Je wajua - Spice Islander imeua watu kuliko Titanic?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wajua - Spice Islander imeua watu kuliko Titanic?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, May 21, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ni kitu ambacho kinasikitisha kila ninapokifikiria, kwamba disaster ya Spice Islander ya Zanzibar iliua watu wanaokadiriwa kuwa 2800, wakati ile ya Titanic iliua watu wapatao 1500. Na ni kweli watoto na wanawake wengi sana walikufa Spice Islander ukilinganisha na Titanic. Machozi yananilengalenga nikifikiria kina mama katika Spice Islander wakiwa hawana la kufanya bali kukumbatia watoto wao waliokuwa wakilia kwa woga na kujiandaa kufa nao, wakijua hakuna ambalo wangeweza kufanya kujiokoa wao na watoto wao wadogo. Nafikiria ningekuwaje ikiwa mwanangu mdogo na mama yake wangekuwa katika hali ile, ndoto gani ningeota kila usiku nikilala; ninajaribu kuwaokoa?

  Kwa nini basi dunia ilikaa kimya juu ya Spice Islander ukilinganisha na Titanic? Ina maana dunia inajali zaidi gharama ya meli zilizohusika kuliko roho za binadamu zilizopotea?

  Na viongozi wetu wamesahau kama vile lilikuwa tu ni jambo la kawaida. Imekuwaje binadamu tumekuwa wanyama kiasi hiki?
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  inaweza ukawa sawa mkuu lakini ukumbuke dunia yetu ni kubwa na binadamu wana tabia ya kujiangalia zaidi kabla ya kutegemea kuonwa na wakazi wengine wa dunia. Ndio maana kuna maeneo tofauti ya utawala.
  Wazungu kama wao wilitangaza sana Titanic na kushughulika nayo kwa sababu ilikuwa imewabeba wao, na baada ya hapo ndio maana wanajitahidi kuweka sheria za vyombo vya majini na kuzifuata kikamilifu.
  Pia ukumbuke wao wanaamini kuwa sisi hatuthamini maisha na sio ajabu siku ule msiba wa Spice Islander wanasiasa walikuwa kwenye siasa zao wakati wamekufa watu zaidi ya 2800 lakini uliona siku basi lilivyogonga ukuta Uswizi likiwa na watoto kutoka Belgium, EU nzima iliomboleza.
  Hivyo usiwalaumu wazungu bali jilaumu mwenyewe na viongozi wetu kwa kuwa kama tulivyo (kutojali maisha).
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Yeah, nilikuwa namsomesha mtu kuhusu hili. Halafu huko Malaysia/ Singapore/ The Phillipines watu wanakufa kila mwezi karibu hata hatusikii sana. Ukiwa na mshiko hata historia unaweza kuiandika unavyotaka.

  Halafu hata hapa nchini ajali za barabarani zinaua watu wengi zaidi ya za majini, lakini za majini hutokea mara chache na zinaua wengi kwa mpigo.

  Lakini utaona HIV/AIDS na ajali za majini zinapewa kipaumbele zaidi.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  2800? WENGI SANA ,
  EH MUNGU NA SERIKALI ILITANGAZA WANGAPI?
  Hivi vyote vinachaNGIWA NA KUWA NA TAKWIMU HAFIFU NA KUTOKUWA WAWAZI.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Hii Habari ilipaswa kuwepo kwenye Jukwaa la kimataifa kwa sababu Zanzibar ni nchi. Mungu awaweke marehemu wote sehemu wanazostahili motoni/peponi,
   
 6. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Peoplessssssssssssssssssssss
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,350
  Likes Received: 2,688
  Trophy Points: 280
  mimi mkuu nitakuuliza tu swali moja...hivi ajali ya Titanic ilikugusa vipi? hata kama ilitokea ukiwa hujazalia ila najua habari zake utakua unazifahamu
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Hata wewe ni kama walimwengu wengine tu. Leo tarehe 21/5/2012 ni miaka 16 kamili tokea MV Bukoba ipinduke na kuzama, ila wewe umekumbuka Titanic na kusahau MV Bukoba iliyoua watanzania wengi.
   
 9. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ulitaka nilinganishe MV Bukoba na Spice Islander? Japo kifo hata cha mtu mmoja ni majonzi, nadhani unapaswa kuwa na akili ya kuona kwa nini nililinganisha Spice Islander na Titanic. Na hapa naongelea tukio la karibuni ambalo limetokea tukiwa na JF. Kama wewe unaona ni vema kulinganisha MV Bukoba na Titanic go ahead, anzisha thread. Fikiria kabla ya kukurupuka na kutuhumu.
   
 10. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Watu8, disaster ya Titanic ilinifanya nione kama watu walishtushwa na kilichotokea na hata kuchukua hatua stahili kuhakikisha haijirudii tena, na nikidhani yote haya yalitokana na idadi kubwa ya watu iliyopotea. Nilitarajia dunia pia itashtushwa na idadi ya watu iliyopotea Spice Islander. Naona labda sikuwa sahihi, issue ilikuwa ni mali iliyopotea. Labda ndio maana uchunguzi wa kina na gharama unafanywa ndege ikianguka - japo idadi ya abiria si kubwa kama wanaokuwa katika meli, bali kwa kuwa gharama ya ndege ni kubwa sana.
   
 11. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,871
  Likes Received: 4,252
  Trophy Points: 280
  Kitu gani kimekufanya uikumbuke MV SPICE ISLANDERS wakati leo tunaadhimisha miaka 16 ya kuzama kwa meli ya mv BUKOBA, au we ni mzanzibari?
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  na wao walipata habari ya mv bukoba yetu
   
 13. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwani Wapemba wangapi walifia kwenye MV Bukoba hadi aikumbuke?.
  Wapemba ni wabaguzi sana jombaa!!
   
 14. nasnee

  nasnee Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana
   
 15. javascript

  javascript Senior Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Why does Titanic hold the record? And i keep asking myself, hawa weupe ni wa bei ghali sana? wanadiriki hata kubadilishana mweupe mmoja kwa mamia, hivi exchange rate ya mtu mweusi kwa mweupe ikoje?
   
 16. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  mtu mmoja mweupe ni sawa na watu elfu kumi weusi!
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  zzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Unakasirika nini? Nimekuuliza hivyo kwa vile pamoja na kuwa umeanzisha thread yako ambayo kimsingi ina mantiki umelinganisha Spice Islander na Titanic na kusahau MV Bukoba tena katika siku ya kumbukumbu ya ajali hiyo. Ndio maana nasema hata wewe ni kama hao unaowalaumu kwa kupuuza Spice Islander wakati nawe unakumbuka Titanic tuu.
  Aliye kurupuka bila kufikiri ni wazi ni wewe.
   
 19. lusubilo lucas

  lusubilo lucas Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  we chakaza mbna unakurupuka umesoma ile thread au ndio unajipima uwezo wako humu kwa ubish wa kijinga
   
 20. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  inategemea nani anayefanya hiyo exchange.
   
Loading...