Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Swali la msingi hapa ni hili.

Unakubali kwamba CCM imeharibu sana uchaguzi na kuiba kura sana na hivyo matokeo ya uchaguzi huu ni batili?

Tafadhali jibu kama Mtanzania anayependa haki, na si kada anayetetea chama chake tu.
Mkuu Kiranga , uchaguzi hauendeshwi na CCM, unaendeshwa na NEC ambayo ni Tume huru ya uchaguzi japo sio Shirikishi!.

Kitu ambacho nakubali ni CCM imapiga kampeni kubwa safi na chafu, iliyofanya CCM ikubalike sana na upinzani ukataliwe. Mfano baadhi ya sisi makada wazalendo wa CCM, hatukuunga mkono zile kauli za vitisho kuwa mkichagua upinzani, maendeleo mtaishia kuyasikia, ni kauli za kibaguzi, ila Watanzania wamezikubali, wakaichagua CCM na kuwapiga chini wapinzani.

Sina uthibitisho wowote wa CCM kuiba kura zozote, hivyo despite dosari ndogo ndogo za hapa na pale, uchaguzi ulikuwa huru na haki na walioshinda wameshinda kihalali na kwa haki, walioshindwa wameshindwa kihalali na kwa haki kwa kukataliwa, the winner takes it all the loser standing small, it's simple and its plain, why should you complain?.

Na baada ya matokeo hayo ya wapinzani kukataliwa, tsunami ya CCM imekuwa too big kiasi italiathiri Bunge letu, ndio maana nimeshauri wapinzani wahurumiwe tuu ili Bunge letu lipate kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
P
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,695
2,000
Public interest ya vyama inaanzia pale serekali na vyombo vyake inapoiacha democrasia ya wananchi ichukue mkondo wake.Inapokua tofauti na hapo tayari huo unakua ni ujinga mwingine ambao kamwe hauwezi kuvifanya vyama vikawa na public interest.Sasa unakosea sana unapowaza vyama kupata ruzuku alafu unajisahaulisha kua vyama ni muunganiko wa wananchi wanaotakiwa kuiishi democrasia.sasa kama democrasia imebanwa au kuingiliwa kwa namna yoyote ile hivyo vyama vinakua nikama haviko kwamaana yakutekeleza majukumu yake kupitia hao wawakilishi unaotaka wewe wawepo ili chama kipate ruzuku.Sasa hizi sio zama zakua na vyama jina ilimradi tu vinapata ruzuku.Vinginevyo inakua haileti maana kua na nchi yenye katiba inayotambua vyama vingi.
 

mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,934
2,000
mwanzo nilidhani malalamiko ya wapinzani kuibiwa kura yana ukweli ndani yake but juzi nilipokua nafuatilia sakata la ndugu ambae ni miongoni mwa walokamatwa ajili ya vurugu za uchaguzi ndo nikaujua ukweli wa mambo...

police walitumia mbinu ya kutaka kitambulisho cha mpiga kura ili kubaini kama walokamatwa wamepiga kura au wanatumika vibaya kisiasa bt cha ajabu
zaidi ya 80% ya waliokamatwa hawana kitambulisho cha mpiga kura akiwemo ndugu yangu, kwa mantiki hii upinzani unapaswa kujitafakari na kuchukua hatua madhubuti kama wanataka kuwa washindani wa kweli wa chama tawala na sio kufanya siasa za majitaka ajili ya maslahi yao.
Huna lolote gamba wew
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,540
2,000
Paskali,
Unawaambia Chadema waache ubinafsi,ignorance ,insanity,selfishness.Je unawaambai CCM nao waache nini?
Binafsi ,I am tired,my heart is down kwa niliyoyaona na kuyasikia katika uchaguzi huu.
Mtu yoyote aliyeshiriki katika haya yaliyotokea ndiye ambaye anatakiwa kukemewa.
Chadema inaelekea kufa kama NCCR mageuzi na demokrasia inarudi chini.Mwaka jana tumevuruga serikali za mitaa na mwaka huu tuna bunge la Chama kimoja.
Bunge likae chini libadilishe kanuni na ikiwezekana katiba maisha yaendelee.
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
9,996
2,000
Mkuu yuzazifu , asante kwa hoja hii, upinzani Tanzania ni michosho sana, ukiwaeleza ukweli wanakuwa wakali, tunawashauri upinzani wa kweli ni upinzani Bungeni na kule ni kushindana kwa hoja, lakini hawasikii.

Sasa wananchi wamewakataa, wanakuja na visingizio kibao.

P
Pascal Mayalla wewe ni akili kubwa , una uhakika wananchi wamewakataaa wapinzani kabisa ? Tusiongee kwa ushabili , tuangalie tumeanguka wapi ili tutoe ushauri mzuri ...wewe katika kalamu yako hata ndani ya roho yako najua unaumia kwa yanayoendelea nchini ...
Mimi binafsi naumia sana sana na siamini ...naongea kama Mtanzania Mzalendo ...hii hali sio ya kawaida ..Ukweli usemwe
 

Don Nzoko

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
230
250
Walipobana matamasha yako ukipiga kelele hukutaka kuiangalia interest ya wengine leo umerudishiwa kelele zmekuwa nyingi, pathetic
 

Koffi Yardley

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
553
500
Anko P-
Well provocative as usual and again, the coded message is by the lines, in between them. The intrinsic stuff is for the expert.

That said, you got me into this dichotomy selection of appropriate entries into matters of PRINCIPLE and as you assert, of PUBLIC INTEREST! Very relative.

But then one might also say, when you want to reap MAHINDI, the seeds remain essentially MAHINDI. Corresponding husbandry of that crop remains, kimahindi.
Else you are bonkers, albeit UNPRINCIPLED to your own f×××××g interests as a member of same PUBLIC domain.
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,540
2,000
Pascal Mayalla wewe ni akili kubwa , una uhakika wananchi wamewakataaa wapinzani kabisa ? Tusiongee kwa ushabili , tuangalie tumeanguka wapi ili tutoe ushauri mzuri ...wewe katika kalamu yako hata ndani ya roho yako najua unaumia kwa yanayoendelea nchini ...
Mimi binafsi naumia sana sana na siamini ...naongea kama Mtanzania Mzalendo ...hii hali sio ya kawaida ..Ukweli usemwe
Umenena ukweli.Mimi ni mwana CCM wa kadi ya kusomea (unasoma miezi mitatu na unapewa kadi),JKT mwaka mzima tukifundwa uzalendo na kuipenda nchi yetu.
Ukweli tumejivuruga wenyewe.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,778
2,000
Kwa jinsi uchaguzi wa mwaka huu ulivyoendeshwa na kuja kuletewa matokeo yenye mashaka mengi, ni dhahiri kabisa kuwa uongozi wa taifa wa chama tawala umefilisika mno kifikra na kimaono. Hiki kinachoitwa kuwa ni CCM mpya, si chochote wala lolote lile zaidi ya genge la watu waliopoteza dira na muelekeo.
tapatalk_jpeg_1557319509156.jpg
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
9,996
2,000
Umenena ukweli.Mimi ni mwana CCM wa kadi ya kusomea (unasoma miezi mitatu na unapewa kadi),JKT mwaka mzima tukifundwa uzalendo na kuipenda nchi yetu.
Ukweli tumejivuruga wenyewe.
Kabisa mafunzo ya uzalendo miezi mitatu ....bado JKT na vita vya ukombozi ...alafu ukitoa maoni hapa watu wanakuchukulia poaaaa ....tatizo hapa kuna vijana wakati tunakata issues hapa miaka ya 2000s ndio walikuwa wanazaliwa , siku hizi hatuna uzalendo wala mawazo chanya .....nikikumbuka enzi zile tamko dogo tu la waziri wa elimu kesho yake anakutana na umati wa vijana 5,000 kila mmoja kafika kwa njia yake ofisini kwake .....leo vijana wamekua toooo soft soft soft badi laana .....umeona wapi vijana wadogo wanashindwa hata kuhoji mambo ya kawaida..tunajenga kizazi gani .....hata viongozi baadhi tulionao walijenga ujasiri na uwezo wa kuwa critical wakiwa vijana ....leo tuna vijana walamba miguuu kwa hofu ya tumbo .....hawana kazi wapooo tu hata hawawezi kuhoji na kushauri wanadanganyika ....shaaaame vijana wa leo
 

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,279
2,000
Wanabodi,

JF ni ukumbi huru wa kuhabarishana, kuelimishana, kuburudishana, na kitu kikubwa zaidi, kusaidiana. Kama kuna kitu unakijua, na unaona kinafanyika ndivyo sivyo, unajitolea kusaidia, na hiki ndicho ninachofanya hapa, kwa kuendelea na zile makala zangu elimishi kuhusu Maslahi ya Taifa.

Declaration of Interest
Mimi ni kada wa chama cha siasa, ila ninapoandika hapa, siandiki kama kada, bali naandika kama Mtanzania Mzalendo, ukinisoma with preconceived kuwa huyu ni kada wa chama fulani, hutaweza kuiona rationale ya bandiko hili, hivyo nakushauri bara uishie hapa.

Vyama vya Siasa Tanzania ni Public Parties
Japo vyama vya siasa ni mali ya wanachama na kuhudumiwa na michango ya wanachama, kwa Tanzania, vyama vya siasa ni private parties vya wanachama, wakati wa kuanzishwa tuu, lakini vikiisha ingia kushiriki uchaguzi na kushinda, status ya vyama hivyo ina change from private parties za wanachama into public parties za umma na ndio maana vinalipwa ruzuku ya serikali. Fedha za serikali ni public money, yoyote anayelipwa by taxpayers money ni public entity, kufuatia viongozi wa vyama hivyo kuchaguliwa na wananchi, the public, to hold a public office, serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, walio wachagua ni public ya Watanzania na sio wanachama wao pekee, hivyo hivi vyama vyote vya siasa vyenye viongozi waliochaguliwa na wananchi ni public parties.

Kufuatia status hii ya vyama vya siasa kuwa ni public parties, then maamuzi yoyote ya chama kuhusu uchaguzi, lazima yazingatie the public interest na sio the selfish motives ya viongozi wake wajinga wajinga kutokana na bitterness ya kushindwa kwenye sanduku la kura, kwa kujiaminisha walishinda hivyo wamepokwa ushindi!.

Miongoni mwa walioshinda, ni baadhi ya wapinzani. Inasemekana vyama vyao vimepanga kuwazuia kuwatumikia wananchi waliowachagua!. Huu ni ujinga uliopitiliza!.

Japo mgombea lazima adhaminiwe na chama cha siasa kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, kwa maoni yangu, udhamini una lengo zuri la kupata viongozi safi, lakini pia huu ni ujinga na ni kinyume cha katiba, japo ujinga huu sasa umehalalishwa na kuchomekewa ndani katiba yetu kinyume cha dhamira ya mtunga katiba.

Lakini huyo mgombea akiisha chaguliwa kwa kura za wananchi kuwa kiongozi, status yake ina change from mdhaminiwa wa chama cha siasa into a public service, kiongozi huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio mgombea wa chama. Uwezo wa chama cha siasa kumfukuza uanachama mwanachama wake ambaye ni kiongozi wa umma, bila kosa lolote, au kosa lake ni yeye kuchaguliwa kuongoza eneo lake, wakati vigogo wa chama chake wameshindwa na kupigwa chini na wananchi wao, huu ni ujinga na kutowatendea haki wananchi wa eneo husika walio onyesha imani yao kwa mgombea huyo na kumchagua!.

Baadhi ya Viongozi wa Vyama ni Insane, Hawajui Watendalo!
Wanabodi, naomba kutanguliza kuomba radhi kwa haya ninayoyaandika kuhusu baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa ni insane bila ya wao kujijua they are insane, ila ni kweli baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ni insane na utawajua kwa mawazo yao, maneno yao na matendo yao. Kuna kauli za ajabu ajabu zinatolewa na baadhi ya viongozi wetu, mtu hadi unajiuliza kama vingozi hawa wana akili timamu!

Ili kuielewa hii dhana ya viongozi insane, katibu hapa ili umjue insane ni nani na utamtambuaje na kumtofautisha na mtu mwenye akili zake timamu.


Insanity Inawapataje Viongozi wa Siasa?.
Kama nilivyoeleza pale juu, mtu kuwa insane ni hali tuu, kwa Kiswahili kizuri ni kughafilika. Mtu unaweza kuwa timamu kabisa, lakini ukatibuliwa na jambo fulani, ukachukua maamuzi ya hamaki, hasira na kufanya kitendo ambacho sio cha kawaida sometimes hata kuua!, halafu ukiisha tulia, ndipo unajiuliza umefanya nini na kuanza kuujutia uamuzi wako.

Lengo la chama cha siasa, ni kushika dola, hivyo viongozi wanaogombea nafasi mbali mbali kwa lengo la kushika dola (urais), kushika jimbo (ubunge), kata (udiwani), na mitaa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sasa katika kugombea, kukijitokeza umati mkubwa wa watu katika mikutano yako, kunakupa matumaini ya kukubalika, hivyo mgombea unakuwa na too great expectation ya kushinda, kumbe ni just some false hopes, hivyo uchaguzi ukifanyika, matokeo yakaonyesha umeshindwa, unapagawa, unachanganyikiwa unakuwa huamini matokeo, hivyo unaghafilika, unarukwa na akili, una despair, hiyo hali inakusababishia hali inayoitwa preudo insanity, hivyo unatoa maamuzi ya ajabu ajabu, kwanza ni hatua ya kwanza inaitwa denial, hukubali matokeo, unaamini ulishinda ukaibiwa kura, hivyo una wabibilize wafuasi wako muingie barabarani!, this is insanity kutaka kuwafolenisha watu kuwaingiza barabarani ili iweje?.

Hatua ya pili ni kutoa taarifa kuwa hukubali matokeo, hii ni kawaida kwa kila asiyakubali kushindwa. Hatua ya tatu ni kusema huwatambui walioshinda. Unaweza usiwatambue kwa muda, lakini walioshinda wakiisha apishwa, kutowatambua ni muendelezo wa insanity!. Hatua ya nne ni kususa, na kutaka kuwazuia wengine walioshinda kihalali, au kususia kutoa ushirikiano kwa walioshinda, kama hili la kugomea kutoa majina ya wabunge wa viti maalum!

Kuna wanaoshindwa na kubakia kuwa stable, lakini kuna wanaoshindwa na kuchanganyikiwa hadi kurukwa akili, sasa hawa walioshindwa na kurukwa akili wakitoa maamuzi ya ajabu ajabu, wenye akili timamu mkiwafuata, wote mtaonekana insane!

Mtu Kuwa Insane Sio Kosa, ni Hali Tuu, Lakini Kikundi cha Watu, Chama, Kikao au Wanachama Wote Kukubali Kufuata Ushauri wa Isane, Wote Mtaonekana Insane!. Wale Wasio Insane, Wasikubali Maamuzi ya Isane!.
Uchaguzi umekwisha, walioshinda, wameshinda, walioshindwa wameshindwa, zipo taarifa za baadhi ya viongozi walioshindwa kutaka kuwazioa walioshinda wasitumikie wananchi waliowachagua!, this is insanity!.

Kuna taarifa za chama fulani kugomea kuteua wabunge wa viti maalum kwa hoja za kususu, this too is insanity!.

Wito wangu kwenye hivyo vyama, kama kuna viongozi ambao sio insane, please stop this madness ndani ya vyama vyenu, vinginevyo wote mtaonekana ni insane!.

Jee Kila Uamuzi wa Kugomea Jambo au Kususia Kitu ni Ujinga, Insane?
Hapana, sio kila kugomea jambo au kususia jambo fulani ni ujinga. Kugomea jambo fulani ili kutuma ujumbe mzito kwa watawala, kuwa this is not right, kunakubalika, hivyo maandamano ya kutuma ujumbe, demonstrations au industrial actions kwa wafanyakazi, kudai haki zao, ni migomo halali na ina justification kwa ajili ya kutimiza malengo fulani.

Kipimo cha kususia jambo fulani au kugomea fulani, kipi ni uamuzi sahihi na kipi ni ujinga na uendawazi, ni kipimo cha kutumia matokeo, jee ukigomea jambo fulani, una goma ili kuachive nini?, kama unagoma tuu ili mradi kugoma, au unasusa tuu ili mradi kususa, kwa kugoma huko, huta achieve anything, huku ndio kugoma kwa ujinga na uendawazimu, viongozi wa vyama wanaohimiza vyama vyao kusasa huku na kugoma huku ambapo there is nothing they'll achieve kwa kususa huko au kugoma huko, huu ndio uendawazimu ninaouzungumza hapa!.


Huwezi kususa kumtambua rais wa nchi- huu ni uendawazimu. Mgombea ameshinda, huwezi kumzuia asitumikie wananchi walio mchagua- huu ni uendawazimu. Chama kinastahili kupata idadi fulani ya wabunge wa viti maalum, kugoma kupeleka majina NEC ni uendawazimu, unasusa ili iweje?.

Hitimisho.
Kwa vile vyama vya siasa ni public parties, viongozi wa vyama, mna wajibu wa kuviendesha vyama vyenu kwa kutanguliza mbele maslahi ya umma na sio maslahi binafsi ya viongozi wenu, msiruhusu ignorance, insanity, selfishness ya baadhi ya viongozi wenu wabinafsi, kuviangamiza vyama vyenu kwa ignorance, insanity, selfishness yao, wakati miongoni mwenu sio wote mko insane.

ACT Wazalendo, acheni ujinga wa ignorance, insanity, selfishness ya viongozi wenu insane!, pelekeni jina la Makamo wa Kwanza wa Rais kwa Dr. Mwinyi!

Chadema acheni ujinga wa ignorance, insanity, selfishness ya viongozi wenu insane!, pelekeni majina ya maalum NEC
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Chadema acheni ujinga wa ignorance, insanity, selfishness ya viongozi wenu insane!, pelekeni majina ya maalum NEC
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali.....hapo acheni ujinga wa ignorance ndo nini mbona unaoneka umepanic kimwili na kiakili na kiroho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom