Je wajua kwamba sayansi haina majibu ya mambo haya?

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,982
2,915
Hivi unajua kwamba mpaka sasa japo kuwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia kuwa ya kiwango cha juu bado sayansi haijaweza kuthibitisha kwa hakika kuna sayari ngani kwenye mzunguko wetu wa Solar system.

Pluto iliondolewa katika hesabu ya sayari kwasababu haina sifa ya kuwa sayari kwasababu ni ndogo sana. Hivyo mtu akiulizwa kuna sayari ngapi asiyejua kuwa Pluto iliondolewa atasema kuna sayari 8 na anayejua atasema 7. Ila ukweli ni kwamba sayansi haijaweza kuthibisha kwa hakika kuna sayari ngani katika mfumo wetu wa jua.

Pia kuna watu wanaodai sayari ya Venus siyo sayari bali ni nyota mfu ambayo ipo siku italipuka na kumeza sayari zote.

Namba yoyote ya sayari inayotolewa na wanasayansi juu ya idadi ya sayari kwenye mfumo wetu wa jua, ni namba ya kubahatisha. Japo vimetengenezwa vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kutafuta na kunasa sayari zilizo umbali wa mamilion ya miaka ya kasi ya mwanga (light years), lakini bado sayansi imeshindwa kujua kwa hakika idadi halisi ya sayari zilizopo katika mfumo wetu.

Kuna maeneo mawili hasa ambayo yanaleta tatizo.

Eneo la kwanza ni kati ya jua na sayari ya Mercury (Zebaki). Eneo hili ni vigumu sana kuona kuna kitu gani kwakuwa kuna mwanga mkali wa jua hivyo hata kwakutumia vifaa kama Darubini kali zilizoko angani ni vigumu kuona chochote.

Eneo la pili ni eneo kuanzia sayari ya Venus kwenda mbele, eneo hilo kuna giza nene ambalo linaleta ugumu wa kuona chochote kilichopo eneo hilo. Njia inayotumika kugundua vito vilivyopo eneo hili ni kwa kutumia njia inayojulikana kama Mapping the trajectory of asteroids. Kwa data zilizo kusanywa kwa kutumia hii njia zinaopnyesha kwamba kuna uwezekano kuna sayari baada ya 50 asteroid nomical units (kipimo cha umbali) kutoka kwenye sayari ya Pluto.

Na pia kuna dalili za uwepo wa Sayari kubwa mara nne ya Jupiter huko. Na jambo linguine la kusahangaza, kuna theory ilianzishwa na mwanafizikia ajulikanaye kama Richard A. Miller inayodai pia kuna uwezekano wa uwepo wa jua linguine huko kwenye mfumo wetu.

Je wajua kuwa wasayansi wanajua mambo mengi kuhusu anga za juu kuliko ni kitu gani kinaendelea chin mwa bahari?

Japokuwa madai haya ni madai ambayo hayawezi kuthibitishwa kwa vipimo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mwanadamu hajui mambo mengi kuhusu kina kirefu cha bahari. Zaidi ya asilimia 95 ya bahari haijaweza kuchunguzwa kwa kiwango cha kuridhisha. Na inasemekana kati ya 1/3 mpaka 2/3 ya viumbe walioko baharini hawajaweza kugunduliwa kwasababu vinaishi kwenye kina kirefu cha bahari.

Utajiuliza ni kwanini inakuwa hivyo kwani hakuna vyombo vya uzamiaji?

Jibu ni kwamba siyo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria. Eneo la bahari ambalo linajulikana kwa kuwa na kina kikubwa linaitwa Challenger Deep linalopatikana katika Bahari ya Pacific Kusini mwa Meriana trench. Eneo hilo lina kina cha futi 38,200, hili eneo limeweza kutembelewa na vyombo alivyotengeneza mwanadamu mara nne tu wakati binadamu kafanya safari za kupeleka vyombo mwezini mara sita.

Lakini katika hizo mara nne kila chombo kulipozama eneo hilo walivumbua viumbe vipya. Mara ya mwisho kutembelea huko mwezi wa 5 mwaka 2016 kwa kutumia chombo kisichokuwa na binadamu kijulikanacho kama Deep Discoverer, kiligundua aina mpya ya jerry fish ambayo haikuwa inajulikana kabla.

Je wajua baiskeli inafanyaje kazi?

Ukimuuliza mtu yoyote jinsi ya kuendesha baiskeli atashangaa mbona ni swala rahisi, ni kiasi cha kuipanda na kukanyaga pedo baiskeli itaanza kusonga.

Lakini je ni kitu gani kinaifanya baiskeli iweze kusimama kwa matairi mawili ukiwa unaiendesha? Hata sayansi mpaka sasa haina jibu juu ya hilo swali. Maoni yote ya kanuni za kifizikia yanapingana juu ya swala hili la baiskeli kusimama kwa matairi mawili pasipo kuanguka.

Mwanzoni ilidhaniwa kwamba kanuni ya kifizikia ijulikanayo kama Conservation of Angular Momentum ilihusika kuelezea hili jambo sawa na ambavyo gyroscope inavyofanya kazi. Lakini mwaka 2011 kwenye makala ya jarida la Fizikia wahandisi walithibitisha kwamba kanuni za Gyroscope hazikuhitajika katika kufanya baiskeli isimame wima bila kuanguka wakati wa kuiendesha. Pia kanuni nyingine ijuliknayo kama Trail Effect nayo ilionekana haina umuhimu katika majaribio ya wahandisi hao.

Hivyo mpaka kufikia sasa hivi sayansi haijajua ni kitu gani kinaifanya baiskeli isanguke unappokuwa unaiendesha.

Je wajua sayansi haijaweza kujua ni sababu gani binadamu tunatofautiana makundi ya damu?

Kuna aina zaidi ya 20 za makundi ya damu ambayo yanaaminika kuwa binadamu ametokana nayo zaidi ya miaka milioni 20 iliyopita. Japokuwa bado haijulikana kwanini kua makundi haya lakini inajullikana kwamba kila kundi lina tabia tofauti na kundi jingine.

Watu wenye damu kundi A wanashambuliwa kirahisi na small Pox wakati wenye Kundi B wanaadhiliwa kirahisi na bacteria aina ya E.coli ambao mara nyingi huppatikana kwenye utumbo wa wanyama. Ni wazi kuwa kuna uhusiano kati ya uwezo wa kuambukizwa gonjwa flani kirahisi na kundi lako la damu.

Je tofauti na hilo kuna sababu nyingine ya binadamu kutofautiana makundi ya damu? Mfano kuna watu wanaamini atu wenye damu kundi la Rh ni aliens,
 
Umefanya vizur mkuu kutufumbua macho, habar ya hicho kina cha bahar nilkua siijui
 
Hivi unajua kwamba mpaka sasa japo kuwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia kuwa ya kiwango cha juu bado sayansi haijaweza kuthibitisha kwa hakika kuna sayari ngani kwenye mzunguko wetu wa Solar system.

Pluto iliondolewa katika hesabu ya sayari kwasababu haina sifa ya kuwa sayari kwasababu ni ndogo sana. Hivyo mtu akiulizwa kuna sayari ngapi asiyejua kuwa Pluto iliondolewa atasema kuna sayari 8 na anayejua atasema 7. Ila ukweli ni kwamba sayansi haijaweza kuthibisha kwa hakika kuna sayari ngani katika mfumo wetu wa jua.

Pia kuna wanasayansi wanaodai sayari ya Venus siyo nyota bali ni nyota mfu ambayo ipo siku italipuka na kumeza sayari zote.

Namba yoyote ya sayari inayotolewa na wanasayansi juu ya idadi ya sayari kwenye mfumo wetu wa jua, ni namba ya kubahatisha. Japo vimetengenezwa vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kutafuta na kunasa sayari zilizo umbali wa mamilion ya miaka ya kasi ya mwanga (light years), lakini bado sayansi imeshindwa kujua kwa hakika idadi halisi ya sayari zilizopo katika mfumo wetu.

Kuna maeneo mawili hasa ambayo yanaleta tatizo.

Eneo la kwanza ni kati ya jua na sayari ya Mercury (Zebaki). Eneo hili ni vigumu sana kuona kuna kitu gani kwakuwa kuna mwanga mkali wa jua hivyo hata kwakutumia vifaa kama Darubini kali zilizoko angani ni vigumu kuona chochote.

Eneo la pili ni eneo kuanzia sayari ya Venus kwenda mbele, eneo hilo kuna giza nene ambalo linaleta ugumu wa kuona chochote kilichopo eneo hilo. Njia inayotumika kugundua vito vilivyopo eneo hili ni kwa kutumia njia inayojulikana kama Mapping the trajectory of asteroids. Kwa data zilizo kusanywa kwa kutumia hii njia zinaopnyesha kwamba kuna uwezekano kuna sayari baada ya 50 asteroid nomical units (kipimo cha umbali) kutoka kwenye sayari ya Pluto.

Na pia kuna dalili za uwepo wa Sayari kubwa mara nne ya Jupiter huko. Na jambo linguine la kusahangaza, kuna theory ilianzishwa na mwanafizikia ajulikanaye kama Richard A. Miller inayodai pia kuna uwezekano wa uwepo wa jua linguine huko kwenye mfumo wetu.

Je wajua kuwa wasayansi wanajua mambo mengi kuhusu anga za juu kuliko ni kitu gani kinaendelea chin mwa bahari?

Japokuwa madai haya ni madai ambayo hayawezi kuthibitishwa kwa vipimo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mwanadamu hajui mambo mengi kuhusu kina kirefu cha bahari. Zaidi ya asilimia 95 ya bahari haijaweza kuchunguzwa kwa kiwango cha kuridhisha. Na inasemekana kati ya 1/3 mpaka 2/3 ya viumbe walioko baharini hawajaweza kugunduliwa kwasababu vinaishi kwenye kina kirefu cha bahari.

Utajiuliza ni kwanini inakuwa hivyo kwani hakuna vyombo vya uzamiaji?

Jibu ni kwamba siyo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria. Eneo la bahari ambalo linajulikana kwa kuwa na kina kikubwa linaitwa Challenger Deep linalopatikana katika Bahari ya Pacific Kusini mwa Meriana trench. Eneo hilo lina kina cha futi 38,200, hili eneo limeweza kutembelewa na vyombo alivyotengeneza mwanadamu mara nne tu wakati binadamu kafanya safari za kupeleka vyombo mwezini mara sita.

Lakini katika hizo mara nne kila chombo kulipozama eneo hilo walivumbua viumbe vipya. Mara ya mwisho kutembelea huko mwezi wa 5 mwaka 2016 kwa kutumia chombo kisichokuwa na binadamu kijulikanacho kama Deep Discoverer, kiligundua aina mpya ya jerry fish ambayo haikuwa inajulikana kabla.

Je wajua baiskeli inafanyaje kazi?

Ukimuuliza mtu yoyote jinsi ya kuendesha baiskeli atashangaa mbona ni swala rahisi, ni kiasi cha kuipanda na kukanyaga pedo baiskeli itaanza kusonga.

Lakini je ni kitu gani kinaifanya baiskeli iweze kusimama kwa matairi mawili ukiwa unaiendesha? Hata sayansi mpaka sasa haina jibu juu ya hilo swali. Maoni yote ya kanuni za kifizikia yanapingana juu ya swala hili la baiskeli kusimama kwa matairi mawili pasipo kuanguka.

Mwanzoni ilidhaniwa kwamba kanuni ya kifizikia ijulikanayo kama Conservation of Angular Momentum ilihusika kuelezea hili jambo sawa na ambavyo gyroscope inavyofanya kazi. Lakini mwaka 2011 kwenye makala ya jarida la Fizikia wahandisi walithibitisha kwamba kanuni za Gyroscope hazikuhitajika katika kufanya baiskeli isimame wima bila kuanguka wakati wa kuiendesha. Pia kanuni nyingine ijuliknayo kama Trail Effect nayo ilionekana haina umuhimu katika majaribio ya wahandisi hao.

Hivyo mpaka kufikia sasa hivi sayansi haijajua ni kitu gani kinaifanya baiskeli isanguke unappokuwa unaiendesha.

Je wajua sayansi haijaweza kujua ni sababu gani binadamu tunatofautiana makundi ya damu?

Kuna aina zaidi ya 20 za makundi ya damu ambayo yanaaminika kuwa binadamu ametokana nayo zaidi ya miaka milioni 20 iliyopita. Japokuwa bado haijulikana kwanini kua makundi haya lakini inajullikana kwamba kila kundi lina tabia tofauti na kundi jingine.

Watu wenye damu kundi A wanashambuliwa kirahisi na small Pox wakati wenye Kundi B wanaadhiliwa kirahisi na bacteria aina ya E.coli ambao mara nyingi huppatikana kwenye utumbo wa wanyama. Ni wazi kuwa kuna uhusiano kati ya uwezo wa kuambukizwa gonjwa flani kirahisi na kundi lako la damu.

Je tofauti na hilo kuna sababu nyingine ya binadamu kutofautiana makundi ya damu? Mfano kuna watu wanaamini atu wenye damu kundi la Rh ni aliens,
Nafikiri sayansi inayo majibu ila wanasayansi bado hawajayapata.
 
Sayansi pia Haijui hata Kisukari kinatokeaje... Wanachojua ni either Ini linafeli kuconvert sugar au Kongosho kufeli kuzalisha Insulin.. Ila kwanini Ini au Kongosho linafeli Hakuna Jibu
 
Back
Top Bottom