Je, wajua Simu ya Mkononi ya kwanza Duniani ilikuwa na uzito wa kilogram 2 na ilijaa chaji kwa saa 12?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Zaidi ya miaka 42 iliyopita simu ya kwanza ilipigwa kutumia simu ya mkononi, simu hiyo ya kwanza ya mkononi ilitengenezwa na kampuni ya Motorola.

Ilikuwa mwezi wa 4 tarehe 3 mwaka 1973 walijaribu kupiga simu kwa kutumia simu hiyo ya kwanza ya mkononi iliyokuwa inafahamika kwa jina la Motorola DynaTAC.

Mfanyakazi wa Motorola aitwaye Marty Cooper alitumia simu ya mkononi kupiga simu kwenda ofisi yao (kwenye simu ya mezani), ilipoita na kupokelewa alisema, “Napiga simu kutaka kufahamu kama nasikika vizuri upande huo.”

Bwana Martin Cooper akishikilia Motorola DynaTAC kushoto kwake na simu yake nyingine aliyokuwa anatumia, picha hii ni ya mwaka 2009.

Simu hii ilikuja kuingia sokoni mwaka 1983 baada ya muda kidogo ikitumia jina la Motorola DynaTAC 8000x na hii ndiyo simu ya kwanza ya mkononi kuingia sokoni na watu kuweza kununua. Na ilikuwa inauzika kwa bei ya juu sana, dola 3995 za kimarekani za wakati huo, ambayo ni si chini ya Tsh 8,000,000 za kitanzania.
Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine kadhaa ya maboresho zaidi
Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine kadhaa ya maboresho zaidiFahamu sifa za Motorola DynaTAC 8000x
  • Ilikuwa inatumia teknolojia ya analogia hivyo haikuwa na uwezo wa kuwekwa laini, teknolojia ilikuwa haijafikia huku.
  • Ilikuwa na uzito wa kilogramu 2 ukilinganisha siku hizi simu nyingi zinakuwaga na uzito wa gramu 100 hadi 150 (Kumbuka kilogramu 1 = gramu 1000)
  • Ilikuwa na urefu wa sentimita 33 kwa 8.89 na kawembamba ka sentimita 4.4.
  • Kioo (display) chake kilikuwa kiduchu, cha kuandika mstari mmoja tuu.
  • Iliitaji kuchajiwa kwa muda wa masaa 10 kutoka kutokuwa na chaji kabisa hadi kujaa kabisa
  • Na ata baada ya kuchaji kwa muda wa masaa 10 muda wa maongezi wa takribani dakika 30 tuu ungemaliza chaji hiyo.

    Mlinganisho rahisi wa ukubwa wa simu hii na zingine za kisasa

Sasa kama ni simu ya kwanza aliweza vipi kuwasiliana na upande mwingine? Hiyo aliyowasiliana nayo upande wa pili ilitokea wapi??
 
Ndugu simu zilikuwepo zile za mezani ninaunganishwa na waya soma kichwa habari vizuri na habari yenyewe utaelewa na pia fuatilia historia ya simu kama unatka na una mda.
 
ndugu simu zilikuwepo zile za mezani ninaunganishwa na waya soma kichwa habari vizuri na habari yenyewe utaelewa na pia fuatilia historia ya simu kama unatka na una mda.
Simu ya mezani (landline)
Nimesoma na kuelewa kumbuka katikati ya mada alisema hakukuwa na teknolojia ya line kwa kipindi hicho, je simu ya mkononi iliwezaje kuingiliana na simu ya mezani?
 
Simu za mkononi za mwanzo kabla ya kuja gsm/2g/gprs zilikuwa ni kama Radio call, unaongea then unasubiri na mwenzako aongee, hamuwezi kuongea kwa pamoja, hivyo hazikuwa kama simu za sasa,

Kama wewe ni mpenzi wa movie utaona movie za kizamani kama Arnold na Van Dame kila Gari ina simu fulani ina waya unao connect na gari, zile ndio zilikuwa simu za mwanzo, nazo pia ni kama radio call.

Hivyo ulikuwa ni mfumo kabisa umewekwa, ambao unatumika na simu zote iwe ya mezani, mkononi ama Hata kwenye gari ama ofisi.

Kama kumbukumbu zipo sahihi mkuu walikuwa wanatumia frequency, mfano kuna frequency ya polisi ukiseti mapolisi wote wanaongea kwenye hio frequency.
 
Kivipi? Hapa nilipo hata uzunguke masaa 6 hukuti mtu ana simu ya motorola!
Motorolla kama Mtengeneza Network Equipments pamoja na Siemens mtengeneza Network na Nokia hawa wote Ni kampuni Moja sasa hivi Inaitwa Nokia Networks na ndio wana Lead Race ya 5G kwenye Mitandao ya simu. Hivyo bado wapo relevant kwa Dunia ya sasa.

Motorola kama Mtengeneza Simu amenunuliwa na Lenovo na soko lao kubwa wanalotarget ni North America kwa nchi kama USA. Hawauzi simu nyingi ila hilo soko pia lina utajiri hata kama unauza chache.
 
Simu za mkononi za mwanzo kabla ya kuja gsm/2g/gprs zilikuwa ni kama Radio call, unaongea then unasubiri na mwenzako aongee, hamuwezi kuongea kwa pamoja, hivyo hazikuwa kama simu za sasa,

Kama wewe ni mpenzi wa movie utaona movie za kizamani kama Arnold na Van Dame kila Gari ina simu fulani ina waya unao connect na gari, zile ndio zilikuwa simu za mwanzo, nazo pia ni kama radio call.

Hivyo ulikuwa ni mfumo kabisa umewekwa, ambao unatumika na simu zote iwe ya mezani, mkononi ama Hata kwenye gari ama ofisi.

Kama kumbukumbu zipo sahihi mkuu walikuwa wanatumia frequency, mfano kuna frequency ya polisi ukiseti mapolisi wote wanaongea kwenye hio frequency.
Correct this is what I need to hear, sio bla bla Naelewa chief, sometimes tunapima uelewa. Eti mtu ananisimulia kama hadithi wakati naelewa evolution ya simu tangu sauti pekee, sauti na ujumbe, gprs hadi tulipofikia leo.
 
Simu za mkononi za mwanzo kabla ya kuja gsm/2g/gprs zilikuwa ni kama Radio call, unaongea then unasubiri na mwenzako aongee, hamuwezi kuongea kwa pamoja, hivyo hazikuwa kama simu za sasa,

Kama wewe ni mpenzi wa movie utaona movie za kizamani kama Arnold na Van Dame kila Gari ina simu fulani ina waya unao connect na gari, zile ndio zilikuwa simu za mwanzo, nazo pia ni kama radio call.

Hivyo ulikuwa ni mfumo kabisa umewekwa, ambao unatumika na simu zote iwe ya mezani, mkononi ama Hata kwenye gari ama ofisi.

Kama kumbukumbu zipo sahihi mkuu walikuwa wanatumia frequency, mfano kuna frequency ya polisi ukiseti mapolisi wote wanaongea kwenye hio frequency.
Na kuhusu hivi frequency ni hadi leo polisi wanazitumia kwenye radio call zao kama sikosei ni High freq from 3Mhz to 9Mhz. Ambayo kirange imo katika 3Mhz - 30Mhz.
 
Zinatumika dunia nzima mkuu, sema siku hizi vyombo vya usalama ndio wanatumia zaidi.

Sifahamu polisi wanatumia ipi ila kuna list wikipedia wameelezea frequency na vyombo husika wanavyotumia

International distress frequency - Wikipedia
 
Zaidi ya miaka 42 iliyopita simu ya kwanza ilipigwa kutumia simu ya mkononi, simu hiyo ya kwanza ya mkononi ilitengenezwa na kampuni ya Motorola.

Ilikuwa mwezi wa 4 tarehe 3 mwaka 1973 walijaribu kupiga simu kwa kutumia simu hiyo ya kwanza ya mkononi iliyokuwa inafahamika kwa jina la Motorola DynaTAC.

Mfanyakazi wa Motorola aitwaye Marty Cooper alitumia simu ya mkononi kupiga simu kwenda ofisi yao (kwenye simu ya mezani), ilipoita na kupokelewa alisema, “Napiga simu kutaka kufahamu kama nasikika vizuri upande huo.”

Bwana Martin Cooper akishikilia Motorola DynaTAC kushoto kwake na simu yake nyingine aliyokuwa anatumia, picha hii ni ya mwaka 2009.
Bwana Martin Cooper akishikilia Motorola DynaTAC kushoto kwake na simu yake nyingine aliyokuwa anatumia, picha hii ni ya mwaka 2009.
Simu hii ilikuja kuingia sokoni mwaka 1983 baada ya muda kidogo ikitumia jina la Motorola DynaTAC 8000x na hii ndiyo simu ya kwanza ya mkononi kuingia sokoni na watu kuweza kununua. Na ilikuwa inauzika kwa bei ya juu sana, dola 3995 za kimarekani za wakati huo, ambayo ni si chini ya Tsh 8,000,000 za kitanzania.
Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine kadhaa ya maboresho zaidi
Mafanikio ya simu hii ilifanya yatoke matoleo mengine kadhaa ya maboresho zaidiFahamu sifa za Motorola DynaTAC 8000x
  • Ilikuwa inatumia teknolojia ya analogia hivyo haikuwa na uwezo wa kuwekwa laini, teknolojia ilikuwa haijafikia huku.
  • Ilikuwa na uzito wa kilogramu 2 ukilinganisha siku hizi simu nyingi zinakuwaga na uzito wa gramu 100 hadi 150 (Kumbuka kilogramu 1 = gramu 1000)
  • Ilikuwa na urefu wa sentimita 33 kwa 8.89 na kawembamba ka sentimita 4.4.
  • Kioo (display) chake kilikuwa kiduchu, cha kuandika mstari mmoja tuu.
  • Iliitaji kuchajiwa kwa muda wa masaa 10 kutoka kutokuwa na chaji kabisa hadi kujaa kabisa
  • Na ata baada ya kuchaji kwa muda wa masaa 10 muda wa maongezi wa takribani dakika 30 tuu ungemaliza chaji hiyo.

    Mlinganisho rahisi wa ukubwa wa simu hii na zingine za kisasa
    Mlinganisho rahisi wa ukubwa wa simu hii na zingine za kisasa
motorola mkombozi
 
Vyombo vya usalama kwa ajili ya mawasiliano ni kuanzia 3Mhz to 30Mhz ambayo ipo chini ya commercial fm stations(87 -108Mhz). Na hiyo ni dunia nzima. Sema kuna kitu kwao wanaita radio displine huko ndio hupangiana masafa ya kutumia, kama ukiwa na radio yako na ukitaka kuwaskiliza wakiongea (Intercept) unapitia kwenye hizo freq taratibu hadi unawanyaka. Ila ni uhalifu.
Mkuu tupe shule, unawezaje kuingilia mawasiliano yao na kuwaskiliza?
 
Back
Top Bottom