Je, Wakili Albert Msando anafaa ubunge wa Arusha Mjini?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,233
Wakulungwa na wajuba salaam!

Ingawa hajatangaza hadharani nia yake ya kugombea ubunge wa Arusha mjini, pengine hana hiyo nia ama anayo anaogopa kuambiwa ameanza kampeni mapema.

Ikizingatiwa kuwa kipyenga cha ubunge CCM hakijapulizwa, kama Mwanasheria Msomi Albert Msando akitangaza nia ya kugombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CCM ashindane na Godbless Lema vipi atafaa? Ataweza kumshinda Lema?

Hivi karibuni amekuwa akionesha ishara fulani hivi kama vile anautaka ubunge hivi, mfano hivi karibuni amekuwa akitoa misaada mbalimbali e.g msaada wake wa barakoa kwa wanahabari Arusha, pia amekuwa akipost negative kuhusu Lema na CHADEMA e.g juzi hapa alisambaza clip akidai ni ya Lema akimsimanga Lissu.

NB: Sijahitimisha kuwa atagombea ila mfano akagombea na akapitishwa na CCM na hata baadaye kuchaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mjini vipi atafaaa?
 
Aliyewahi kuwa Diwani huko Moshi na mshirika wa masuala ya kisheria kuna tetesi za kulitaka jimbo hilo kupitia CCM.

Ikumbukwe ni hivi karibuni Wakili Msando alitoa misaada ya vitakasa mikono na barakoa ktk janga la corona na baadaye jeshi la polisi kumtia ndani kwa kile watu walichodai ni maelekezo ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo kwa madai ni "maelekezo toka juu" kabla ya aliye juu kuamuru iwe hivyo kwa watakaogawa Barakoa.

Msando mwenye uzoefu wa sheria Takribani miaka 12 sasa na aliyeishi CHADEMA, ACT Wazalendo na sasa CCM
ni wazi ana uzoefu na masuala ya siasa

20200702_182410.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom