Je, wajua matumizi ya "A" na "THE" katika lugha ya kiingereza?

Hizo ni articles.kuna articles za aina 2
1.Definite artile' the'
2.indefinite articles "an,a"
Nipe ufafanuzi kila kazi zinavyofanya kazi,au ukasome zaidi
 
Maneno "a" pamoja na "the" ni kifungu cha mameno ambayo huwa yanatumika kama utambulisho wa nomino katika lugha ya kiingereza .utofauti wa haya maneno mawili ni:-
"A" hutumika kutambulisha nomino ambayo haina umbo maalum.kwa mfano:- tuchukue nomino ambayo haina umbo maalum kama "maji" basi sentensi itakuwa, "this is a water from indian ocean".hatuwezi kusema "this is the water from indian acean.
"THE" ni kinyume cha "A" ambapo hutumika kwa ajili ya utambulisho wa nomino ambayo ina umbo maalum hapa tutumie kitabu sentensi yetu itakuwa ni, "this is the book".hatuwezi kusema "this is a book
nafikiri nitakuwa kidogo nimetoa darasa kwa ambao walikuwa wakichanganyikiwa juu ya maneno haya mawili.

This is a water? Hapana kamanda !!!

1. A - kama kiambishi hutumika kwa nomino zinazohesabika na kamwe haiwezi kutumika katika nomino zinazoelezea vitu visivyohesabika kama maji.

This is a water
This is water

2. A - kama kiambishi hutumika kwa nomino ili kutoa taarifa za jumla tu.

This is a book (Hiki ni kitabu)

2. The - kama kiambishi hutumika katika nomino zinazorejelewa au zinajulikana tayari. Zinaweza kuwa zinahesabika ama la!

This is the water that I drank (Haya ni maji niliyokunywa)

This is the book (Hiki ni kitabu ila kitabu hiki kinajulikana na kinakuwa kimezungumziwa au kutajwa kabla)

3. The pia hutumiwa kwenye nomino peke (mf. Jua, mwezi n.k)

The sun is extremely hot today

The clouds are covering the moon

Angalau tuanzie hapa
 
huwa naangali series na zile za Philippines huwa naangalia zenye subtitles basi
Okay,
Kwa kuanza download movies na subtitles. Halafu usijiweke tuu kwenye kusoma subtitles wasikilize pia. Itakusaidia kujua namna wanavyotamka maneno.
Mpaka movie iishe unajaribu kuirudia bila subtitles utaona mabadiliko.

Jaribu movies kutoka nchi mbali mbali maana kila nchi ina accents zake. Wengine ni rahisi kusikika wengine ni ngumu.
 
Ila kiswahili nacho ni kigumu sana.
Zinazorejelewa, za jumla, kiambishi. ew!!!
 
Lakini pia "the" huwekwa ktk nomino/jina ambalo Mimi mtamkaji na wewe msikilizaji tulifahamu au tunafahamu vizuri hicho kitu au jina lililotamkwa.Hii "a" Ni pale ambapo jina au nomino sio maalum au daaah...sijui nisemeje hapa ,kufundisha nako kazi sana Yan.
Hapa ndipo nilipokuwa nimesimama mwanzo
 
Nimesoma, lakini wewe hauoni hivo vitu ni vigumu? Namaanisha sio kiswahili cha kawaida kinachoongelewa na kila mtu.
Na hapo bado hatujaanza mambo ya viambishi yambwa, mofimu changamano, viambishi tamati yakinishi, ukanushi rejeshi

Ni sawa tu na kwenye sarufi ya Kiingereza. Mambo ya relative clauses, object markers, null traces, propositional phrases....

Kila taaluma ina kilugha chake tofauti na lugha ya kawaida ya kuzungumza mtaani. Madaktari na mainjinia wakianza lugha yao ndo kabisaaa mtu huelewi cho chote...Wanasheria hali kadhalika...
 
"relative clauses, object markers, null traces, propositional phrases".
Hizi zinapatikana kwenye English?. Basi hamna palipo na nafuu. Lol
 
Back
Top Bottom