Je, wana CHADEMA wamemdharau Mwenyekiti wao Mbowe?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Nimejiuliza sana kuhusiana na kile kinaendelea nchini kuhusiana na suala la chanjo za korona!

Yaani kwa ufupi ni kuwa, kama CHADEMA ingekuwa kwa sasa madarakani, chanjo ya korona nchini ingekuwa ni LAZIMA kwa kila mwananchi nchini. Ikumbukwe kuwa, Mbowe wakati akiongea na vyombo vya habari tarehe 19 Julai 2021 alinukuliwa akisema, “serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iweke utaratibu mzuri wa chanjo kuwa ya LAZIMA kwa Watanzania”

Kama hukumsikia Mbowe akisema, gonga hii LINK kwenye gazeti la viongozi wa upinzani;

Bahati nzuri sana “Mwenyezi Mungu” alituepusha watanzania kuwa na viongozi serikalini wenye mawazo kama ya Freeman Mbowe katika maamuzi ya chanjo za korona.

Kinachoendelea kwa sasa nchini kuhusu chanjo za korona kinaonyesha hata wanachama wengi wa CHADEMA hawakubaliani na fikra za Mwenyekiti wao wa taifa.

Fikiria mpaka sasa ni Watanzania laki tatu na ushee pekee ambao wamejitokeza kwenda kupata chanjo za korona. Ieleweke kuwa kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na nusu tokea chanjo milioni 1.5 zianze kutolewa.

Tunaambiwa na viongozi wa CHADEMA kuwa CHADEMA ina wanachama milioni 7.

Ukijiuliza kati ya watu laki tatu na ushee waliojitokeza kwenda kupata chanjo ya korona ni wanachama wangapi wa CHADEMA ambao ni miongoni mwao?

Kinachoendelea katika zoezi la chanjo za korona kinaonyesha wana CHADEMA wengi wamempuuza Mwenyekiti wao wa Taifa kwenya suala la chanjo za korona.

Kama aliyekuwa Rais wa Tanzania, Magufuli aliwatia kasumba(brainwash) watanzania kwenye suala la chanjo za korona kama tunavyoambiwa na baadhi ya watu ina maana hata wana CHADEMA wengi walikubaliana na kasumba hiyo ambayo inadharau fikra za Mwenyekiti wao wa CHADEMA, Freeman Mbowe?

Kwa sasa tunaona baadhi ya viongozi wa CCM na serikali yake wakisaidiwa na bunge wameanza kutafuta “mbuzi wa kafara” baada ya zoezi la chanjo za korona kudoda ili baadaye watuambie zoezi limedoda kwa sababu ya Askofu Gwajima na Polepole kuwatia kasumba(brainwash) wananchi wengi nchini.

Je, Mbowe pia atamtafuta nani kuwa “mbuzi wa kafara” kwenye suala la chanjo ndani ya CHADEMA baada ya wazo lake kukataliwa na wanachama wengi ndani ya chama hasa ikichukuliwa alitueleza mara nyingi kuwa Rais Magufuli hana ushawishi mkubwa nchini achilia mbali kwa wana CHADEMA?

Kiufupi, chanjo za korona zimekataliwa na watanzania wengi nchini kwa sababu wananchi wameonyesha wanajitambua bila kujali wanachokitaka viongozi wao pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitaka kulifanya suala la korona kama la kisiasa.

Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wamepewa somo ambalo kama wana akili timamu watajifunza.

Juzi wananchi wa Kawe walimwambia Rais Samia “HATUCHANJI” baada ya kuwauliza kama wanachanja au hawachanji.
 
Nafikiri Chadema hawako kama hao wengine, kwamba zidumu fikra za Mwenyekiti.
Mimi sio Chadema kiviile lakini NIMECHANJA.
 
Acha porojo kwenye suala hili,kwa manufaa yako na manufaa ya taifa hili na kizazi kijacho, hutaki chanjo ni hiari yako acha mwenye hiari ya kuchanja afanye hivyo, ulimwengu uliostaarabika wanaheshimu mawazo ya kila mmoja. Usilete hapa weledi mpya wa kitanzania unaokosa ustaarabu.
 
Jamaa hii issue ya chanjo ya Corona naona ndio umeifanya mlango wako wa kutokea, naona hakuna kitu kingine kwenye ubongo wako kwa sasa.

Unajisifu wengi kutochanjwa, kwa hiyo ndio mmeshinda au? yule "hero" wako yuko wapi mkapewe kombe? ooh, yuko futi sita chini ya ardhi, wewe unamuita askari aliefia vitani, askari asiejua mbinu za kivita na silaha sahihi zakutumia akifia vitani ni uzembe, kama sio ujinga.

Kilichomuua? tukaambiwa moyo, na wale wasaidizi wake waliondolewa na nini? ok, labda moyo siku hizi unaambukiza!.

Mwenzio alituasa tufanye maombi, sijui wewe unakumbuka kuomba au ndio unajitutumua tu, au nyungu umejifukiza? hizi mbinu zenu za kishamba hata wewe huzikumbuki vuvuzela tu, nimekumbuka kitu, vipi yale mapapai yenu yenye Corona yalishapona au nayo yalifariki?
 
Acha porojo kwenye suala hili,kwa manufaa yako na manufaa ya taifa hili na kizazi kijacho, hutaki chanjo ni hiari yako acha mwenye hiari ya kuchanja afanye hivyo, ulimwengu uliostaarabika wanaheshimu mawazo ya kila mmoja. Usilete hapa weledi mpya wa kitanzania unaokosa ustaarabu.
Kama ulimwengu uliostaarabika wanaheshimu mawazo ya kila mmoja, mbona wewe unaonyesha kutoheshimu mawazo yake?
Unaposema asilete weledi mpya wa kitanzania unaokosa ustaarabu ni kutudharau watanzania wote, na kutuonyesha kuwa sisi siyo wastaarabu, isipokuwa wewe tu, au watu wenye mawazo kama yako. Too bad!
Fikiria kitu kwanza kabla ya kuandika.
 
Jamaa hii issue ya chanjo ya Corona naona ndio umeifanya mlango wako wa kutokea, hakuna kitu kingine kwenye ubongo wako kwa sasa.

Unajisifu wengi kutochanjwa, kwa hiyo ndio mmeshinda au? yule "hero" wako yuko wapi mkapewe kombe? ooh, yuko futi sita chini ya ardhi, kilichomuua, tukaambiwa moyo, na wale wasaidizi wake waliondolewa na nini? ok, labda moyo siku hizi unaambukiza!.

Mwenzio alituasa tufanye maombi, sijui wewe unakumbuka kuomba au ndio unajitutumua tu, au nyungu ulijifukiza? nimekumbuka kitu, vipi yale mapapai yenye Corona yalishapona au nayo yalifariki?
Huo umekuwa weledi wa wa Tanzania walio wengi kweye hii issue ya chanjo kama ulivyo kuwa weledi mpya wa kitanzania hii leo. Kwenye siasa, uhuru na haki za kikatiba na kisheria.
 
Kama ulimwengu uliostaarabika wanaheshimu mawazo ya kila mmoja, mbona wewe unaonyesha kutoheshimu mawazo yake?
Unaposema asilete weledi mpya wa kitanzania unaokosa ustaarabu ni kutudharau watanzania wote, na kutuonyesha kuwa sisi siyo wastaarabu, isipokuwa wewe tu, au watu wenye mawazo kama yako. Too bad!
Fikiria kitu kwanza kabla ya kuandika.
Wewe ni mmoja wa waumini wa huo ustaarabu mpya wa kitanzania hata wote waliostaarabika watashuhudia hilo,kama ni mmoja wa wale wanaofurahia manyanyaso,mateso,uonevu na uvujifu wa sheria na Katiba ya taifa letu,kwa kuwa uu mmoja ya wanufaika wa mfumo huo,ama kwa kukosa uelewa ,unataka nikuweke kundi gani?
 
Chadema ni chama cha kidikteta sana. Wanapenda sana kuweka vitu vya lazima na kutovumilia maoni tofauti.

Hata kwenye social media zao ukiwa na mawazo tofauti tu wana kublock. Wakishindwa kufanya hivyo ni kuporomosha matusi. Ndiyo hulka yao hiyo ya udikteta.

Tunajua kilichompata marehemu Chacha Wangwe alipompinga Mbowe. Kama unataka uwe huru kuamua mambo kwa uhuru , Chadema siyo chama muafaka kwako.
 
Wewe ni mmoja wa waumini wa huo ustaarabu mpya wa kitanzania hata wote waliostaarabika watashuhudia hilo,kama ni mmoja wa wale wanaofurahia manyanyaso,mateso,uonevu na uvujifu wa sheria na Katiba ya taifa letu,kwa kuwa uu mmoja ya wanufaika wa mfumo huo,ama kwa kukosa uelewa ,unataka nikuweke kundi gani?
Kama unadhani kwamba mawazo na misimamo yako pekee ndiyo kielelezo cha ustaarabu na mawazo ya wengine wote ni potofu, basi wewe ndiye kielelezo halisi cha kutostaarabika.
Umesema ustaarabu ni kuheshimiana kimawazo na kimitazamo, lakini bado unataka kulazimisha watu wote wawe na mawazo kama yako! Huko ni kuchanganyikiwa.
 
ivo tu yaaani
Tena ni aibu kwa picha hiyo kunathibishwa na mawazo , maoni na mitazamo ya viwango hivyo, kama mhusika ni mwenye picha hiyo, hii haija kaa vizuri, ila kama picha inatunika tu.Usikubali iendelee kutumika,tafuta mtumiaji mwingine angalau mwenye mtazamo unaoeleweka?Huo ni ushauri wabure,ushauri ni hiari kukubalika au kukataliwa.
 
