Je, Wakurugenzi na Maafisa Utumishi walichukua hatua gani kuhusu watumishi hewa kabla ya Mh Rais?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Hodi humu ndani!

Kuna wakurugenzi, maafisa utumishi na waajiri kwenye taasisi na idara mbalimbali za serikali ambazo kumekutwa na watumishi hewa na wale wenye vyeti vya kugushi, hawa nao walitimiza wajibu wao kabla ya Mh Rais na Waziri kuingilia kati mchakato huu? Walichukua hatua gani wakiwa ofisini? Hawakuona haya madudu?

Hao ndo ambao wamekuwa wakicertify nyaraka za watumishi hao hewa, kuithinisha mikopo, fedha za likizo, fedha za uhamisho, kupanda vyeo na madaraja. Na haohao ndo wamekuwa wakiwathibitisha wafanyakazi serikalini mwaka mmoja baada ya kuajiliwa.

HAWA NAO WALIWAFANYA KAZI YAO AU NAO NI HEWA?

Haiwezekani mtu wan je aje kukwambia kwamba chini ya kitanda chako kuna uchafu, safisha.Haiwezekani!

Natambua Mh Rais ana nia nzuri na serikalini yake na watu wake wanyonge, tunakuomba uwatazame hawa wakuu wa idara, wakurugenzi na maafisa utumishi ambao kwakweli wameleta hiimkasumba wao wenyewe. Hapakuwa na haja ya wao kukusubiri were Mh Rais.

Huku mtaani hekaheka kila kona. Watu wanahaha na familia zao, wanabeba magodoro, wanauza viwanja, wanauza magari, ugomvi ndani ya familia, stress za kila aina, ada za watoto sasa taabu, ndugu wanarudishwa vijijini kulima.

Hili swala liangaliwe kwa mapana yake. Likate kote kote.

Asanteni sana.
 
Hao huwa wanachukua order kutoka uongozi wa juu yao.

Mfano, maafisa elimu wenyewe walijambishwa haswa na kuna baadhi ya maafisa utumishi walitumbuliwa.
 
Dyu!! Mkuu 9932 hawajatosha! Bado unataka na wengine waondoke!!
 
walikuwa wazembe Sana
maafisa utumishi ni miongoni mwa watendaji wazembe kuwahi kutokea huwexi amini asilimia kubwa ya majina yenye utata. vyeti feki wanajua

Mkuu huwezi amni walikuwa wanashirikiana kutengeneza hewa Na Leo feki

Wilaya ya [HASHTAG]#Lushoto[/HASHTAG] wanahusika kwa hili
 
Kuna Wilaya hadi watumishi 300 vyeti feki
. Mhh,kazi ipo.
 
Mchwa wa nchi hii ni Hatari sana ukienda kwa Wakuu wa Idara ndiyo utalia kabisa chini ya Mkurugenzi wa Wilaya au Halmashauri au Municipal.

Yaani Rais Magufuli ana kazi ngumu mno na bila kupata support ya kila mpenda maendeleo ya nchi hii kuna watu wanaoeneza sumu ya kumlaumu kila siku ili tu Maslahi yao ya kuwaibia watanzania yasiguswe.

Rais Magufuli ana nia nzuri sana na watanzania na kila siku anasema tumeibiwa sana Sasa ifike Mwisho. Mwenye akili na atambue usemi huu
 
Kwa Dar, Ilala imetia fora. Wapo 330!
Ila nilichojifunza, watumishi tunatakiwa tujizoeshe mifumo mingine ya kujipatia kipato cha ziada nje ya ajira. Watumishi wengi wataathirika kwa kuwa hawakuwa na namna mbadala ya kipato.
 
Back
Top Bottom