Je wajua kwamba - Serikali ya Muungano haisaidii ruzuku kwa SMS kujiendesha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wajua kwamba - Serikali ya Muungano haisaidii ruzuku kwa SMS kujiendesha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teamo, Jul 13, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ''..kwa mujibu wa hoja iliyotolewa kwenye bunge la baraza la wawakilishi leo na waziri husika,ni kwamba serikali ya muungano haitoi msaada wowote wa ruzuku ili kuisaidia SMZ kujiendesha...''ITAENDELEA!

  wewe jiulize tu kama 'madai ya wazanzibari ' kuhusu marekebisho ya baadhi ya vipengele vya makubaliano ya muungano ni genuine?au inakuwaje?

  ................stay tuned!
  Nitarudi
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huku hawataki Muungano, huku wanataka wasaidiwe ruzuku, hawaeleweki! Wanaleta hoja ya ruzuku ili kufunika suala la mafuta na gesi asilia ambalo wanajifariji kwamba wameliondoa kwenye orodha ya mambo ya Muungano bila kufuata taratibu!
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unazungumza nini Mheshimiwa? Hivi Zanzibar lini wameomba ruzuku kutoka Serikali ya Muungano. Lakini uelewe Zanzibar hawaombi, wanadai kurejeshewa kile ambacho ni haki yao. TRA inakusanya kodi Zanzibar-kodi inapelekwa wapi? Ndiyo wanaomba vitu kama hivyo virejeshwe Zanzibar. Msaada unatolewa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -unakwenda wapi? Wanaotoa wanasema Tanzania wakijua fika kuwa na Zanzibar imo . Jee mnawapa?
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kwa hiyo ule magao wa 4% wanayopata kutoka hazina ya Tanzania kila mwezi ya jumla ya mapato yote haiwatoshi tu?? Zanzibar kuna watu wangapi kati Mil.35 waliopo Tanzania !!!!!!!! Watu hawazidi 1.5Mil. wanapata 4% huoni ni nyingi sana hizo mnawadhulumu watu wa Shinyanga!!!
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe!!! sisi siyo Shinyanga . Sisi ni Nchi. Hujaelewa tu? Ukipambana na vichwa ngumu wanakwambia tuwachieni tunaweza kupata zaidi ya hiyo asilimia yenu 4.
   
 6. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hebu angalia kwenye ramani, au google hapo ulipo kama Duniani kuna nchi inaitwa Zanzibar!!!
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huo uchokozi .....
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii ndiyo hoja inayotakiwa Wazanzibar waizungumzie...Ni haki yao kukatiwa ruzuku toka pato la Taifa kama sehemu yao halali ya muungano wa nchi mbili..
  Lakini pia wakumbuke ni lazima nao watoe mchango ktk mfuko wa Taifa sii mchezo ule wa changu Changu, chako Changu!
  NMi muhimu yafanyike marekebisho makubwa ktk ukusanyaji wa kodi ili ifahamike fungu la serikali mbili hizi toka ktk mfuko wa Taifa..NI LAZIMA iundwe serikali ya Bara kuwezesha zoezi hili laa sivyo tutakuwa tunajenga juu ya Kichuguu..
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hilo la ruzuku lipo kwenye makubaliano ya awali ya Muungano au liliwekwa 'kinyemela' kama idaiwavyo kwenye suala la mafuta na gesi asilia?
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Fanya marekebisho ya mada hii, pls! SMZ badala ya SMS! Usiwape nafasi watu kuanza kujadili title wakaacha hoja ya msingi!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Haki gani wanayodai Wazenj na kwa nani? Kila kukicha laja jipya. Ukiona hivyo kuna mawazo mufilisi.
   
 12. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Jamaa ana wake ng'ombe 99 na mimi nina ng'ombe 1 anasema tuchanganye tufanye biashara, wana JF naomba mawazo yenu.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..mtoa mada ana ripoti kuhusu habari niliyowawekea hapa toka Tanzania Daima.

  ..Zanzibar inapata misaada toka kwa Wafadhili, pamoja na gawio toka Hazina ya Muungano.

  ..Zanzibar ni sehemu ya Muungano. wanapotosha kwa kudai hawawakilishwi ktk mgawanyo wa mapato ya muungano.

  ..Zanzibar wamekuwa wakipewa umeme bure, au wakiuziwa kwa bei poa. pia serikali ya Tanganyika mara kwa mara imekuwa ikilipa mishahara ya watumishi wa SMZ. kwa mtizamo wangu hiyo ni RUZUKU.

   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sina hakika kama unaelewa unaachokiongea, hiyo 4.5% unayosema ni kasma ya magawanyo ya misaada ya kibajeti iliyoshauriwa na wafadhili, mpaka muda huu formula ya kugawana mapato katika vyanzo vya Muungano ambayo zanzibar inachangia hakuna, tume ya pamoja ya fedha iliyoundwa imesha wasilisha ripoti yake juu ya tatizo hili, ambapo mpaka sasa katika kugawana mapato ya muungano tunatumia formula hiyohiyo ya inayotumika katikia misaada ya wafadhili kwa muda tu, mpka hapo serikali zitakapo tolea tamko ripoti ya tume ya pamoja ya fedha.
  Na kuhusu hiyo habari hapo juu alichosema waziri wa fedha na uchumi zanzibar Dr. Mwinyihaji, ni kuwa SMT haitowi fungu lolote kuchangia bajeti ya zanzibar kutoka bajeti yake, sasa kuna tatizo gani wakati huo ndo ukweli? Na si kuwa wanalalamika la hasha! alipokuwa najibu swali hilo alitaka kumuhakikishia muulizaji kuwa zanzibar inaandaa bajeti yake bila ya kutegemea msaada wa Tanganyika ambao wao wenyewe hawajijuwi hawajitambui kama sisi. Bakuli mkononi kila kukicha! Ila wao ni wezi sana tu!

  Naona kazi pevu aliyokuwa nayo mwalimu wako wa jiografia na historia ulipokuwa shule!

  No si uchokozi anaonyesha kiwango chake cha uwelewa wa historia ya taifa lake na jiografia, usishangae ikawa ndo miongoni mwa hao wanapita mitihani ya shule kwa kughushi majibu kwa kununuwa mitihani. Taifa hili linafisidika kwa mengi ati mpaka thinkings za raia zake kama hawa zinapinda pinda.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..kulingana na kauli ya Maalim Seif waZenj wanakatiwa fungu toka serikali ya Muungano.

  ..tatizo ni kwamba hawakubaliani na kiwango cha mgao huo. wanataka wapewe asilimia 10% ingawa kwa idadi yao na ukubwa wa uchumi wao hawastahiki kiwango hicho.

  ..pia inaelekea hawachangii chochote hawa kama anavyoelekeza Maalim Seif. kama wangekuwa wanachangia hawa asingelala mtu kwa kelele zao.

  ..pia wakiulizwa kwanini hawatoi fungu lolote kusaidia matumizi ya taasisi za Muungano wanaanza kuleta maneno na kucheza na lugha.

  ..anauliza mchango wa Tanganyika uko wapi !! sasa askari, ofisi za ubalozi etc wanalipwa na nani kama siyo Tanganyika wanaotoa fedha hizo.

  ..tumewadekeza hawa.

  ..WABUNGE WA TANGANYIKA VUNJENI MUUNGANO.

   
 16. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naona una matatizo ya kuelewa wakati unasoma, Unachopinga na unachokubali ni nini sasa!!! Mara unasema hawapati chochote toka hazina zaidi ya fedha za wafadhili, mara unakubali tunagawana fedha za hazina kwa kutumia formula ya fedha za wafadhili!!!

  Inaonesha ulivyona na kichwa kigumu kama kambale!, sometimes kama umeishiwa cha kuandika unaweza ukapita kwa kusoma tu bila kuchangia wala siyo kosa na hakuna atakayekuuliza, kuliko kubisha kitu na kukubali tena mwenyewe. Watu watakuona kama mwenda wazimu. Kama kweli umesoma ungekuwa umeshajigundua kosa lako!!

  Nawasiwasi na elimu yako, kwani mara nyingi mtu asiyesoma hupenda kujisifu kuwa yeye ndiye, na wenyewe wenye elimu zao hata siku moja hawajitangazii.
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ni kwamba serikali ya muungano haitoi suzuku ya SMZ KUJIENDESHA!narudia,RUZUKU KWA AJILI YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUJIENDESHA!
   
 18. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Punguza ghadhabu kwa huyo ndugu yangu. Be fair please!
   
 19. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili suala ni pana kabisa. SMZ ina jukumu la kuwahudumia Wazanzibari katika mambo yale ya kijamii (elimu, afya, makaazi, kilimo, uvuvi, na kadhalika). Mambo hayo niliyoyaorodhesha hapo wa-Tanzania bara (Wa-tanganyika) wanahudumiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(ambayo ni yetu sote hata sisi kule Zenj) sasa kwa nini Serikali hiyo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inafumbia jicho kuwahudumia Wazanzibari katika mambo hayo -sawia na wenzao wa bara. Hapo ndio maana tunasema Bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima iwe na kasma ya kuhudumia Watanzania(Wazanzibari) katika hayo mambo ya elimu, afya, na mengineyo- Hiyo kasma iite kwa jina la ruzuku kama unapenda.
   
 20. t

  tishekwavb Member

  #20
  Jul 15, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuu!! hizo mbona ni mgao mkubwa!! Yaani wanataka mafuta wachukue wao, ruzuku wachue 4% na TRA wasikusanye kodi. Sasa hiyo 4% itoke wapi kama mafuta ni yao, TRA hakusanyi kodi, tunalipa mshahara majeshi ya Tanzania ambayo yanalinda Zanzibar, tunalipa wabunge wao wanaowawakilisha bunge la Muungano, tunasomesha watoto wao elimu ya juu. Halafu wanachukua 4% kwa idadi ya watu sawa na Wilaya moja ya Bara. Sasa tugawe sawa mgao kulingana na idadi ya watu huone kama hakuna upendeleo kwa Wazanzibar na khali hakuna uchumi walio nao uko visiwani. Kumbuka hiyo 4% inatoka kwenye madini yetu, pamba, kahawa, korosho utalii wa mbuga zetu, uvuvi toka maziwa yetu. Mimi naona waondoke na wabaki na mafuta yao na sisi tuna gesi na mafuta hivi karibuni tutapata
   
Loading...