Justdr
Member
- Jun 1, 2021
- 51
- 89
Habari za muda huu?
Najua mko wazima kabisa! Wale mnaoumwa Mungu awajalie mrudi kwenye hali zenu za kawaida.
Kumekuwa na hii imani kuhusu Virusi Vya UKIMWI watu wanatumia isivyo vipimo vya VVU(HIV SD BIOLINE au OraQuick HIV test) kama namna moja ya kijikinga ya haya maradhi. Watu wamekuwa wakipima mtu wakikuta yuko negative basi wanaona ni salama kufanya ngono bila kinga kwa maana kipomo kinasoma negative.
Ukweli ni kwamba kipimo kusoma negative haimaanishi kwamba hauwezi kuambukizwa VVU/HIV.
Ukiwa na uelewa wa vitu hivi viwili hautarudia kufanya tena hii mistake, Kitaalam kuna kitu kinaitwa WINDOW PERIOD na INCUBATION PERIOD. Tutaongelea zaidi window period maana ndo inahusika zaidi hapa.
WINDOW PERIOD ni Kipindi toka mtu ambukizwe hadi kutengenezwa kwa kingamwili dhidi ya VVU kwa kawaida huwa chini ya mwezi 1 lakini inaweza kuwa hadi miezi 3.
Hizi kingamwili(antibodies) ndo uwa zinapimwa na hivi vipimo Tajwa hapo juu mtu akiwa nazo ndo kipimo kinasoma positive yani ameathirika (Ndo maana ukienda vituo vya kutolea huduma za afya kupima afya yako unaambiwa upo okay but rudi baada ya miezi mitatu)
INCUBATION PERIOD hiki ni kipindi toka mtu apate maambukizi ya VVU hadi hatakapoanza kuonesha dalili ambayo kwa kawaida ni kuanzia mwezi mmoja mpaka zaidi ya miaka kumi (binadamu tunatofautiana)
Kwahiyo ikitokea umefanya mapenzi/ngono zembe na mtu ambaye umempima yuko negative ila yupo Window period unakuwa uko hatarini zaidi kupata HIV /VVU kwasababu huu ndo muda virusi vinakuwa vinajizalisha zaidi kwenye mwili na kingamwili bado inakuwa haijatengenezwa kupambana na hivi virusi. Let's be care!
Points to Note.
Kama una swali karibu.

- Kutumia vipimo vya HIV siyo namna sahihi ya kujikinga na haya maradhi.
- Kuna uwezekano mkubwa wa kupata HIV hata kama mwenzi wako umempima na ukakuta yuko Negative
- Matumizi ya kondomu yatabaki kuwa kinara wa kujikinga na HIV pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.
Kama una swali karibu.