Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Kwani wewe ulipata kura ngapi kwenye kura za maoni?
Mkuu Mhdiwani , mimi nilipata kura mbili tulikuwa wagombea 176, hivyo nikijitathmini nilivyo jiandaa kwa uchaguzi huo, investment niliyowekeza, na kura nilizopata, kiukweli kura mbili ni nyingi sana, haswa kwa kuzingatia kuna wengine wengi tuu, hawakupata kura kabisa!.
P
 
Ila kwa kuwa nakuheshimu sana dingi ila ningekupa kubwa kuliko .

Kiufupi ACT na CHADEMA wamegoma kuwa sehemu ya uhalamia na hawawezi kuhalalisha uhuni

Kama waliona umuhimu wao upinzani kwanini wameporwa ushindi
 
Hili jamaaa linajiona lina haki ya ujuaji wa kuwasema wengine kumbe ni lipuuzi fulan kutoka Lumumba....hata hvyo mh amesema hateui tena wew endelea na upuuzi wako wa kutafuta sifa kwa sbb unajua ulichoandika ndicho wanachokipenda maccm wenzio
 
CHADEMA wamesema uchaguzi ulikua batili na si halali, kwaio kupeleka wabunge wa viti maalumu huko ni kuhalalisha wizi uliofanyika na kwenda kinyume na matamko yao ya awali.

Pili Raisi wetu mpendwa alishasema wapinzani wanachelewesha maendeleo kwaio kama wameamua kususa ndio vyema zaidi sisi makada tukajivinjari Bungeni Dodoma peke yetu.
 
Mkuu Mhdiwani , mimi nilipata kura mbili tulikuwa wagombea 176, hivyo nikijitathmini nilivyo jiandaa kwa uchaguzi huo, investment niliyowekeza, na kura nilizopata, kiukweli kura mbili ni nyingi sana, haswa kwa kuzingatia kuna wengine wengi tuu, hawakupata kura kabisa!.
P
Huna lolote mpuuzi wew eti unajipendekeza tu ili wakuone kwenye cake ya taifa sbb ulichoandika ndicho wanachokiwaza wakubwa kwa ss hvyo umejitahidi kuwafurahisha
 
mwanzo nilidhani malalamiko ya wapinzani kuibiwa kura yana ukweli ndani yake but juzi nilipokua nafuatilia sakata la ndugu ambae ni miongoni mwa walokamatwa ajili ya vurugu za uchaguzi ndo nikaujua ukweli wa mambo...

police walitumia mbinu ya kutaka kitambulisho cha mpiga kura ili kubaini kama walokamatwa wamepiga kura au wanatumika vibaya kisiasa bt cha ajabu
zaidi ya 80% ya waliokamatwa hawana kitambulisho cha mpiga kura akiwemo ndugu yangu, kwa mantiki hii upinzani unapaswa kujitafakari na kuchukua hatua madhubuti kama wanataka kuwa washindani wa kweli wa chama tawala na sio kufanya siasa za majitaka ajili ya maslahi yao.
 
mwanzo nilidhani malalamiko ya wapinzani kuibiwa kura yana ukweli ndani yake bt juzi nilipokua nafuatilia sakata la ndugu ambae ni miongoni mwa walokamatwa ajili ya vurugu za uchaguzi ndo nikaujua ukweli wa mambo...

police walitumia mbinu ya kutaka kitambulisho cha mpiga kura ili kubaini kama walokamatwa wamepiga kura au wanatumika vibaya kisiasa bt cha ajabu
zaidi ya 80% ya waliokamatwa hawana kitambulisho cha mpiga kura akiwemo ndugu yangu, kwa mantiki hii upinzani unapaswa kujitafakari na kuchukua hatua madhubuti kama wanataka kuwa washindani wa kweli wa chama tawala na sio kufanya siasa za majitaka ajili ya maslahi yao.
Mkuu yuzazifu , asante kwa hoja hii, upinzani Tanzania ni michosho sana, ukiwaeleza ukweli wanakuwa wakali, tunawashauri upinzani wa kweli ni upinzani Bungeni na kule ni kushindana kwa hoja, lakini hawasikii.

Sasa wananchi wamewakataa, wanakuja na visingizio kibao.

P
 
pascal,
Public parties na Public interest maana yake ni nini?
Ni nani anasimamia au na kujua ni nini hiyo public interest?
Je public interest inaruhusu kuiba Kura?
Je Public party ni lazima ifuate public interest?
Ni nini maana ya public party ?
Ni nini maana halisi ya hiyo insanity, naona ina walakini kwa tafsiri yako...

