Je, wakati tunajiandaa kuingia katika Uchaguzi Mkuu, CHADEMA Ikiwa katika vipande vipande Mbowe bado Mtu sahihi?

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Wakuu tumebakiwa na mda mchache kabla ya kipyenga cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kupulizwa, Tumeshuhudia CHADEMA ikigawanyika katika vipande vipande na kusababisha vijana makini waliowanoa kwa miaka mingi kukihama chama hiki.

CHADEMA iliundwa na Vijana makini waliokua wamejengeka kisiasa na walikua wanawavutia wengi ambao wanachama na si wanachama vijana hawa wote wameondoka ndani ya Chama na Kukiacha kikiwa kipopo.

Wabunge wengi wameondoka kwa kutaja bayana maamuzi mabaya ndani ya chama ambaoy Mheshimiwa Mbowe amekua akiyatoa kwa kushirikiana na wahuni wachache wanaomuunga mkono.

Nini kifanyike CHADEMA inahitaji reforms kuelekea Oktoba 2020 au wasubiri uchaguzi wa 2025?

Je Mbowe bado mtu sahihi wa kuendelea kukiongoza Chama?

Vipi rasimu ya mabadiliko ya katiba ya kikundi cha Chadema yatapokelewa kweli kwenye kikao cha Halmashauri kuu kama ikiwa inakinzana na yeye hasa michango ya wabunge ambayo labda ndiyo inayomfanya asiachie ngazi?

CF598778-621B-42C4-9287-AD57BC9732B8.jpeg
 
Back
Top Bottom