

Yes bado anatupenda ndio maana alimtoa mwanae wa pekee/Yesu aje kutukomboa lakini pamoja na yote hayo hamna kitu bado binadamu wanazidi kuasi. Soma vitabu vya Daniel na Ufunuo ujue hatma ya huu ulimwengu. Na ni lazima unabii utimie hata Yesu alikuja kutimiza unabii na kutukomboa toka kifungoni mwa shetani.

Nawashangaa sana watu mnaokaa hapa na kuanza kumshushia lawama Mungu wakati ni matokeo ya uasi wetu toka mwanzo.
 
everyone has free will; one can choose to do good, or evil. The ability to choose freely defines us as human beings; our choices define us as individuals. Freedom to choose is an essential and inherent right, but it is not absolute; there are consequences to actions.
 
Habari zenu wakuu,swali Hilo linanisumbua Sana,je Ni kweli tuna uwezo WA kuamua nini cha kufanya juu ya maisha yetu??je tuna uwezo WA kuchagua wema au ubaya??sio hatma yetu imeshaamriwa kabla??nimesoma thread ya member flani akizungumzia kisa cha Yuda na Yesu,je yuda alikua na free will au tayari ishapangwa aje amsaliti yesu???..karibuni..
Tuna free but not 100%... Our free will is only 75% the rest 25% is out of our control and is very powerful
 
Habari zenu wakuu,swali Hilo linanisumbua Sana,je Ni kweli tuna uwezo WA kuamua nini cha kufanya juu ya maisha yetu??je tuna uwezo WA kuchagua wema au ubaya??sio hatma yetu imeshaamriwa kabla??nimesoma thread ya member flani akizungumzia kisa cha Yuda na Yesu,je yuda alikua na free will au tayari ishapangwa aje amsaliti yesu???..karibuni..

Hakuna kitu inaitwa freewill,always kuna causality somewhere!

Hii Freewill ya kwenye bible ni pure lie na myth tu.

Mwanangu Sam Harris ka-debunk it left and right!

See him here:

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom