Je, wameondoa vibao vya mwendokasi kuzidi?

Kuna kimoja ukimaliza wami tu nacho kimetolewa au huu msimu wa mvua vibao vingne vinafunikwa na nyasi kama huna uzoefu unapigwa mkono kila mara
 
Ukiona cha kuruhusu upande kinzani jua upande wako cha kuzuia wamekitoa vinginevyo utapigwa tochi na kubaki unajiuliza hii ni wapi!
mkuu hawa askari hovyo kabisa, kuna siku kaniambia nimeover speed, akanionesha picha ilibaki kidogo nikubali ile kucheki vizuri gari zinafanana rangi na ukubwa ila sio gari yangu.... hata hakubisha akaniacha niende. Sema tuu umakini ndio unahitajika
 
Kuna kimoja ukimaliza wami tu nacho kimetolewa au huu msimu wa mvua vibao vingne vinafunikwa na nyasi kama huna uzoefu unapigwa mkono kila mara
True kuna ambavyo vimefunikwa na majani...lakini jamaa ndio wanavizia hivi hivi
 
mkuu hawa askari hovyo kabisa, kuna siku kaniambia nimeover speed, akanionesha picha ilibaki kidogo nikubali ile kucheki vizuri gari zinafanana rangi na ukubwa ila sio gari yangu.... hata hakubisha akaniacha niende. Sema tuu umakini ndio unahitajika
Mchezo huu wanao sana kama Una haraka unaliwa!
 
Nilishawahi kutana na jambo kama hilo.

Siku hiyo nimetoka arusha kama saa 4 asubuhi, nimefuata vibao vyote toka arusha mjini mpaka njia panda ya himo...
Wanakupotezea muda kusudi wanajua utaboreka tu na hutaki kupoteza muda.
 
Ukiwakomalia hawakufanyi kitu. Walileta huu ujinga Dar mkubwa wao akasema hakuna kitu kama hicho.
Hili ndio jibu la huu Uzi mkuu

Mimi mpaka leo msimamo wangu ni ule ule na kuna thread kadhaa nilichangia humu kuhusiana na hizi faini za Overspending kwa kutumia picha za watsapp.

Msimamo ni kwamba sitoi leseni na sikubali kuandikiwa(Kukomaa/kubisha) mpaka trafiki anionyeshe hiyo sehemu physically. Anioneneshe picha(kutoka kwenye kamera sio simu) na anionyeshe nilipokua na kibao cha kukataza(Ila uwe tayari kulala lockup/kupoteza muda).

Huu ujinga wameuanza upya tokea mwezi February/March nadhani.

Na wanachukulia udhaifu wa kuwa watu wengi hatupendi usumbufu na kupotezewa muda unakubali kuandikiwa.

Mimi nilianza huu ubishi katikati ya March njia ya Dar-Arusha mpaka saivi naona unanisaidia japokua napotezewa muda sana ila ukikomaa MAHAKAMANI HAWAKUBALI KUKUPELEKA.
 
Hili ndio jibu la huu Uzi mkuu

Mimi mpaka leo msimamo wangu ni ule ule na kuna thread kadhaa nilichangia humu kuhusiana na hizi faini za Overspending kwa kutumia picha za watsapp...
Shida ni hapo uliposema kupoteza muda...na wanajua hatupendi kupoteza muda.
 
Utajuaje kama ni hicho kibao bila kuingia ndani ya hamsini?
Kwani wewe kwenye hamsini unaingia na mia? Ukiona kibao unapunguza mwendo hadi 50kph ndio tunachoshauri hapa.
 
Utajuaje kama ni hicho kibao bila kuingia ndani ya hamsini?
Ni suala la uzoefu tu kutokana na kuendesha sana kwenye Highways za Bongo...

Hapo juu nimeeleza mazingira yanayopelekea kujua kwamba sasa unaingia kwenye speed limit ya 50 hata kama kibao kimetolewa...
 
True kuna mazingira yake ikiwemo rasta kabla ya matuta...ingawa sio maeneo yote
 
Je ushawahi kupigwa tochi ambayo huielewi? Yaani umefuata vibao vyote vizuri kabisa lakini unafika mbele unaoneshwa picha kwenye 50kph zone imepita na 85kph au zaidi?...
Yaani hiki alichoandika RRONDO kinataka kufanana na hiki kilichowakuta wananchi..
FB_IMG_16152303194118970.jpg
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom