Je, wajua kwanini CCM haikuwachukua mawaziri wa elimu katika ziara zake za mikoani?

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,091
1,195
Katika kile kinachoonekana kuwepo kwa ombwe kubwa la uongozi hapa nchini, hivi karibuni chama tawala CCM imemua kufanya ziara mikoani ikambatana na mawaziri wanaongoza wizara mbali mbali kwa lengo la kutoa mrejesho kwa wananchi kuhusu utendaji wa Serikali yake. Ni ukweli usiopingika kwa elimu ni nyenzi muhimu sana ya kupambana na umaskini na karibu kila kaya hapa nchini ina watoto au wajukuu wanaosoma shule; hivyo elimu kuwa kipaumbele cha kwanza kwa mzazi au kaya yeyote.

Cha kusikitisha katika mrejesho huu wa CCM suala la elimu haligusiwi kabisa kwa maana ya Mawaziri wa Elimu hawakuhusishwa katika ziara hizi. Hii ni dharua kubwa kwa mamilioni ya watanzania wanaogaragazwa na CCM katika lindi la umaskini wao wenyewe, watoto wao na wajukuu.

Haya ni matusi kwa mamilioni ya watanzania kwa kuwa wote waliopanga, wanaofanikisha na wanaopanda majukwaani katika ziara hizi zisizogusa vipaumbele vya watanzania watoto wao hawasomi Shule za Msingi ambazo wanafunzi hukaa chini, Sekondari za Kata zisizo na waalimu, maabara wala hawatibiwi katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za Serikali zisizokuwa na vifaa vya tiba vya kutosha, dawa n.k. Hivi sasa idadi kubwa ya watoto wa Kitanzania wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Sababu ya hali hii ni CCM na Serikali yake kutoipa kipaumbele Sekta ya Elimu kwa kuitengea fedha kidogo katika bajeti. Wakati mwaka 2008/9 Serikali ilitenga kiasi Bilioni 344 kwa ajili ya sekta ya elimu, kiwango kimekuwa kikipungua kila mwaka. Mathalani, mwaka 2009/10 ilitenga Bilioni 302 tu, na 2010/11 imetenga Bilioni 238 tu.

Wakati hali ikiwa hivyo katika sekta ya elimu, CCM na Serikali yake waliojigamba hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa CCM wa 8 mjini Dodoma kuwa wanaweza kutoa elimu bure hadi ngazi ya Sekondari katika bajeti ya 2012/13 wametenga Bilioni 193.86 tu kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Elimu (sawa na 8.5% ya bajeti nzima Sekta ya Elimu) ikiwa ni pungufu kwa Bilioni 2.39 ya bajeti ya mwaka jana. Bajeti ya maendeleo ndio hutumika kujenga au kukarabati madarasa, kununua au kutengeneza madawati n.k.

Wakati CCM na Serikali yake ikitenga 8-9% ya bajeti ya Elimu kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Elimu, nchi jirani ya Uganda imekuwa ikitenga kati ya 20-24 ya bajeti ya Elimu kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ya katika sekta ya Elimu. Huku Kenya ikitenga kati ya 14-15 ya bajeti ya Elimu kwa ajili ya miradi ya Maendelo katika sekta ya Elimu. (PER, 2011, Kenya), (Madina et al, 2011). Hivyo haishangazi kukuta watoto wa kitanzania katika nchi iliyosheheni raslimali lukuki wakijazana kati ya 65 -73 katika darasa moja, wakikaa chini kwa ukosefu wa madawati wengine wakisomea katika mabvu za mbwa, chini ya mti n.k. CCM na Serikali yake pia wametenga Bilioni 2089.14 kwa ajili ya matumizi ya kawaida (sawa na 91.5% ya bajeti nzima ya Sekta ya Elimu) ikwa ni ongezeko la Bilioni 240.39 ya bajeti ya mwaka jana. Fungu hili la “Matumizi ya Kawaida” pamoja na kutumika kulipa mishahara ya watumishi, kiasi kikubwa sana cha fedha zinzotengwa katika fungu hili hutumiwa vibaya katika matumizi mbali mbali ya ovyo yenye sura ya kifisadi kama vile “kulipana posho za kukaa” (Sitting Allowance).

