je wajua mtawanyiko wa fedha za matangazo katika vyombo vya habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je wajua mtawanyiko wa fedha za matangazo katika vyombo vya habari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 15, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  VYOMBO vya habari nchini yakiwemo magazeti, redio na runinga vimepata Sh bilioni 84 mwaka jana zilizotokana na matangazo mbalimbali kutoka kwa wadau wake hususani kampuni binafsi na taasisi za serikali.
  Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Utafiti ya Synovate, umebaini kuwa mapato hayo yameongezeka ikilinganishwa na mwaka 2005 ambapo vilipata Sh bilioni 37; 2006 Sh bilioni 40; 2007 Sh bilioni 54 na 2008 Sh bilioni 79.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Jane Meela alisema utafiti huo wa vyombo vya habari umefanywa kwa miaka mitano.
  Alisema Synovate ina vituo vitatu ambavyo vipo Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar na vinapata stesheni zote za runinga, redio pamoja na magazeti yote ya kila siku, kila wiki na majarida ya mwezi na vinafanya kazi kwa saa 24 ili kuhakikisha shughuli zote za vyombo vya habari vinafuatiliwa kwa umakini.
  “Ufuatiliaji wa utafiti huu unafanywa kwa umakini kwa kusoma magazeti, kusikiliza redio na kuangalia runinga ili kuweza kujua kiasi cha matangazo yaliyochapiswa na kurushwa hewani na tunaangalia gharama kwa kila chombo kupitia kadi ya malipo ya matangazo ya vyombo hivyo,” alisema Meela.
  Akizungumzia watoa matangazo, alisema kampuni za simu ndizo zinazoongoza ambapo zilichangia Sh bilioni 59, zikifuatiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na serikali waliochangia Sh bilioni 28 na vinywaji Sh bilioni 17.
  Aidha, alisema katika matangazo hayo ya mwaka 2009, runinga zilipata Sh bilioni 39 sawa na asilimia 46; redio Sh bilioni 34 (asilimia 40); magazeti Sh bilioni 10 (asilimia 12) na majarida Sh bilioni mbili (asilimia mbili).
  Utafiti huo unaonesha kwamba kwa mwaka jana, redio iliyoongoza kwa kuwa na wasikilizaji wengi ni Radio Free Africa asilimia 39 iliyopata matangazo ya Sh bilioni tisa, ikifuatiwa na TBC Taifa asilimia 35 kwa matangazo ya Sh bilioni nne, Clouds Fm na Radio One Sh bilioni sita, Magic Fm Sh bilioni tano na Kiss Fm Sh bilioni moja.
  Kwa upande wa runinga zinazoongoza kwa kutazamwa ni TBC1 iliyopata matangazo ya Sh bilioni nane, ITV iliyopata Sh bilioni 12, Star Tv na Channel Ten Sh bilioni nane, na EATV Sh bilioni 4.

  Halikadhalka katika upande wa magazetini ya kila siku, kwa mwaka jana, Guardian lilipata matangazo ya Sh bilioni mbili (asilimia 25) na Daily News ambalo lilipata Sh bilioni 1.2 sawa na asilimia 16.
  Meela alifafanua kwamba kampuni zilizotumia fedha nyingi kwa ajili ya matangazo hadi kufikia Sh bilioni 42 kwa mwaka jana na asilimia zao kwenye mabano ni MIC Tanzania ambao bidhaa yao ni Tigo (27), Vodacom Tanzania (19), Zain (18), SBC Tanzania (8), PSI (7), Zantel na TBL (5), ABMP, Nokia Corporation na Serikali (4).
   
 2. L

  Lukwangule Senior Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilituma thread hii kuona namna watu wanavyoweza kuchambua mambo na kuona maana yake. lakini wengi wanaojua kuchambua wamekaa kimya.Takwimu zinagonga nini? Maana yake haijulikani nini? Wanaojua mambo ya fedha wanaweza kuzungumza maana yake nini fedha hizi.Tunajua sote mtu anayetangaza sana hapa nchini ni serikali kama vile vile inavyoajiri wengi zaidi. Maana yake mnajua kwa vyombo vya habari nba nguvu zake kwa watu binafsi? ha ha ha demokrasia wakati fulani unaishangaa kama inahimili ...kama ina usafi unaopstahili kama trend ya namna hiyo sio inawezesha kibri cha watu! watu wanaelewa kodi zao zinazounguka namna gani?Samahani nilitaka kuwazingua tu nijue kama mnachambua au mnakimbilia cheap material ambayo digestion yake ni rahisi. Huyu mtu anayejidai kusema hizi takwimu hakusema mambo mengi mnayajua lakini?
   
Loading...