Mwisho :
Unasemaje kuhusu madai ya wapinzani kwamba kura ziliibwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za uchaguzi na je ni sawa kwa wapinzani wakubali kuhalalisha wizi huo kwa kukubali matokeo ya wizi wa kura?

ushauri.. tafadhari, punguza kuandika andika humu vitu ambavyo hauna uhakika na maana yake kiufasaha... watu bado wana makovu na maumivu ya uchaguzi... ya nini kuwawekea chumvi kwenye vidonda vyao? waache wapone kwanza ndio uje na mabandiko yako...


Ni hayo tu kwa sasa...
 
kwa sasa hawana option nyingine itakayowafaa zaidi ya kujitafakari, na ikiwa wataendelea na mwenendo huu wa visingizio na uzushi ndo watakua wanajizika kisiasa maana watanzania washazijua hila zao
 
Wewe P kwasasa hutumikii kazi yako bali maslahi mbele yako. Insane, insanity, siyo hali unayoielezea bali umeshawatukana Viongozi wa vyama vya siasa mbadala nchini. Look at Cambridge dictionary: Insane,insanity is the condition of being seriously mentally ill. Ni kweli Lipumba, Zitto au Mbowe wana hali hiyo? Ongea kwa lugha nzuri tu uwafikishie ujumbe kuliko kuwatusi
 
Not all special interest groups a deleterious travesty to national and social security, peace and sustainable development; but their case is obviously an untenable, indefensible situation.
You are using the word "obviously" rather lightly.

I asked you to provide justification and rationale for saying so, you haven't.
 
Mkuu Mhdiwani , mimi nilipata kura mbili tulikuwa wagombea 176, hivyo nikijitathmini nilivyo jiandaa kwa uchaguzi huo, investment niliyowekeza, na kura nilizopata, kiukweli kura mbili ni nyingi sana, haswa kwa kuzingatia kuna wengine wengi tuu, hawakupata kura kabisa!.
P
Kwahiyo hukushindana ili ushinde, bali ulishindana ili usiwe wa mwisho!
 
Pumba producer katika ubora wako.

Ama kweli maisha yamekua magumu sana buku saba ya muhimu kiasi inabidi ujitoe akili.
 
  1. pascal,
    1. Public parties na Public interest maana yake ni nini?
    2. Ni nani anasimamia au na kujua ni nini hiyo public interest?
    3. Je public interest inaruhusu kuiba Kura?
    4. Je Public party ni lazima ifuate public interest?
    5. Ni nini maana ya public party ?
    6. Ni nini maana halisi ya hiyo insanity, naona ina walakini kwa tafsiri yako...
    7. jee ni sawa kwa wapinzani wakubali kuhalalisha wizi huo kwa kukubali matokeo ya wizi wa kura?
    8. ushauri.. tafadhari, punguza kuandika andika humu vitu ambavyo hauna uhakika na maana yake kiufasaha... watu bado wana makovu na maumivu ya uchaguzi... ya nini kuwawekea chumvi kwenye vidonda vyao? waache wapone kwanza ndio uje na mabandiko yako...


    Ni hayo tu kwa sasa...
 
Kwahiyo hukushindana ili ushinde, bali ulishindana ili usiwe wa mwisho!
Mkuu tindo , kwenye hili la mimi kugombea, nililieleza vizuri kabisa hapa

Baada ya matokeo nirejea JF nikajieleza
P
 
Swali la msingi hapa ni hili.

Unakubali kwamba CCM imeharibu sana uchaguzi na kuiba kura sana na hivyo matokeo ya uchaguzi huu ni batili?

Tafadhali jibu kama Mtanzania anayependa haki, na si kada anayetetea chama chake tu.
Mkuu Kiranga , uchaguzi hauendeshwi na CCM, unaendeshwa na NEC ambayo ni Tume huru ya uchaguzi japo sio Shirikishi!.

Kitu ambacho nakubali ni CCM imapiga kampeni kubwa safi na chafu, iliyofanya CCM ikubalike sana na upinzani ukataliwe. Mfano baadhi ya sisi makada wazalendo wa CCM, hatukuunga mkono zile kauli za vitisho kuwa mkichagua upinzani, maendeleo mtaishia kuyasikia, ni kauli za kibaguzi, ila Watanzania wamezikubali, wakaichagua CCM na kuwapiga chini wapinzani.

Sina uthibitisho wowote wa CCM kuiba kura zozote, hivyo despite dosari ndogo ndogo za hapa na pale, uchaguzi ulikuwa huru na haki na walioshinda wameshinda kihalali na kwa haki, walioshindwa wameshindwa kihalali na kwa haki kwa kukataliwa, the winner takes it all the loser standing small, it's simple and its plain, why should you complain?.

Na baada ya matokeo hayo ya wapinzani kukataliwa, tsunami ya CCM imekuwa too big kiasi italiathiri Bunge letu, ndio maana nimeshauri wapinzani wahurumiwe tuu ili Bunge letu lipate kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
P
 
Back
Top Bottom