Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

Wale mabaunsa wakatafute kazi ya ulinzi kwenye makampuni ya ulinzi hasa wale wa chama. Samia atalindwa na wanawake wenzake. Madume ya nini hata akose raha? Ajifunze toka kwa Gadaffi kuwa wadada wanaweza. Kiutendaji na uadilifu ajifunze kwa Angela Merkel.
Hivi hujawahi jua hao 'bodyguards' au "mabaunsa" ka usemavyo ni polisi special wa kazi ile na hata iwe rais hayuko tena, basi wale jamaa hupewa position zingine tofauti kila mmoja kwenye kitengo cha usalama kwa sababu bado ni askari na hawajafikia ku retire. Madame rais Samia anapewa team yake mpya ya ulinzi atakayokuwa nayo kipindi kile atakuwa ofisini. Na lazma yule askari jeshi anayesimama nyuma ya rais wakati wote, pahala popote, awe mwanamke sababu rais ni mke pia, hiyo ndio taratibu ya security ya rais nchi nyingi.
✌️
 
Kama kuna kazi yenye raha na hata changamoto ni hiyo ya kuwa right hand wa rais, raha tu pale, yaani kama rais wa nchi ni mtu wa kutembea nje ya nchi sana, basi wewe dunia utajua kama vile mtaa wako, kila sehemu uko naye, kila chakula uta experience, lugha tofauti za watu utazitabua hata kama kwa kiasi tu,ata connection utajitengenezea mwenyewe ukiwa msharp, ndio maana right hand wa rais wengi huwa wamesoma sana na wana mafunzo hataree
✌️
 
Pamoja na ulinzi woooote, nilichokua namkubali Magu, na yeye alikua hakosi ka mguu ka kuku kiunoni, ili ikitokea hali imekua mbaya basi atajitetea mwenyewe, hiki nadhani ni kitu kigeni kwa marais wetu waliopita, sidhani kama ben wala kikwete kati yao kuna mtu alikua anatembea na mguu wa kuku.

Mara nyinga siku akibeba mguu wa kuku alikua anavaa koti halafu halifungi vifungo
Mbwembwe tu asingeweza ata kuiwasha bastola.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiitifaki wanatakiwa wafanye hivyo Kwake kwakuwa ndiyo walikuwa assigned Kwake kama Walinzi. Hata katika Msiba wa Hayati Nyerere Walinzi wake akina Mzee Mkanzabi, Tendewa, Marehemu Mzee Simon Mohammed na Wengineo Wanne walifanya hivyo Kwake.

Baada tu ya Maziko ( Mazishi ) na Wao watapangiwa Majukumu mengine ya Kiidara hapo Makao au Mikoani au hata Nje kuwa attached katika Missions ( Balozi ) kwa Kazi Maaalum chini ya Mabalozi watakaowakuta huko.
Mzee Mkanzabi ndiye mwenye wanae Oliva Mkanzabi , ambaye ni wakili ?
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom