Rangi ya mkojo wako inasema nini kuhusu afya yako?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,110
Mwili una mifumo mbalimbali ambayo hushirikiana kwa karibu katika ufanyaji kazi. Mara nyingi matatizo katika mfumo fulani huweza kuonekana katika mabadiliko kadhaa ya kimwili ambayo huweza kuonekana nje ya mwili.

Mkojo ni moja ya viashiria vya matatizo mbalimbali mwilini hasa matatizo katika mfumo wa mkojo.

Zifuatazo ni rangi za mkojo na maana zake katika Afya ya mhusika.

1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi)
Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo
Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyopauka
Upo kawaida tu

UrineColor.jpg


4. Njano iliyokolea
Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji baada ya muda mfupi

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali
Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia
Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kama hali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Machungwa yaliyoiva
Una upungufu wa maji mwilini au uwezekano wa matatizo katika ini au mfuko wa nyongo hivyo umuone daktari. Inaweza kutokana na rangi ya chakula pia(food dye).

8. Rangi ya bluu au kijani
Inaweza kusababishwa na rangi za chakula, athari za dawa au ishara ya maambukizi ya bakteria. Muone daktari endapo itaendelea kwa muda mrefu.

9. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu
Kama hujala matunda yoyote nyenye asili ya uwekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugonjwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.

10. Mkojo wenye mapovu
Inaweza kuwa ishara ya matatizo ya figo au protini zilizozidi mwilini. Muone daktari endapo inakutokea mara kwa mara.

11. Rangi nyingine(ukiondoa zilizotajwa juu)
Inaweza kusababishwa na rangi za chakula, dawa au kemikali nyingine. Kama huna uhakika ni vyema kumuona daktari.
 
Mkuu tunashukuru kwa haya maelezo kuhusu rangi ya mkojo.

Harufu kali ya mkojo nayo huwa inasababishwa na nini?
 
Ni muhimu kuhakikisha kuwa unakunywa maji ya kutosha kuanzia asubuhi mpaka jioni, na hii ifanyike kila siku. anza taratibu baada ya muda utazoea.
 
Mkuu tunashukuru kwa haya maelezo kuhusu rangi ya mkojo.

Harufu kali ya mkojo nayo huwa inasababishwa na nini?
Ni Dalili mojawapo ya UTI, hasa kwa wajawazito, mkojo wenye harufu kali, baadae utaanza kusikia maumivu wakati wa kukojoa.Ningelikushauri uende kumuona Daktari haraka iwezekanavyo.
 
habari zenu wakuu kiukweli hichi kitu kinaniumiza kichwa sana yani nilienda hospital kwa ajili ya vipimo vya vidonda vya tumbo lkn kwa bahat nzuri sikuwa navyo ila nasikia maumivu ya tumbo hvyo nikagewa dawa lkn tang nimeanza ktumia hizi dawa aiseeh inanichangany sana...mkojo wangu umebadilika langi imekuja langi ambayo cjawahi kuiona tang nianze kukujoa mpka naanza kushikwa na wasiwasi aiseeh ...mdamwngine naisi lbda inaweza ikawa dawa hiz ila bado cjapata jibu la kutosha hvy naomba mwnye uelewa wa hili sual jamni anisaidie au hata ushauri mna ata sielewi nifanyeje.........NAWASILISHA
 
Ni kawaida. Ni kazi ya ini kusafisha damu na dawa huchujwa na kuvunjwa na kupelekwa kwenye figo na kutolewa nje kwa njia ya mkojo ndiyo maana dawa unakunywa kwa dozi kila baada ya muda fulani ili kuhakikisha kiasi fulani kipo kwenye damu ambacho huweza kufanya kazi.

Labda utuambie kama unapata dalili nyingne ukiachana na mkojo kubadilika rangi kwa sababu siyo kitu cha ajabu.

Pia ungesema dawa gani alikuandikia daktari
 
nashukuru mkuu.....kuusu dalili nyingine ni kwamba nakunywa au natumia dozi lkni nikinywa tuun dawa basi tumbo nalo linaanza visa yan kuuma na baada mda linaacha alaf lnaanza tena ndio mtindo wake uo....pia nikitembea huwa haliumi ila nikiwa nimekaa tuu yan lbda kupumzika basi nalo linaanza kuuma .....Pia kwa upande wa Dawa nimepewa dawa fulan zinaitwa REBOLIC na nyingine ya kunywa ambayo inaitwa RELCER GEL.... na hii dawa pia yab RELCER inanishangaza sna kwani kwa baahati mbaya lbda ikinimwagikia kwnye mkono basi huwa ni kma rangin hiz za kupaka yan mpka nikawa nais unaweza ukawa unakunywa dawa kumbe ni rangi inaenda kukuumiza na EXP DATE ni 2016 na pia MFG 2012 ......nisaidie mkuu
 
Ni kawaida. Ni kazi ya ini kusafisha damu na dawa huchujwa na kuvunjwa na kupelekwa kwenye figo na kutolewa nje kwa njia ya mkojo ndiyo maana dawa unakunywa kwa dozi kila baada ya muda fulani ili kuhakikisha kiasi fulani kipo kwenye damu ambacho huweza kufanya kazi.

Labda utuambie kama unapata dalili nyingne ukiachana na mkojo kubadilika rangi kwa sababu siyo kitu cha ajabu.

Pia ungesema dawa gani alikuandikia daktari

mkuu vip
 
1. Rangi nyeupe
Una maji ya kutosha mwilini.

2. Rangi ya njano iliyofifia au nyeupe yenye unjano kwa mbali
Una maji mwilini yanaelekea kupungua.

3. Rangi ya njano au kahawia
Huna maji mwilini.

4. Rangi ya damu
Una maambukizi nyemelezi au ugonjwa wa zinaa.

Kazi ya maji ni kama mafuta kwenye gari unahitaji maji kila siku kwa vile ni kinga na tiba pamoja na kutoa sumu.
 
mkuu naomba kuuliza. Wakati wa baridi sometimes naweza nsinywe maji na mkojo ukatoka mweupe peeh! so hapo kitaalam inakuaje? akati siku za joto nsipokunywa maji mkojo unatoka wa njano
 
watu wengine wanakojoa mkojo mweupe ila wakienda hospital bado utakuta wamewekewa drip

magonjwa yapo mengi yasiyhusisna na mkojo kama moyo.kichwa. tumbo. maralia na nk magonjwa kama ya figo au yananaendana na damu ndio ysnahisiana na mkojo
 
mkuu naomba kuuliza. Wakati wa baridi sometimes naweza nsinywe maji na mkojo ukatoka mweupe peeh! so hapo kitaalam inakuaje? akati siku za joto nsipokunywa maji mkojo unatoka wa njano

kila mwilo una tabia za kureact kupambana na hali flan kama allerg na nk mwili wako inawezekana hautimii maji meng wakati wa barid
 
Back
Top Bottom