Viongozi na watendaji wa juu wa Serikalini ambao kazi wanazolipiwa mishahara huhusisha kuhudhuria mikutano, akitoka ofisini kwake na kuhudhuria kikao ofisi ya pili hulipwa posho ya kati Shs 100,000/= hadi 1,000,000/= kulingana na cheo cha mtumishi, kwa mikutano ya masaa machache katika siku; na pengine huhudhuria vikao viwili na hata vitatu kwa siku na huko kote hujichotea posho na mwisho wa mwezi mshahara wake upo pale pale ukiambatana na posho zingine lukuki kama vile kulipiwa maji, umeme, nyumba n.k.

Matumizi mengine ya ovyo kabisa yenye sura za kifisadi ni safari zisizoisha na zisizo na tija ambazo hufanywa na mawaziri na viongozi wengine wa Serikali. Mathalani mawaziri wakitembelea majimbo yao hutumia magari ya Serikali na hulipwa posho wao wenyewe na madereva wao pamoja na magari kujazwa mafuta kwa gharama za Serikali ilihali waziri huyu kama Mbunge tayari keshalipwa posho ya gari na dereva kutoka kodi za wananchi huko bungeni, Je huko kwenye majimbo yao kuna kazi gani zinazohusisha majukumu ya kiwaziri? Kama wabunge wengine wote wanatumia usafiri binafisi kuzuru majimbo yao ni kwanini mawaziri watumia kodi zetu kuzuru majimbo yao kwa gharama za Serrikali? Haishangazi kuona kila wiki mawaziri waka barabarani badala ya kufanya kazi kupambana na umaskini wan chi na kutatua kero za wananchi.

Katika mlolongo huo wa matumizi ya kifisadi ya CCM na Serikali yake Maafisa waandamzi Serikalini huzua safari za mikoani na hata nje ya nchi kwa ajili kuhudhuria mikutano, semina, warsha, makongamano n.k na kujichotea mamilioni ya Dola na Shilingi za Kitanzania kwa njia ya posho, tiketi za ndege hulipiwa, magari ya Serikali yanayotumika hujazwa mafuta, madereva na wasaidizi kulazimika kulipwa posho na malipo mengine kwa safari hizi zisizo na tija. Matumizi yote haya yasiyo ya lazima ndio hupelekea Serikali kushindwa kuwapatia wananchi huduma za jamii za kiwango cha kuridhisha.

Katika bajeti ya 2012/13, Wizara ya Elimu inatazamiwa kutumia Bilioni 320.4 kwa ajili ya matumizi ya kawaida huku kiwango kikubwa kikienda katika matumizi ya kifisadi yaliyotajwa hapo juu. Kiwango hiki ni zaidi ya bajeti ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa Bilioni 120.4. Wakati matumizi yasiyo ya lazima yakitengewa fedha nyingi kiasi hiki CCM na Serikali yake wanashindwa kutekeleza kwa vitendo ahadi waliyojiwekea wenyewe toka mwaka 2002 ya kumpelekea kila mtoto aliyeko Shule ya Msingi Shs 10,000/= tu kwa mwaka kwa ajili ya Shule kununulia vitabu, vifaa vya kufundishia, kukarabati majengo na kununua madawati na kuchapa mitihani.

Tanzania inakadiriwa kuwa wanafunzi Milioni 10 katika Shule za Msingi. Kama kila mwanafunzi atatumiwa Shs 10,000/= tu (japo kiwango hiki ni cha 2002, ili mtoto aweze kusoma vizuri hakitoshi) zinahitaji Shs Bilioni 100 tu. Hii ni sawa na 31% tu ya Bilioni 320.4 zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Wizara ya Elimu. Utafiti unaonyesha kuwa licha ya CCM na Serikali yake kutenga fedha nyinga kwa ajili ya posho, safari, mafuita na matumizi mengine yasiyo na tija, Shule za Msingi nyingi jijini Dar es Salaam mwaka 2010 zilitumiwa wastani wa Shs 4,000/= tu kwa kila mwanafunzi; huku kwa shule za mikoani kiwango hiki kikifikia pungufu ya Shs 1,000/= kwa kila mwanafunzi. Waalimu wamekuwa hawalipwi malimbikizo ya mishahara, malipo ya likizo, fedha za uhamisho posho mbali mbali wanozostahili kisheria.

Laiti kama CCM na Serikali yake wangekuwa na mapenzi ya dhati kwa maskini wa nchi hii upo uwezekano wa kupunguza matumizi yasio ya lazima kama vile posho za kukaa, safari zisizo na tija, matuimizi ya mafuta, vitafunwa n.k na hivyo kuokoa 20% ya kiasi kilichotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida katika Wizara ya Elimu, hivyo kiasi cha Bilioni 64 kinaweza kuokolewa. Kiasi hiki kinaweza kujenga maabara 1,280 kwa ajili ya Shule zetu za sekondari kwa gharama ya Shs Milioni 50 kila moja.

Kama katika bajeti ya Sekta ya Elimu waalimu nao wangekuwa wanatengewa posho hizi hali ingekuwaje katika ari ya ufundishaji? Kuna mtoto wa Mtanzania angemaliza darasa la saba bila ya kujua kusoma na kuandika? Kama kweli CCM inawapenda watanzania ni kwanini iendelee kuwarundikia mishahara minono na posho lukuki kundi dogo la viongozi wa serikali badala ya fedha hizo kutumika kupandisha mishahara ya waalimu ili waongeze ari ya kufundisha watoto wa kitanzania maskini?

Matokeo yake CCM na Serikali yake wanawaacha wazazi kurundikiwa michango lukuki kama vile kulipa mlinzi, madawati, ukarabati wa madarasa, kuchapa mitihani n.k na shule zetu za msingi zikiwa hazina madarasa ya kutosha, hazina madawati, hakuna vitabu na vifa vya kufundishia, hakuna vyoo, hakuna maji mashuleni, waalimu wankaa chni ya miti kusahihisha mazoezi ya wanafunzi kwa ukosefu wa ofisi na samani, wanafunzi wanrundikwa kati ya 65-73 kwa darasa moja, watoto wa kitanznia wankaa chini, mwalimu mmoja kwa wanafunzi 55 na mapungufu mengine lukuki. Hii ni aibu katika nchi iliyosheheni raslimali kibao ikiwemo madini, ardhi, mito, bahari, mbuga za wanyama n.k
 

Attachments

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,495
1,250
Kwenye ELIMU wanajua hawajafanya lolote la maana:
-Hizo zinazoitwa ni shule hazina hadhi yoyote ya kuitwa hivo;
-Walimu na matatizo yao ni mengi mno;
-Tuko katika kiwango duni sana cha utoaji wa elimu;
-Elimu inahudumiwa na wizara zaidi ya mbili. Hali inayozua mikanganyiko;
-Tumeshindwa kabisa ku-regulate ELIMU. Elimu imetupwa sokoni kama nyanya;
Kinana na wenzake ni wajanja sana. Wanajua ni nini wapeleke majukwaani na kupata umaarufu na ahueni ya muda. Mpango uliopo ni kuzimaliza kabisa shule za UMMA kitaaluma ili watu wafanye biashara yenye faida kubwa ya kuuza ELIMU!
 

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,066
1,500
Lakini ndo wanazisifia kuwa zimekomboa wanyonge sababu vijana wengi wanaandikishwa kama shule za msingi na kuandikisha vijana wengi sekondari .pamoja na changamoto watotot sasa wanasoma badala ya kuwa wafanyakazi wa ndani, kuwa wachuuzi mitaani.Kimsing hata hao iliyoenda nao kuna kipi zaidi ya propanganda?mfano wameenda mtwara , lakini mbona walimacha huko waziri wa kilimo na chakula huko mtwara akijaribu kuzima suala la kuchelewa kupata mkopo, uafanisi mdogo wa stakabadhi gaharani msimu uliopita.Kimsingi zao la korosho limekumbwa na misusuko mingi huku kukiwa na bodi la korosho iliyokuwa ikilalamikiwa kwa kutumia fedha nyingi bila sababu.Kuna tatizo la mabadiliko ya dawa ya kupuulizia dawa mikorosho, soko na usimamizi wa bei , malipo ya stakabadhi gharani.haya hata huko geita ndo walipokutana na kuzomewa na hata hao wanaccm huko walikuwa wakilalamika waziwazi utendaji mbovu, sasa huyo waziri ataweza kusimamia kila kitu?Kimsingi hata hao waliodamana na kinana si kwamba warejesha khali ya kinachoendelea serikalini.hakuna badala yake ni propoganda zisizo na mashiko.Mbona hata sumbawanga waliishia kuzomewa!Tunachojua hii ni bingo kwa watendaji hao na sekretariati kwa kupata viposho.Lakini hakuna kitu ni kuwahadaa wananchi, kwa kuwapa ghiriba ambazo zimepitwa na wakati.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,297
2,000
Chengi ya rada iko wapi?

Bila elimu bora, watanzania tutaendelea kuwa masikini

Masikini ndo mtaji wa mafisadi ili waje wanunue kura
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
..inawezekana wakati huu ni msimu wa ngoma.

..wananchi huko vijijini hawana muda wa kusikiliza masuala ya elimu.
 

kimeloki

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
2,688
2,000
miaka michache iliyopita serikali ilikuwa na shule nzuri na bora sasa imekuwa historia.
 

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,384
2,000
Mawaziri wa elimu wa nini unataka wawapotoshe wanafunzi wetu? ushaona waziri hajua hata Tanzania ilitokana na muungano wa nchi gani,sasa waziri kama huyo utataka akawaambie nini wanafunzi wake
 

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,091
1,195
Hoja kama n hii niliyotoa ndio hoja wapenzi wa Chadema walitakiwa kuzitumia kuibana CCM kisawasawa. Lakini ni lazima kwanza tujitolee kuwaelimisha wananchi ili waweze kufikiri na kuchanganua hoja hii yenye maslahi kwa watoto wapate kuielewe Bilioni 100 nilizotaja hapo juu maana yake nini ikilinganishwa na matumizi mbali mbali ya Serikali ya CCM. kwa hakika hizi ni fedha kidogo sana kulinganisha na bajeti ya Serikali.Lakini kazi hiyo haiwezi kufanyika kupitia viongozi wa CDM , "Operesheni Sangara" "M4C" n.k pekee ni lazima kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii ikiwemo watoa matusi Chadem ainaposemwa humu JF wafanye kazi hiyo kila mtu akatika mtaa/kijiji chake.

Kila anayejisikia ni mpenzi wa Chadema alitakiwa kuchukua taarifa hizi na kuzipeleka kwa waanachi piopote tulipo kwa na kuwaelimisha wananchi ili waendelee kiunga mkono Chadema, badala ya kubabaishwa na barabara pekee. Mtanzanai maskini atafaidika zaidi kama mtoto wake atapata elimu ya kutosha hata kama ni ya ngazi ya msingi na kisha kuweza kutumia barabara zinazojengwa kujiondolea umaskini. hali ilivyo sasa mfumuko wa bei watanzanai maskini hawataweza kufaidi matunda ya barabara hizi kwa kuwa hawataweza kumudu gharama ya nauli, vyombo vya usafiiri n.k. Kwa maneno mengine CCM inaytumia umaskini wa na ujinga wa watanzani kuwadanganya kuwa watanufaika na hizi barabara; kama watoto wa watanzania hawa maskini hawataelimishwa vya kutosha, ni dhahiri kuwa barabara hizi zinzjengwa ili kutumiwa na wawekezaji na sio watanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom