Je wanachadema tunatambua mzigo mkubwa waliotuvisha watanzania wenzetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wanachadema tunatambua mzigo mkubwa waliotuvisha watanzania wenzetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Mar 4, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010, baadhi ya wanachama, wapenzi na washabiki wa CHADEMA walionyesha wasiwasi kuhusu matayarisho yaliyokuwa yamefanywa kuhakiksha kuwa wizi wa kura unadhibitiwa, ili hatimaye wagombea waliosimamishwa na CHADEMA wapate kura halali walizopigiwa na watanzania.

  Kama ilivyo ada, wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA walijitokeza kupinga hoja hizo kwa nguvu sana. Lakini ukweli ulijidhihirisha kuwa wizi wa kura wa kutisha ulifanyika kutokana na wanachama, wapenzi, wapambe na washabiki wa CHADEMA kujirithisha tabia na mienendo ile ile ya CCM ya watu kushindwa kujitolea ipasavyo. Pale ambapo watu walijitolea vya kutosha wizi wa kura ulithibitiwa na wagombea wa CHADEMA kuibuka kidedea.

  Kwa mara ya kwanza CHADEMA imepata viti takribani 45 vya ubunge na kadhaa vya udiwani. Hii ni dhamana kubwa sana kutoka kwa wananchi ambao hawawezi kutofautisha kati ya Mbunge au Diwani asiye na mafungu ya fedha na Mkurugenzi wa Halmashauri mwenye mafungu, ambaye amebaki chini ya udhibiti wa Dola iliyoko chini ya CCM.

  Jambo moja lililo dhahiri ni kuwa watanzania wanataka kuchagua mtu anayeweza kuwa na kauli ya mwisho juu utatuzi wa matatizo yao. Ndio maana wameonyesha kwa vitendo wanataka mabadiliko. Na watu hao ni Mameya (Executive), Wakurugenzi wa Halmashauri n.k. Ndio pale inapokuja hoja ya mabadiliko ya Katiba.

  Jambo moja la hatari ninaloliona kutoka kwa wanachama, wapenzi, mashabiki na wapambe wa CHADEMA ni kuendelea na tabia na mifumo ya utendaji kazi wa kiCCM, yaani kuwa na kiwango kidogo sana cha kujitolea. Kama tunataka kuendeleza wimbi hili la wananchi kuendelea kuiamini CHADEMA, ni lazima kila mtu popote alipo ashiriki katika kutambua, kubuni, kupanga, kusimamia na kuratibu miradi ya kuondoa kero na shida za wananchi.

  Tukiendeleza tabia ya kungoja kila kitu kufanywa na viongozi wa chama, wabunge, madiwani n.k ni dhahiri kuwa watashindwa kukidhi matarajio ya wananchi walioipigia kura CHADEMA, na ushindi huo utakuwa mgumu sana kupatikana 2015. Hivyo kwa njia moja au nyingine tutakuwa tumekwamisha gurudumu la mabadiliko ha nchini.

  Wengi wetu ni wasomi ni lazima tuwe na utaratibu wa kutumia muda, elimu na kidogo tulichonacho kwa faida ya umma. Ndipo hapo umaa nao utatambua tofauti kubwa iliyopo kati ya mwanaCCM na mwanaCHADEMA na kuwa hapo CHADEMA will be there to stay. Tukishindwa kuwasiaidia wabunge na madiwani walioshinda na kushindwa kutatua kero za wananchi hata sisi tulioko kwenye reserve list hatutaweza kupata namba uwanjani kwa kuwa wananchi watashindwa kuipa CHADEMA hiyo nafasi tena.

   
Loading...