Je, wajua mchezaji gofu maarufu duniani Tiger Woods huwa hajitambulishi kama mtu mweusi?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Tiger Woods anaamini yeye ni mtu wa asili nyingi na hata alijiundia jina mseto kueleza asili yake, na kusema asili yake ni Cablinasian. Cablinasian ni neno linalotokana na Caucasian(Mzungu), Black American (Mwafrika Mmarekani), American Indian (Mmarekani Asilia), na Asian (Asia). Babake, Earl, alikuwa wa asili ya Mwafrika Mmarekani, Mchina na Mmarekani Asili. Mamake Kultida, ni wa asili ya Thailand, Uchina na Uholanzi.

18813531_1559581400727186_969890324467272878_n.jpg

Chanzo: BBC
 
Mbona polisi juzi alipokamatwa fomu yake imeandikwa black....

Itakuwa walikosea. Au labda fomu haina option ya 'biracial' au 'multiracial' hivyo wakaona isiwe shida na wakajaza tu hiyo 'black'.

Lakini kamwe mtu aliyechanganya rangi hawezi kuwa rangi moja na asiwe ingine/zingine.
 
As long as you are Blackman, you are an African "Peter Tosh" na Mungu alivyotujalia watu weusi either uwe mume au Mke ukichanganya Damu tu na race nyingine iwe Mwarabu, Mzungu, Mchina.... Toto lazima liwe jeusi na utatambulika Dunia nzima wewe ni black hata kama wewe mwenyewe hajitambui kama alivyo Tiger Woods
 
Itakuwa walikosea. Au labda fomu haina option ya 'biracial' au 'multiracial' hivyo wakaona isiwe shida na wakajaza tu hiyo 'black'.

Lakini kamwe mtu aliyechanganya rangi hawezi kuwa rangi moja na asiwe ingine/zingine.

Yeye alijiita 'blacklausian' kitu kama hiko
sidhani kama ipo kwenye fomu yoyote
 
Your opinion..
mimi naona kama watu wanakuona ni blackk basi black tu
hata utumie nguvu vipi ku deny..

Hapana, hiyo siyo my opinion.

Kama yeye ni uzao wa watu wenye rangi tofauti basi hiyo ni scientific fact.

Ni kama ilivyo kwa Obama.

Mama yake ni mzungu [mweupe] na baba yake ni mwafrika [mweusi].

That is a scientific fact. Siyo opinion.

Opinion ni kumchukulia Obama kuwa mweusi na si shombe.

Kwa hiyo opinion hapo ni kwa wale wanaomwona kuwa yeye ni black na si mchanganyiko ilhali ukweli wa mambo yeye ni mchanganyiko.

Wanaotumia nguvu ku deny uhalisia wake ni hao wanaosema yeye ni black na kuzikana rangi zake zingine zinazomfanya yeye awe yeye.
 
Hapana, hiyo siyo my opinion.

Kama yeye ni uzao wa watu wenye rangi tofauti basi hiyo ni scientific fact.

Ni kama ilivyo kwa Obama.

Mama yake ni mzungu [mweupe] na baba yake ni mwafrika [mweusi].

That is a scientific fact. Siyo opinion.

Opinion ni kumchukulia Obama kuwa mweusi na si shombe.

Kwa hiyo opinion hapo ni kwa wale wanaomwona kuwa yeye ni black na si mchanganyiko ilhali ukweli wa mambo yeye ni mchanganyiko.

Inafahamika kwa usa ukisema black people ni pamoja na hao mixed
Brazil ndo tofauti.....kina Malcolm X na wengi wengi neo kama Alex Haley..
wote walikuwa mixed but walijiita blacks
 
Inafahamika kwa usa ukisema black people ni pamoja na hao mixed
Brazil ndo tofauti.....kina Malcolm X na wengi wengi neo kama Alex Haley..
wote walikuwa mixed but walijiita blacks

Hata wangejiita ni wa kijani...ukweli unabaki kuwa wamechanganya rangi. Na hiyo ni scientific fact.

Kama siyo scientific fact, ikatae kwa kutoa facts na si opinions.

Mama au baba akiwa mzungu na mzazi mwingine awe wa rangi tofauti, mtoto atakuwa kachanganya rangi.

That's just a fact. A scientific one at that.
 
Hata afanye nini wakati wake umeisha kama golfer. Na hata kifedha anaelekea kubaya sana. Ila mtu mweusi hasa mwanamume ukitaka kumjua kagua bunduki yake. Hata achanganye damu vipi itabakia na shepu yake ya kiafrika.
 
Aiseee... sijawahi kufahamu kwamba shepu ya bunduki za kiafrika ni tofauti na bunduki za kizungu.
 
Back
Top Bottom