Nafikiri Chadema hawako kama hao wengine, kwamba zidumu fikra za Mwenyekiti.
Mimi sio Chadema kiviile lakini NIMECHANJA.

Muundo wa CHADEMA kikatiba ni kama CCM. Tofauti ni kwamba CHADEMA hawajapata madaraka ya kuvisimamia vyombo vya ulinzi nchini!
 
Acha porojo kwenye suala hili,kwa manufaa yako na manufaa ya taifa hili na kizazi kijacho, hutaki chanjo ni hiari yako acha mwenye hiari ya kuchanja afanye hivyo, ulimwengu uliostaarabika wanaheshimu mawazo ya kila mmoja. Usilete hapa weledi mpya wa kitanzania unaokosa ustaarabu.

Hakuna mtu aliyekatazwa kwenda kuchanja!

Wewe kuniambia niache porojo huoni kuwa huheshimu mawazo yangu!

Halafu unaonyesha dharau kwa Watanzania kwa kusema hawajastaarabika!

Ustaarabu wako ni upi wakati umeshindwa kuonyesha kwenye huu mchango wako.
 
Wengi wamechanganyikiwa
Nimejiuliza sana kuhusiana na kile kinaendelea nchini kuhusiana na suala la chanjo za korona!

Yaani kwa ufupi ni kuwa, kama CHADEMA ingekuwa kwa sasa madarakani, chanjo ya korona nchini ingekuwa ni LAZIMA kwa kila mwananchi nchini. Ikumbukwe kuwa, Mbowe wakati akiongea na vyombo vya habari tarehe 19 Julai 2021 alinukuliwa akisema, “serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iweke utaratibu mzuri wa chanjo kuwa ya LAZIMA kwa Watanzania”

Kama hukumsikia Mbowe akisema, gonga hii LINK kwenye gazeti la viongozi wa upinzani;

Bahati nzuri sana “Mwenyezi Mungu” alituepusha watanzania kuwa na viongozi serikalini wenye mawazo kama ya Freeman Mbowe katika maamuzi ya chanjo za korona.

Kinachoendelea kwa sasa nchini kuhusu chanjo za korona kinaonyesha hata wanachama wengi wa CHADEMA hawakubaliani na fikra za Mwenyekiti wao wa taifa.

Fikiria mpaka sasa ni Watanzania laki tatu na ushee pekee ambao wamejitokeza kwenda kupata chanjo za korona. Ieleweke kuwa kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na nusu tokea chanjo milioni 1.5 zianze kutolewa.

Tunaambiwa na viongozi wa CHADEMA kuwa CHADEMA ina wanachama milioni 7.

Ukijiuliza kati ya watu laki tatu na ushee waliojitokeza kwenda kupata chanjo ya korona ni wanachama wangapi wa CHADEMA ambao ni miongoni mwao?

Kinachoendelea katika zoezi la chanjo za korona kinaonyesha wana CHADEMA wengi wamempuuza Mwenyekiti wao wa Taifa kwenya suala la chanjo za korona.

Kama aliyekuwa Rais wa Tanzania, Magufuli aliwatia kasumba(brainwash) watanzania kwenye suala la chanjo za korona kama tunavyoambiwa na baadhi ya watu ina maana hata wana CHADEMA wengi walikubaliana na kasumba hiyo ambayo inadharau fikra za Mwenyekiti wao wa CHADEMA, Freeman Mbowe?

Kwa sasa tunaona baadhi ya viongozi wa CCM na serikali yake wakisaidiwa na bunge wameanza kutafuta “mbuzi wa kafara” baada ya zoezi la chanjo za korona kudoda ili baadaye watuambie zoezi limedoda kwa sababu ya Askofu Gwajima na Polepole kuwatia kasumba(brainwash) wananchi wengi nchini.

Je, Mbowe pia atamtafuta nani kuwa “mbuzi wa kafara” kwenye suala la chanjo ndani ya CHADEMA baada ya wazo lake kukataliwa na wanachama wengi ndani ya chama hasa ikichukuliwa alitueleza mara nyingi kuwa Rais Magufuli hana ushawishi mkubwa nchini achilia mbali kwa wana CHADEMA?

Kiufupi, chanjo za korona zimekataliwa na watanzania wengi nchini kwa sababu wananchi wameonyesha wanajitambua bila kujali wanachokitaka viongozi wao pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walitaka kulifanya suala la korona kama la kisiasa.

Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wamepewa somo ambalo kama wana akili timamu watajifunza.

Juzi wananchi wa Kawe walimwambia Rais Samia “HATUCHANJI” baada ya kuwauliza kama wanachanja au hawachanji.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom