Je, wajua walivyopishana mitazamo "Haki za bindamu"?

David Jesus

Member
Jul 14, 2021
18
45
JE, WAJUWA WALIVYOPISHANA MITAZAMO "HAKI ZA BINDAMU" ?

Awali ya yote nitangulize shukrani kwa Mungu ambaye anatulinda na kutuhifadhi sisi binadamu tulio watu wake maana yeye ndiye mwamuzi wa maisha yetu Usiku na mchana.

Lifuatalo ni shukrani zangu kwako msomaji na mfuatiliaji Mwenye UTU na UBINADAMU katika kuona haki na thamani ya Binadamu mwezako zina zingatiwa.

Tuanze wote pamoja namna hii katika kuleta mtazamo chanya na kuona kila mtu ana haki ya kuishi, kula, kucheza, kusoma, kusikilizwa, kulindwa, kuwa kiongozi, kuheshimiwa, kupendwa/Kupenda, kutoa mawazo/mchango wowote wa kifikra au kimawazo juu ya jambo fulani, haki ya kushiriki shughulu za kijamii n.k

Kipindi hiki cha miaka hii ya karibuni kumetokea sintofahamu kwa maadhi ya matukio ya Ajabu sana yakitukia na yanayofanywa na binadamu mpaka unaanza kujiuliza, Hivi kweli aliyefanya hivi ni binadamu mwenye akili timamu kumfanyia mwenzake hivi kweli...!.?

Katika swala zima la haki za binadamu ni jambo ambalo kila mmoja anatarajia kuishi kulingana na haki hizo,
Ila sasa kuna watu majina yao wasiojulikana wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu kwa binadamu wenzao matukio ya ajabu ajabu kweli ambayo hayafai kumfanyia binadamu mwenzako.

Mfano 1: KUNA NDUGU ZETU WENYE MATATIZO YA ULEMAVU (ngozi/albino, wenye upungufuwa kiungo/viungo) Watu hawa wamekuwa wakiishi kwa mashaka kama siyo binadamu kama wengine.

Jambo hili limeenea mahali pengi sana tena likisemekana lina husiano na imani za kishirikina kwamba mtu akichukuwa kiungo cha Albino atapata utajiri, kwa hiyo wamekuwa wakiwavizia watu na kutoa viungo vyao bila huruma huku wakimsababishia mwenzao maumivu, ulemavu, na pengine hadi kupoteza maisha kutokana na kunyofoa/kukata viuongo vya mwili wa vya binadamu mwenzao.

Jambo hili limekuwa linaharibu kabisa na kuleta sura/picha ya unyanyaswaji au ukiukwaji wa Haki za binadamu tena ni ukatili ambao unatakiwa tuupinge kwa nguvuv zote huku tukiwafichuwa wanaoleta manyanyaso kwa watu wa ulemavu. Maana tambuwa hata wewe ni bindamu kama huyo unayemfanyia hivyo, tena ipo siku utakuja kupata mtoto akiwa Albino je utajisikiaje kama akifanyiwa unacjokifanya?

"Tuungane kuwafichuwa wanaotenda unyanyadaji ili kuutokomeza unyanyasaji huu"
Sambamba na hilo la unyanyasaji kwa watu wa Ualbino kuna watu WENYE UPUNGUFU WA KIONGO/VIUNGO vya mwili.
-Kundi hili nalo limekuwa likisahaulika na kutokupewa nafasi katika nyanja/sekta mbalimbali katika kuleta maendeleo. Lakini wanahesabiwa ni watu wasio na uwezo wa utendaji, usimamiaji, uendeshaji, hata katika kutoa hoja au mawazo katika Jamii, kaya, familia zetu na maeneo mbalimbali.

Kwa kujuwa au kutokujuwa ni kuvunja haki za binadamu kabisa na kuwafanya wajisikie na kujiona kuwa wao kumbe siyo watu wa muhimu katika jamii na kitu kibaya zaidi kuwabatiza majina ya ajabu ajabu kulingana na ulemavu wao hili kwakweli tulipinge kwa nguvu zote, Hata kutoa taarifa kwenye madawati ya haki za binadamu. Mitizamo mibaya kama hii niyakukemewa kabisa, tambuwa kuwa kundi hili lina haki kama mwanadamu mwingine katika kuongoza, kutawala, utendaji katika sekta binafsi na serikali kusimamia shughuli za maendeleo, kutoa mchango wa mawazo n.k

Unayefanya unyanyasaji huu ebu Acha Mara moja ipo siku yatakuja kukupata na wewe utaingia kwenye kundi la ulemavu kama wao, tuwalinde, tuwaheshimu, na kuwathamini. Na katika hili tuna mifanyo ya viongozi wazuri sana ambao ni walemavu na wenye uwezo wa kusimamia mambo na yakaenda vizuri, tuna walimu wazuri tu. Na tunapotoa ajira basi tuangalie usawa/haki Za binadamu.

"Kuungane kukemea n kufichuwa wanyanyasaji katika kuleta haki sawa"

Mfano wa 2: WANAWAKE
-Kundi hili pia limekuwa kwenye wahanga sana wa kutokupata haki zao kwa kuonekana kwamba haliwezi kufanya vizuri katika sekta au nyanja mbalimbali sababu wao ni wanawake tu.

NA WANAWAKE WAMECHUKULIWA KWA MTAZAMO HUU

FB_IMG_16145639285549614.jpg


Mfano unapozungumzia mambo ya kuwa kiongozi na kusimamia mambo fulani imani ya watu inakuwa ndogo kweli mpaka inapekekea kunyimwa nyazifa za juu kutokana na dhana ya kwamba hawana uwezo wa mamuzi katika nyanja za uendeshaji/usimamizi wa mambo mbalimbali. Na jambo hili limepelekea mpaka kwenye sekta ya uchumi kupitia viwanda vyenye mitambo mikubwa na shughuli fulani kutokupata nafasi, kuchagua wazo la mwanamke na kukubaliwa, kutoa maamuzi kama msuluhishaji, n.k ni asilimia ndogo sana kwako waliopo kwenye hizo nafasi.

•Njoo kwa upande wa madhehemu au dini WAO WANA MTAZAMO GANI JUU YA HAKI YA BINADAMU kwa MWANAMKE?

-Hapa napo kumekuwa na mitazamo tofauti, Dini "X" inasema wao wawawezikuwapa nafasi wanawake kuongoza Yani wawejuu ya wanaume Maana Mara zote maamuzi yao nitofauti tena wanakukuu na kwenye kitabu chao cha Imani yao kwamba mwanamke ni wakuongozwa na si kuongoza, tena anatakiwa kukaa ndani na kuletewa mahitaji, Maana akifanya shughuli za kuongoza kipato atakuwa na jehuri kwa mumewe na tena ni rahisi kushawishika na kumkosea mmewe hivyo anatakiwa tu kutulia.

Dini ya pili "Z" hiyo nayo miongoni mwao kumekuwa na matabaka mawili katika utekelezaki wa haki za binadamu kwa mwanamke.

{A} Wapo wanaosema hapaswi mwanamke kuongoza, kuhubiri, kuwa Mchungaji, Nabii, Mwalimu, Mwinjilisti na Mtume Maana yeye siyo nafasi yake na wala siyo kichwa cha familia na uwezo wake ni mdogo katika kupambanua mambo na wametohoa kwenye KITABU chao cha Imani yao ambacho ni muongozo wao(Yesu alikuwa na wanafunzi wanaume tu). Na hii misingi wanafundishwa tangu wakiwa wanahudhulia mafundisho yao. Huo ndio mtazamo wao.

{B} Na kundi lingine katika Dini "Z", Mtazamo wao ni kwamba, wanatambuwa Haki za binadamu kwa mwanamke anapaswa kuwa kiongozi wa nafasi ya juu kama kuhubiri, kuwa Mchungaji, Nabii, Mwalimu, Mwinjilisti na Mtume; Maana katika kuamini kwao kwamba yeyote aliyefanyika kuwa mwanafunzi wa Yesu basi atambue anauwezo wa kuwa mtumishi katika ngazi yeyote. Maana hakuna utofauti katika utendaji na wote wanauwezo huo maadamu tu awe vizuri na Mungu tu. Na wao kulingana na mwongozo wa KITABU chao cha Imani na ndivyo wanavyoamini.

NB: katika kundi hili kumekuwa na asilimia ndogo za wanawake katika utumishi kulingana na sababu ambazo zimekuwa zikiwabana kulingana na jinsia yao.

Mfamo 3: WATOTO ni watu ambao wamekuwa hawanga sana Maana hawana watu wa kuwawakilisha na kuwatetea ndio Maana wanakutwa na mambo ya kutisha na yakusikitisha kwakweli.

FB_IMG_16099075334392613.jpg


Watoto ndio kundi ambalo linaongoza kwa kuvunjiwa haki za binadamu, tena kuanzia kwenye familia (utasikia kesi za kupigwa mtoto mpaka majeraha,kuvunjwa kiungo,kuchomwa moto, kujeruhiwa kwa vitu vya ncha Kali,ubakaji,ulawiti), koo, jamii, taasisi binafsi na serikali, kwa sehemu wanaonewa sana na kwakuwa wanaonekana wana maumbo madogo wanafanyiwa chochote kwa kutekwa, kulazimishwa, kutumiwa kwa jambo baya, kunyimwa kucheza, kuchomwa moto, kuuwawa, kufanyishwa kazi ngumu chini ya umri wake, kupigwa kupitiliza kwa hasira tena hakuna sehemu maalumu inayoangaliwa kwa kumchapa Bali ametekeleza hadhima yake ya kumchapa. Mtoto hapaswi kunyimwa kucheza,kulindwa, kusoma, kutoa mawazo, adhabu kwa kiasi.

Mfano 4: WAZEE - Kundi hili limekuwa tegemezi kwa sehemu na lisipoangaliwa au kujaliwa tunapoteza kabisa kumbukumbu na sehemu ya kupata historia za nyuma/zamani. Kundi ambalo halijawekewa kipaumbele kwa kuwa wazee na hawana nguvu sana kulingana na miaka yao na miili kuchoka. Wanahitaji kuangaliwa, kusikiliza, kutunzwa mfano kuna wazee walikuwa tangia kupigania Uhuru wengine wamefariki bila kupata haki zao za malipo na wengine wapo hai wanafuatilia mpaka leo ingawa ilitakiwa kuwa ni sehemu ya uangalizi mzuri na kupatiwa haki zao, kupata ulinzi maana baadhi ya maeneo wazee wanauwawa kulingana na ITIKADI za pale kwamba akionekana na macho mekundu ni ishara kuwa ni mchawi.

TAMATI YANGU
"Haki za Binadamu yeyote bila kuangalia hali yake"
1. KUSOMA/KUPATA ELIMU, 2. KUTOA MAONI NA KUSIKILIZWA, 3. KUISHI, 4. KUHESHIMIWA, 5. KULINDWA, 6. KUPATIWA MATIBABU, 7. KUCHEZA n.k

(kama wewe unaapenda kutendewa vyema ebu mtendee na mwingine vyema na pia tuungane kutoa taarifa na kupinga na kufichuwa vitendo vya UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom