Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Hilo ni suala la kihuni na kilevi..lakini ntakujibu hivi..sikuuliza hati yao ya ndoa kwani wote wawili walinipenda na kunipa malezi mazuri na elimu ya kuweza kupambana na maisha.hivyo sikua na sababu ya kuhoji ..lakini wangeniacha na kuhangaika na ulimwengu na kunitupa kama mtoto wa kambo basi nigedai hati kujua kama kweli wao ni wazazi wangu...ama ni mtoto wa kulea ...
na kama unaleta mfano ndoa katika muungano basi wanandoa wakikosana huachana ....Mkandara ufisadi na uongo na mbini chafu zilizotumikia kufikia muungano ndio mambo ambayo tunataka kuyafuatilia ili mchawi apatikane...
Ahahaha sawa mkuu wangu kaa lingekuwa swali la kihuni na kilevi mbona umelijibu au nawe mlevi na mhuni kama mimi?.. Tuache mas-hala cheti cha ndoa hakiwezi kukuhakikishia kwamba wao ni wazazi wako kwa sababu sio cheti kinachozaa mtoto bali kitendo cha wazazi wako kukutana kimwili.

Hivyo hata kama watakutesa watakutenga ythe Only way kwako wewe kuhakikisha kama kweli ni wazazi wako ni swala la wewe mwenyewe kufanya DNA maana mwenye mashaka ni wewe. Na hata ukikuta hawa ni wazazi wako ama sio wazazi wako bado haitajibu swali gumu ambalo wewe unataka kulifanya nalko ni kujikata. Hivyo basi kama unataka kujikata iwe kwa taabu au mafanikio unaweza kabisa kufanya maamuzi hayo bila ruksa yao..

Na ndivyo tunacvyowaambia ya kwamba Hati ya Muungano baina ya Tanzania na Zanzibar ipo na picha zimewekwa kuonyesha kilichofanyika. Zanzibar wanayo copy yao na Bara na viongozi wetu hawana sababu wala jukumu la kutuonyesha isipokuwa tunaweza kudai kutokuwepo Usiri ktk makubaliano haya kama vile wenzetu Marekani walivyofanya BOFYA japokuwa kizazi hiki hakiwezi kuelewa sababu zilizolazimisha muungano huo ili hata vyuoni wanafunzi wanajifunza sheria wapate kuelewa na wanalinda kitu hiki kwa kupitia sheria uhalali upi. Hata Marehemu Profesa (RIP) aliandika makala zake akijiuliza sababu na utata ulofuatia makubaliano haya..

Maadam tulishaungana na wengi wetu ni kizaiz cha Muungano huo, uhalali wa ndoa hauwezi kabisa kuleta ufumbuzi wa matatizo ya Wazanzibar wala wabara isipokuwa kero zilizopo ktk muungano kama alivyoanisha Profesa ndizo za kuzitafutia Ufumbuzi na kama haiwezekani ni bora mwenye kuitaka talaka kama kweli ni mawazo ya baraza la Mapinduzi basi wajitoe, na kama ni mawazo ya wananchi wa Zanzibar majibu lazima yatoke ktk kiungo cha Muungano wetu nacho ni Baraza la Mapinduzi. Na amini maneno yangu mchawi sii yeyote bali Ukweli usipokubalika ya kwamba serikali ya Zanzibar ina wenyewe na wenyewe ndio hawataki kabisa kusikia habari za kuvunja Muungano maana ndio hifadhi yao wao..

Hawa ndio wabaya wao kama sisi tunavyopambana sasa hivi na CCM bara kutokana na imani waloijenga ya kwamba CCM ina wenyewe na wenyewe ndio watawala. Vita hii naweza sema ilianzishwa na CUF kupambana na viongozi wa CCM visiwani hadi kufikia karibu na ushindi lakini kama wanavyodai CCM wana silaha nyingi na za kila aina. Wakawazidi ujanja CUF kwa kujenga chuki baina ya chama hicho na Chadema wakati hawa wote walikuwa na agenda moja.

Kumwondoa CCM madarakani, hivyo walipojitenga wakifikiria Wazanzibar wanaweza kuwa na UMOJA kudai serikali yao bila kujua kwamba CCM wanajua fika hawakubaliki na wakijitenga CUF itaendelea kupambana na CCM mpya ya Zanzibar sijui wataitwa ASP au nini na uhasama utarudi palepale na itaishia CUF kuchukua madaraka. Hili ni swala ambalo baraza la mapinduzi hawataki kabisa kusikia kama CCM wanavyohaha kusikia Chadema inaweza chukua nchi mwaka 2015.... Akili mu kichwa!
 
Hukunijibu hili suali! umegeuka komba kula embe hili kidogo na lile kidogo japo hana njaa lakini aharibu tu huku akirukia matawi mengine

suali:

Huo muungano uliosema wa OAU wapi umeona TRA / VAT wanakwenda asubuhi kwenye nchi wanakusanya pesa yote ya kodi jioni wanarudi Dar-salaam na vikapu vyao vya pesa. mwisho wa mwezi nchi mnaipa 4% ya hiyo pesa ??? huu kama si umafia ni kitu gani?? Hata mkoloni mweupe alikuwa hafanyi wizi huu

Mkiambiwa mnakuja juu ahhh! hizo ni kero za Muungano , Kwa Mtindo huu kweli vijana wameamua na msifanye mchezo

Tuje hapo uliporukia :

Alikuambia nani maneno hayo , Okello au baba yake Okello , kwa vile hakujua kuandika ndio serikali ikaogopa watu kuutambua ukweli ikapiga marufuku hicho kitabu???

By the way, hata Thabit Kombo hakuandika kitabu ameandikiwa , nikuulize alifika darasa la ngapi???
au kitabu chake tusikisome???

Hayo unayoyaandika umeyatoa kitabu gani ??? HAYO MAANDALIZI YALIKUWEPO ZAMANI NI KWELI NA YANAENDELEA


Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.


ANGALIA HUU MKANDA PIA

Imani Petro Mbinu za makafiri 5 13 - YouTube
KAMwewe, mkuu wangu badop huelewi ya kwamba kuna tofauti baina ya JUMUIYA na MUUNGANO? - Jumuiya ya AU au UN ni kama chama unakubaliwa kujiunga wewe na kwa kila treaties unaweza jiunga au kutojiunga..Lakini Muungano wa nchi hii sio chama ni UNDSUGU kama kula yamin vile hivyo undugu huo hauna mashatri zaidi ya kukubaliana na kupangiana majukumu, mamlaka na kadhalika wakati ktk JUMUIYA hakuna kupangiana mamlaka.


Na uposema ya kwamba TRA wamekwenda kukusanya pesa kisha jioni wanaonsddoka na makapu ya fedha kwenda dar... pengine hili ungenifafanulia zaidi maanake sisi wenyewe huku tunatuma mizigo yetu Zanzibar ambako kuna ushuru nafuu kuliko badari ya tanga au Dar na tukisha pitisha zanzibar tukifika Dar tunalipishwa tena iweje kuwepo na utaratibu huu ikiwa wausanyaji wa ushutru wanatoka bara. Ebu nijuze pengine tunaibiwa kweli na tuanzishe kelele za mafisadi wanaotutoza ushuru mara mbili mbili..
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mmoja wa wale wanaotaka Muungano huu ufe moja kwa moja; huwa sipendi marudio. Nataka ufe, siyo kwa sababu Muungano huo ni mbaya au muungano huo siyo halali bali ni kwa sababu muungano huu unasababisha watu watumie nguvu kubwa kushughulikia jambo ambalo halina maana kabisa katika maisha ya kawaida ya mwananchi wa leo. Ndugu zangu wengi pale Isevya hawajui hata ilipo Zanzibar zaidi ya Singida, lakini wana matatizo mengi yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali ambayo inajikuta inatumia raslimali zake kutetea muungano badala ya kuwatumikia raia wake. History has never been wrong; kama Muungano huu ni mbaya au ni mzuri basi historia itaonyesha hivyo huko mbeleni. Tuliwahi kuwa na Jumuia ya Afrika Mashariki huko nyuma, wakatokea watu wa aina hii hii ya leo na kuiua jumuia hiyo, halafu eti leo ndio wanakurupuka kwa nguvu sana kuitaka jumuia hiyo hiyo irudi tena. Nimekuwa nafuatlia kwa makini sana jinsi Tanzania inavyojiingiza katika jumuia hiyo kutokana na sababu za kihistoria, na nadhani iwapo mwenyezi Mungu atanipa uhai wa kutosha, nitapenda nione pia nchi hizi zinaendelaje baada ya kuvunja muungano wao.
 
Where did you get the assertion that "ni lazima ifanyike kwa maandishi na siyo kwa kauli"? Sheria gani ya Kimataifa inayosema hivyo or this is your construction based on a false premise - kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni ya kimaandishi vivyo hivyo...


How did you get this conclusion kuwa ni 'lazima' iwe?

This borders the pedantic (not as a compliment), but could be argued to be central, in context.For it could nullify the need for written ratification on the Zanzibar part, which, at least in the letter of the law, has been argued to be a pitfall of the Union. Of course I am not sure we even have recordings of any formal oral agreement, which introduces quite another animal. Let alone the consideration of the difference between a plain vanilla bilateral treaty compared to a union of two countries, whose jurisprudence could still require a higher level of fidelity.

Furthermore, the spirit of the law calls not only for a ratification, but ample justification and adequate involvement of the populations. Hence my call for a national referendum.

Sir Gerald Fitzmaurice posed a similar question regarding the lack of some aspects of formalism in the Vienna Convention on the Law of Treaties of 1969 (which Tanzania is party to, signatory and ratifier ) as demonstrated by the various then pre-existing notes verbales. See the matter of the Norwegian Minister of Foreign Affairs, Mr. Ihlen, made on behalf of his government "in response to a request by the diplomatic representative of a foreign power" on a matter regarding The Legal Statuses of Eastern Greenland". The Permanent Court of International Justice considered the "Ihlem Declaration" binding upon Norway without expressly pronouncing on th legal status of the declaration, it is considered by scholars as a case of bilateral agreement.

The ground here is murky indeed. More updated input and cases of precedents are needed.

See The Vienna Conventions on the Law of Treaties: A Commentary - Olivier Corten, Pierre Klein - Google Books

The Vienna Convention on The Law of Treaties, pp 39 Corten, Oliver. Klein, Pierre
 
Pasco I hope umemaliza hilo darasa ulilotutisha nalo. Kama umemaliza basi umeshindwa kabisa kuonesha kuwa BLM halikuridhia muungano. Inaonekana umetafsriri kwa Kiswahili maandishi ya watu wengine ambayo umeshindwa kuyawekea shaka ya kisomi. Umeyakubalikuwa ni kwel bila kuyahoji na kutuletea tuyaamini kuwa ni kweli.
Mzee Mwanakijiji, ni kweli nimemaliza on ratification. Namalizia zilizobakia kwa para moja moja ndipo nianze kujibu maswali.

Ni kweli nimefanya tafsiri tupu maandishi ya wengine pasi kuyatilia shaka na japo mashuhuda wa Zanzibar wamebaki wawili, sijapanga hata kuwatafuta kwa sababu sitegemei ukweli wowote tofauti na huu iliokwisha andikwa!.

Nasubiria somo la ratification kwa kauli tuu bila process wala maandishi!.

Pasco
 
4. Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964.

Asante Pasco inatosha, zaidi ya hapo ni kutaka kujikuna pale mkono wako usikofika...:confused2:
 
Mzee Mwanakijijib, ni kweli nimemaliza on ratification. Namalizia zilizobakia kwa para moja moja ndipo nianze kujibu maswali.

Ni kweli nimefanya tafsiri tupu maandishi ya wengine pasi kuyatilia shaka na japo mashuhuda wa Zanzibar wamebaki wawili, sijapanga hata kuwatafuta kwa sababu sitegemei ukweli wowote tofauti na huu iliokwisha andikwa!.

Nasubiria somo la ratification kwa kauli tuu bila process wala maandishi!.

Pasco

Hili la ratification ninawaachia nyie la kwangu litakuwa kubea kidogo.
 
Pasco, kumbuka kuwa in situations where a new parliament has not been organized, the will of the government is implemented by decrees of the president. Hivyo baada ya mapinduzi na katiba ikiwa imesimamishwa, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali was irrelevant kama zilivyokuwa bunge, mahakama na mihimili mingine ya dola. Lazima ukumbuke kuwa serikali iliyokuwa imeundwa na Shamte chini ya Sultani, ilikoma tokea usiku wa tarehe 12 Januari, 1964 sasa huyo Dourado angefanya kazi chini ya katiba ipi?
 
Last edited by a moderator:
Asante Pasco inatosha, zaidi ya hapo ni kutaka kujikuna pale mkono wako usikofika...:confused2:
Bantugbro, nakuunga mkono, wewe soma na meza yale tuu yanayomezeka kwako, yake usoweza kumeza yateme tuu na kuyahesabu kuwa ni sehemu ya Alfu Lela U-Lela za muungano!.

Wazanzibar wendawazimu waliochoma makanisa wanasahau jemedari wao mkuu wa mapinduzi yale ni Mkristu John Okello akisaidiwa na Eddington Kisasi!. Dhambi ya ukosefu wa fadhila itawatafuna mpaka basi!.
 
Tunapokuwa tunajadiliana uhalali wa Muungani tusiesahu kuwa pia tunakuwa tunafungulia a can of worms.

(a) Serikali halali ya Zanzibar mwaka 1964 huo wa muungano haikuwa ile ya Baraza la Mapinduzi la akina Karume na rafiki zake kwa vike baraza lile halikuchaguliwa na wananchi bali walijichukulia madaraka kwa nguvu. Mapinduzi yale hayakupigiwa kura ya maoni na wananchi wa Zanzibar, yalitokea ndani ya siku mia moja tu tangu serikali halali iliyokuwa imechaguliwa na wananchi ikae madarakani. Mwaka 2007, niliweka article moja pamoja video fulani hapa JF iliyokuwa inayonyesha kuwa mapinduzi yale yalikuwa ni ya kinyama na haramu.

(b) Baada ya mapinduzi hayo kufanyika, katika kipindi ambacho muungano ulifanyika, Zanzibar haikuwa na katiba na wala hakukuwa na utaratibu wa kisheria kuhusu nani mwenye madaraka yapi; baraza la mapinduzi na Karume ndio waliokuwa mwanzo na mwisho katika serikali hiyo ya mapinduzi ambapo uamuzi wa Karume ulikuwa ni final. Mwenye nakala ya Katiba ya Zanzibar yenye kuonyesha mipaka ya madaraka ya Karume katika kipindi hicgo aitoe hapa tuone ni wapi Karume alipokiuka madaraka yake.


Pamoja na kuwa na uhakika kuwa katika mazingira tuliyopatia Muungano huo kila kitu kilikuwa ni halali, nimechoshwa sana na manung'uniko ya muungano huo kiasi kuwa ninataka tuuvunje sasa hivi ili tuhamishie nguvu zetu katika mambo ya maana zaidi. wakati mwingine huwa inainudhi sana kuwa wazenj wote tuliosoma nao UDSM waliporudi kwao wakateuliwa mara moja kwenye nyadhifa kubwa sana ndani ya serikali ya muungano kutokana na uchache wao wakati sisi watanganyika hatukujulikana popote kwenye system hiyo pamoja na kuwa baadhi yetu tulikuwa tunawapiga tutorial baadhi ya wazenj hao walioibuka kuwa na madaraka makubwa juu yetu.

Watu wengi tuna tabia ya kualaumu wengine kwa mapungufu yetu, kwa hiyo nadhani kuwa kuondoka kwa muungano huu kutasaidia sana kuondoa kisingizio kimojawapo cha mapungufu yetu.
 
Pasco, kumbuka kuwa in situations where a new parliament has not been organized, the will of the government is implemented by decrees of the president. Hivyo baada ya mapinduzi na katiba ikiwa imesimamishwa, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali was irrelevant kama zilivyokuwa bunge, mahakama na mihimili mingine ya dola. Lazima ukumbuke kuwa serikali iliyokuwa imeundwa na Shamte chini ya Sultani, ilikoma tokea usiku wa tarehe 12 Januari, 1964 sasa huyo Dourado angefanya kazi chini ya katiba ipi?
Mkuu Mag3, jurisdiction ni terirorial!, Hakuna ubishi baada ya mapinduzi, Karume ndio alikuwa kila kitu, ila jurisdiction yake kwenye decrees inaishia Zanzibar kwenye teritorial iliyokuwa Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar!.

Chochote alichokifanya alifanya kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kiliandikwa kama decree, kwa vile yeye ndiye alikuwa kila kitu, ule mkataba wa muungano umesainiwa kwake Zanzibar ile tarehe 22 April 1964 na ulibaki kwake!. Kwanini asiitishe kikao cha BLM na kuwaamuru wapitishe ratification ili ile siku ya muungano angekuja na ratified contract na decree yake hata kama angeipitisha yeye mwenyewe tuu lakini ratification ingetoka Zanzibar accompanied by a decree na ingetangazwa kwenye Zanzibar Gazette!.

Kitendo cha kuibukia bara na ratification iliyoandaliwa bara bila any reference ya BLM na sheria hiyo ikatungwa bara na kusainiwa bara na kurekodiwa na GN ya bara, was not proper kwa sababu kabla ya muungano uwezo wa kisheria wa Karume kuhusiana na sheria za ndani, uliishia kwenye mipaka ya Zanzibar!. Hivyo ile ratification aliyoifanya Dar ilikosa uhalali wa kisheria kule Zanzibar na hili lilikuwa ni jambo dogo tuu la kulihakalisha kisheria kwa Zanzibar kurekodi kwenye miniti za BLM, kulitungia Decree na kurekodi kwenye Zanzibar Gazette!.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, bado nasubiri makaratasi to substantiate your claim(s), kuanzia kule kwa 'puppets' hadi huku unakosema kuwa Zanzibar haikuridhia. So far, naona kama unaungaunga story sana and I expected a very rich essay yenye viambatinishi. Sijui hata unapeleka wapi huu mjadala kwa sasa? Do you still have something in store for JF au ndio umemaliza?
 
Pasco, bado nasubiri makaratasi to substantiate your claim(s), kuanzia kule kwa 'puppets' hadi huku unakosema kuwa Zanzibar haikuridhia. So far, naona kama unaungaunga story sana and I expected a very rich essay yenye viambatinishi. Sijui hata unapeleka wapi huu mjadala kwa sasa? Do you still have something in store for JF au ndio umemaliza?
Mkuu FJM, unasubiri viambatishi as if ndio nafanya submition kwani hapa ni mahakamani?, au niweke reference kama academic presentation?.

Kwa ratification ndio nimemaliza, just pick whatever makes sense to you, points ambazo they don't make sense, just regard them as Alfu Lela U-Lela za siasa za Zanzibar!. If nothing makes sense at all just moves on!.
 
Wanabodi,

Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.
Natanguliza shukrani.

Pasco.


Hahahaha! ......mkuu Pasco umenifurahisha sana!
 

Attachments

  • 403153_238721636199021_100001835595463_575666_480209508_n.jpg
    403153_238721636199021_100001835595463_575666_480209508_n.jpg
    45.4 KB · Views: 66
pasco go and advise the zanzibari all your findings, God knows the end of it all.


To me all those things are irelevant what people need to say is that we are no longer confortable with this Muungano so we have decided to detach ourselves from it.


Suppose there is a referendum and 51% zanzibari says we dont want Muungano and 49% says they need it how are you going to treat the minority, are going to ingnore them?.


Kuubuka Mwalimu Nyerere alisema zambi yakujitenga hayitakufa bali yitaendelea. To me I can say he prophesized, there is every possibility that Muungano shake maybe even break, the milk and honey people hope for will end up a nightmare.

Best of lucky

hivi kuna hasara gani ya kutengana iwapo kila mmoja ataendelea vizuri zaidi ya kuwa kwenye muungano??

what do we learn from russia and from smaller countries of 1M or 500,000 people??

is there any lesson from rwanda kulinagnisha na kongo?? if congo ingetoa nchi nne, hali bado ingekua ile??

and who brought the borders??
 
Pasco, bado nasubiri makaratasi to substantiate your claim(s), kuanzia kule kwa 'puppets' hadi huku unakosema kuwa Zanzibar haikuridhia. So far, naona kama unaungaunga story sana and I expected a very rich essay yenye viambatinishi. Sijui hata unapeleka wapi huu mjadala kwa sasa? Do you still have something in store for JF au ndio umemaliza?
i have never loved pasco's posts more than in this thread

some of the things you want to see is just like trying to put pasco kwenye ile other side of the scenario awe mmiliki wa nyara.... thats not the way
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tuonyeshe record yeyote ya Baraza la Mapinduzi (ki memo, barua, minutes za kikao , tamko, shairi, decree (sheria), n.k.) inayosema "Sisi Baraza la Mapinduzi tumeridhia Muungano."

Bahati mbaya wajumbe wengi wa baraza hilo hawakusoma
 
Back
Top Bottom