Je, wajua ni muhimu kuwapa watoto elimu ya afya ya uzazi?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Wataalamu wa #Malezi wanatuambia ni muhimu kuwapa watoto elimu ya afya ya uzazi ili kuwaepusha na madhara kama kujihusisha na kujamiiana wangali wadogo, mimba za utotoni, ndoa za utotoni na kupata magonjwa ya zinaa.

Lengo kuu likiwa ni kuwawezesha watoto kujilinda na kujitunza ili waendelee kukua wakiwa na ustawi na maadili bora yatakayowafikisha kwenye ndoto na malengo yao ya baadae.
 
Tusindikize ujumbe na burudani kidogo
 
Kwenye jamii zetu swala la uzazi wa mpango na ngono limekuwa ni swala linalochukuliwa kuwa linawahusu watu walio kwenye ndoa tu au watu wazima (tena hawa wanawake). Hii inafanya iwe ngumu kwa jamii zetu kumpatia elimu ya uzazi na mahusiano kijana mdogo ambaye kafikia umri wa kupevuka (hasa kijana wa kike) kutokana na imani tulizo jiwekea kuwa kufanya hvyo ni kumfundisha huyu binti/kijana wa kiume tabia mbaya(umalaya) kitu ambacho sio kweli matokeo yake ni kijana(wa kike na kiume) kukoswa uelewa tosha juu ya elimu ya uzazi na mahusiano, kukoswa uelewa juu ya kukabiliana na changamoto za mabadiriko ya kumaumbile yanayomtokea, ukoswa mahali sahihi pakueleza na kusikilizwa changamoto zake anazokutana nazo wakati wa umri wa kupevuka. hii upelekea vijana kushauriana wao kwa wao juu ya mambo wasio kuwa na uelewa nayo(kupotoshana) na kujaribu kujihusisha na mahusiano ya ngono pasipo kuwa na elimu sahihi juu ya madhara ya vitendo hvyo.

USHAURI: 👉Ni vizur jamii zetu kufahamu kuwa zama zimebadirika dunia ya sasa sio sawa na dunia ya miaka 20 au zaid iliyopita, ulimwengu sasa unamuwezesha kijana/ mtoto kujifunza mambo mengi (mazuri na mabaya) kwa urahisi zaidi pasipo mzazi kutambua. Kwaiyo ni vyema wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kumpa kipaumbele huyu mtoto aliekwenye/anaekaribia/ alievuka umri wa kupevuka juu ya maswala ya uzazi na mahusiano.

👉Somo la uzazi wa mpango na mahusiano liingizwe na kufundishwa kwa undani zaidi kwenye mitaala ya elimu kuanza elimu ya msingi hadi vyuoni

👉wazazi kutenga mda wao kusikilizwa na kutatu changamoto za watoto wetu hasa wanapokuwa kwenye umri wa kupevuka, kuvua vazi la aibu na kujivika ujasir wa kuwa walimu na wataalam wa kwanza kutoa elimu ya afya ya uzazi na mahusiano kwa watoto wao.

👉Wahudumu wa afya(sekta ya afya) kwa kushirikiana pamoja na sekta ya elimu kuandaa program maalum ya kutoa elimu juu ya afya ya uzazi kuanzia shule za msingi, sekondari hadi ngazi za juu za elimu.
 
Halafu akili ya binaadam iko kama unapomwambia usifanye hiki ndiyo kama umemuhamasisha afanye hilo jambo, ukiwaambia watoto msipande kwenye mlango, utawakuta wanabembea kwenye huo mlango
 
Back
Top Bottom