Je, wajua tatizo kubwa sana kwenye nchi yetu ni lipi?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,514
17,424
Wakuu,

Nakubali tatizo kubwa ni katiba iliyopo na najua muda si mrefu tutaipata!

Tatizo kubwa zaidi hapa kwetu ni kwamba;-tuliamua kama Taifa
, kuwepo mishahara MIKUBWA sana, posho kubwa sana na mafao makubwa Sana yawepo kwenye siasa kuliko kada nyingine zenye mashiko na maendeleo kwa wote!!

YAANI kada nyingine zinadharaulika SIO kitu na wataalamu kuzikimbia Kwasababu hazina utajiri wa haraka kama wa kwenye siasa!

Naamini yupo atashika hatamu ambaye alishakinai Fedha na ukwasi na kuona SIO kitu atashusha mishahara na kuondoa posho za anasa za siasa na Hapo tutapata maendeleo ya kweli kuliko blah blah zilizopo Sasa!

Tutaepuka matatizo mengi Sana kama mauaji,unafiki,sifa za kijinga kama hizo zilizopo,hata rushwa zitapungua, ulozi na uchawi utapungua kwenye siasa na tutapata wanasiasa wazalendo wa kweli kuliko wachumia tumbo wengi waliopo!

Ninaamini kama SIO mimi ni wewe unaeweza kupindua meza kibabe kwenye HILI ukishika hatamu siku Moja!

Tuendelee kuimba kwa PAMOJA WIMBO huu;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"!!
 
walio madarakani hawana akili wana amini wameajiliwa kwa ajili familia zao na vizazi vyao na sio kuitumikia jamii.
WANANCHI NDIO WAJINGA wacha VIONGOZI wawanyooshe Viongozi wanalipwa Mamilioni Magari ya Anasa Matibabu First Class Wao na Familia zao nyie mmebweteka na Umasikini wenu kuleni Ujinga wenu
 
Tatizo kubwa kwenye familia ukoo kitongoji kijiji kata tarafa wilaya mikoa nchi mabara hadi huko duniani ni tamaa na ubinafsi. Vurugu zote unaziona ni tumbo ndo linawatesa watu. Njaaa haina komando. Emu fikiria tusingekuwa na matumbo nani angetamani kula nani angetamani kula cha mwenzie.
 
Katiba mpya haiwezi kukubalika kwa sababu hizi

1) Inagusa muungano
2) Inagusa uraia pacha

CCM hawatakubali muungano uguswe kwa sababu ukiguswa utadhoofika na baadaye kuvunjika. Uraia pacha ukiletwa waliokimbia nchi baada ya mapinduzi ya ZNZ na Azimio la Arusha watarudi kudai mali zao.
 
Wakuu

Nakubali tatizo kubwa ni katiba iliyopo na najua muda si mrefu tutaipata!

Tatizo kubwa zaidi hapa kwetu ni kwamba ;-tuliamua kama Taifa,kuwepo mishahara MIKUBWA Sana,posho kubwa Sana na mafao makubwa Sana yawepo kwenye siasa kuliko kada nyingine zenye mashiko na maendeleo kwa wote!!

YAANI kada nyingine zinadharaulika SIO kitu na wataalamu kuzikimbia Kwasababu hazina utajiri wa haraka kama wa kwenye siasa!

Naamini yupo atashika hatamu ambaye alishakinai Fedha na ukwasi na kuona SIO kitu atashusha mishahara na kuondoa posho za anasa za siasa na Hapo tutapata maendeleo ya kweli kuliko blah blah zilizopo Sasa!

Tutaepuka matatizo mengi Sana kama mauaji,unafiki,sifa za kijinga kama hizo zilizopo,hata rushwa zitapungua,ulozi na uchawi utapungua kwenye siasa na tutapata wanasiasa wazalendo wa kweli kuliko wachumia tumbo wengi waliopo!!

Ninaamini kama SIO mimi ni wewe unaeweza kupindua meza kibabe kwenye HILI ukishika hatamu siku Moja!

Tuendelee kuimba kwa PAMOJA WIMBO huu;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"

UBINAFSI
 
Back
Top Bottom