Je, wajua matumizi ya "A" na "THE" katika lugha ya kiingereza?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
3,395
2,000
Maneno "a" pamoja na "the" ni kifungu cha mameno ambayo huwa yanatumika kama utambulisho wa nomino katika lugha ya kiingereza .utofauti wa haya maneno mawili ni:-
"A" hutumika kutambulisha nomino ambayo haina umbo maalum.kwa mfano:- tuchukue nomino ambayo haina umbo maalum kama "maji" basi sentensi itakuwa, "this is a water from indian ocean".hatuwezi kusema "this is the water from indian acean.
"THE" ni kinyume cha "A" ambapo hutumika kwa ajili ya utambulisho wa nomino ambayo ina umbo maalum hapa tutumie kitabu sentensi yetu itakuwa ni, "this is the book".hatuwezi kusema "this is a book
nafikiri nitakuwa kidogo nimetoa darasa kwa ambao walikuwa wakichanganyikiwa juu ya maneno haya mawili.
Mara nyingi, tunatumia (indefinite article) 'a' kama tukitaja mtu au kitu tunachokielezea kwa mara ya kwanza na (definite article) 'the' kama tayari kinafahamika kwa wengine tunaowasiliana au ongea nao. Mfano, kama nilikutana na mkazi fulani nisiyemjua Dar es Salaam jana na kama nitataka kuongea habari zake, nitasema 'I met a man/woman dressed in red ni Dar es Salaam yesterday.

Halafu baada ya kusema hivyo, nikirudia kumtaja sitasema tena 'a' maana kwa sasa 'audience' yangu inafahamu kwamba ninaongelea mtu niliyekutana naye Dar es Salaam jana, hivyo nitatumia 'the'. Mfano: The man/woman (na siyo 'a') I met yesterday was killed in a road accident. Angalia pia matumizi ya 'a' mbele ya 'road accident' na siyo 'the'. Lakini nikitaka kutumia 'the' nitasema, 'He/she was killed in the road accident as he was crossing Mtakuja Road in 'Wagagagigigogo City'.

Lakini kuna pia majina famous ya mbuga za wanyama, mito au mengineyo ambayo hatutumii 'a' hata kama tukiyataja kwa mara ya kwanza, bali 'the' - mfano, The Serengeti, The East African Rift Valley, The Nile, The Indian Ocean, The Pacific, The Moon, The Sun etc na majina mengine tunaacha kutumia (kuna moot 'the') - mfano, Lake Tanganyika, Lake Victoria, Mount Kilimanjaro, Oldonyo Lengai.
 
Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
5,905
2,000
Wanaongea Kama wameweka bamia mdomoni....mbaya zaidi umkute mmarekani mweusi anaongea ndo utajuta Bora hata ya mzungu.

Wengine huwa wanaongea "EBONICS" na Wengine huchanganya English na Ebonics. Hii pia huwa inawapa shida wazungu kuwaelewa baadhi ya Black Americans.
 
Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
5,905
2,000
Faraja vitalis,
Unatakiwa ujifunze zaidi, nenda Google na uangalie matumizi ya hizo articles; "a, (an)" na "the"--- yenye matumizi mapana sana ni hiyo definite article " the, mfano unaposema; I don't have the money to buy a new car, hapo maana yake ni; Sina pesa za kutosha kununua gari (yoyote moja), hapo utaona maneno; "the money" yanabeba maana ya; pesa za kutosha. Lakini indefinite article "a (an)" haina matumizi makubwa mbali na introduction (utambulisho), maelezo, uhitaji wa kitu kipya (kimoja). Unaweza kuangalia kwenye Dictionary.com ili upate picha nzuri.

Keep it up.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,779
2,000
Hili tatizo la kutokuelewa mzungu katamka Nini kwenye tv lipo hata kwa wasomi tunaowaamini.Ukitaka kujua hilo tafuta wasomi wetu Hawa tunaowajua afu kaa nae kwenye tv Kisha mfungulie aljazeera afu muulize hv mtangazaji kaongea Nini pale??....aisee jibu atakalokupa utakoma kuuliza tena yan.
Wakati niko O-Level tulipata walimu wa field kutoka Queen's University, Canada, Yaani walikuwa wanaongea hatuelewi kabisa.

Hata Majina tu kuyajua ilikuwa shida mpaka, wakaandika "Name Tags" Kila mmoja akabandika kifuani.

Yaani kama ulikuwa unajiona ushajua English inabidi urudie madaftari uweke juhudi upya
 
Paula Paul

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
3,417
2,000
Badala ya wewe kumfundisha katika makosa kama haya; " this is a water----" 🤣??!!.
Mimi naamini yupo anajifunza. Na leo alifundishwa sehemu kidogo sasa yeye akahisi topic imeisha.

Ila akiendelea kujifunza zaidi na zaidi ataelewa matumizi sahihi ya hizo articles.
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
7,647
2,000
Maneno "a" pamoja na "the" ni kifungu cha mameno ambayo huwa yanatumika kama utambulisho wa nomino katika lugha ya kiingereza .utofauti wa haya maneno mawili ni:-
"A" hutumika kutambulisha nomino ambayo haina umbo maalum.kwa mfano:- tuchukue nomino ambayo haina umbo maalum kama "maji" basi sentensi itakuwa, "this is a water from indian ocean".hatuwezi kusema "this is the water from indian acean.
"THE" ni kinyume cha "A" ambapo hutumika kwa ajili ya utambulisho wa nomino ambayo ina umbo maalum hapa tutumie kitabu sentensi yetu itakuwa ni, "this is the book".hatuwezi kusema "this is a book
nafikiri nitakuwa kidogo nimetoa darasa kwa ambao walikuwa wakichanganyikiwa juu ya maneno haya mawili.
"A" hutumika kwenye Umoja (singular)
I need A coat (koti ni moja)
 
Paula Paul

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
3,417
2,000
Nadhani hiyo ni mbinu mbadala ya kuomba kufundishwa au kupima kama unachojua kiko sahihi.

Kwa michango ya watu humu naona kabisa amefanikiwa.
Seconded!
Nimekumbuka kuna lugha nilikuwa najifunza, kila nikiona nimeweza naenda kwenye Forums zao za ndani (wanaoongea lugha husika) naenda kupima uelewa wangu. Wananirekebisha narudi najifunza tena. Baada ya kuweza nikafungua Username mpya na sasa tuna chitchat kama vile ni mzawa wa hiyo lugha.
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,613
2,000
Nadhani hiyo ni mbinu mbadala ya kuomba kufundishwa au kupima kama unachojua kiko sahihi.

Kwa michango ya watu humu naona kabisa amefanikiwa.
Basi haka kadenti kajanja sana....

Unajua shule zilikuwa zimefungwa, madogo wamekuja na style ya kijanja ya kufuta ujinga...
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,613
2,000
Seconded!
Nimekumbuka kuna lugha nilikuwa najifunza, kila nikiona nimeweza naenda kwenye Forums zao za ndani (wanaoongea lugha husika) naenda kupima uelewa wangu. Wananirekebisha narudi najifunza tena. Baada ya kuweza nikafungua Username mpya na sasa tuna chitchat kama vile ni mzawa wa hiyo lugha.
Lazima kitakuwa kiitaliano... LOL
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
14,294
2,000
Seconded!
Nimekumbuka kuna lugha nilikuwa najifunza, kila nikiona nimeweza naenda kwenye Forums zao za ndani (wanaoongea lugha husika) naenda kupima uelewa wangu. Wananirekebisha narudi najifunza tena. Baada ya kuweza nikafungua Username mpya na sasa tuna chitchat kama vile ni mzawa wa hiyo lugha.
Hongera aisee, mimi ni mbovu sana kwenye kujifunza lugha.

In fact sina hata lugha moja nayoifahamu kiufasaha kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom