Je Wakulima wa Tumbaku wanapata Value For Money | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wakulima wa Tumbaku wanapata Value For Money

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by August, Nov 23, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu ninaomba tujadili hili suala, maana lina madhara kwa Mazingira, yaani ukataji wa Miti, na Hali za Affya za Wakulima Wenyewe, ninaona wanaofaidika zaidi ni Watu wa Nje labda na Serikali Bila Kujali hali ya Wahisika au kuwasaidikia wahusika kwa Madhara wanayo pata Kiafya na kimazingira.
  Na miundo mbinu au ndio Janja ya Serikali kuwafanya wawe watumwa wao wa Kudumu?

  'Tumbaku inadhuru lakini muhimu'
  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 3rd November 2009 @ 21:00 Imesomwa na watu: 225; Jumla ya maoni: 1 Kutokas Gazeti la Habarileo

  SERIKALI inatambua madhara ya tumbaku kwa watumiaji lakini inathamini umuhimu wa zao hilo kwa uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi.

  Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk Mathayo David, amesema bungeni kuwa, hawezi kuchagua kati ya uchumi na afya za wananchi kwa kuwa vyote hivyo ni muhimu.

  Dk David amelieza Bunge mjini Dodoma kuwa, ushuru wa sigara una faida kiuchumi lakini matumizi ya tumbaku yanaathiri afya za watumiaji ikiwa ni pamoja na kuwasabishia saratani ya mapafu, kinywa, koo, shingo ya mfuko wa uzazi, magonjwa ya moyo, na kuziba mishipa ya damu.

  Kwa mujibu wa Dk David, Serikali haina mpango wa kuwafanya wakulima wa tumbaku wasilitegemee zao hilo na inashirikiana na wadau kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

  Amesema, asilimia 85 ya tumbaku inayozalishwa nchini inauzwa nje ya nchi, na asilimia 15 inatumika nchini. Dk Mathayo amewaeleza wabunge kwamba, katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imekusanya sh bilioni 340 kutokana na kodi mbalimbali katika zao la tumbaku.

  "Wakulima katika maeneo yanayozalisha tumbaku wanayo hiyari kuzalisha mazao mengine ambayo yana uwezo wa kuwapatia faida au kipato" amesema Dk David wakati anajibu swali la Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa.

  Mnyaa amedai bungeni kuwa, tumbaku inasababisha wagonjwa wapya 40,000 wa saratani kila mwaka hivyo aliiuliza Serikali kama imefanya utafiti kupima faida wanayoipata kwa ushuru unaotozwa kwenye sigara na madhara wanayopata watanzania.

  Kwa mujibu wa Dk David, Serikali inapata Sh bilioni 100 kwa mwaka kutokana na kodi ya sigara, watanzania 500, 000 wamejiajiri kwenye kilimo cha tumbaku, na pia kaya 92,000 zinategemea zao la tumbaku.

  Amesema pia kwamba, kilimo cha tumbaku hakiathiri ardhi, kinairutubisha.
   
Loading...