Je, wajua kuwa watanzania wanavipenda vyombo vyao vya ulinzi na usalama ila hukatishwa tamaa?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,116
33,089
Sio siri Watanzania wengi sana huwa wanavipenda sana na kuvisifu vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama,Hususan JW,TISS,FFU na hata TP.
Mara nyingi utawakuta vijana wakiwa vijiweni wakiyasifu majeshi yetu kwa kazi nzuri ndani na nje nchi baada ya kufanya kazi nzuri huko.JW walifnya vizuri sana Liberia,Comoro,Msumbiji n.k.
TISS hufanya kazi nzuri sana mahala pote alipo Mtanzania ndani na nje,FFU na TP mara nyingi kuzuia ghasia na kupambana na majambazi hufanya kazi nzuri na njema sana.
Wananchi wengi huwaita majina ya kuwasifia kama "wazee wa kazi, wanaume,wagumu,wataalam na majina mengi ya kuwasifia.
Wananchi hawa huvunjika moyo pale tu vyombo hivi vinaposhindwa kukata kiu zao ,na wannchi kujiona kama wametengwa na watu wanaowategemea.
Raia wa nchi hii wanapowazungumzia Walinzi na Wanausalama hawa, huwazungumzia kwa sifa na uzuri,lakini hukatishwa tamaa kwa mambo mengi ambayo huwa hayajadiliki hadharani.
Tujadili,bila matusi.
 
Polisi hujisifu namna wanavyo wabambika makosa raia hao na kuwakamua pesa kisawasawa. Na wakati mwingine hujisifu jinsi wanavyo wabambikia makosa ambayo wala hawajayafanya.
 
Polisi hujisifu namna wanavyo wabambika makosa raia hao na kuwakamua pesa kisawasawa. Na wakati mwingine hujisifu jinsi wanavyo wabambikia makosa ambayo wala hawajayafanya.
Ni kweli hawa ndio taasisi ya dola inayolaumiwa zaidi,ila wakiamua hutoa dozi murua kwa majambazi.
 
Kuna polisi mmoja aliwahi kuniambia ; kwa jinsi watu wanavyobambikiziwa kesi zisizo zao na pesa wanazopigwa raia juu ya makosa yao ya kweli na yasiyo kweli. Kama raia hawa wanamlilia Mungu na anasikia vilio vyao basi polisi tuna makosa mengi mno mbele ya Mungu.

Mwisho alinambia kuna wakati anatamani asitembee na sare za polisi.
 
Me mwenyewe navikubali sana vyombo hivi,basi tu hata mashine Hauko 100%.. Lazima na wao watakua na mapungufu Yao.
 
sijui mkuu ulifanya vipi utafiti wako huu kuhusu kupendwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama;kwanza hivi vyombo vipo kisheria kwa ajili yetu kwa hiyo havifanyi fadhila kwetu ila ni lazima vitekeleze wajibu wake tena kisheria;binafsi jibu ni NO hivi vyombo haviko kwa ajili yetu ila kwa wateule wachache;hapa hapa kwenye SADCC yetu(Namibia ,Botswana na kidogo SA) vyombo vyao vya usalama na ulinzi vipo karibu mno na umma ni kitu cha kawaida kabisa kuona wanausalaama wao wakikusaidia hata kubadilisha tairi lililopata pacha,ukiharibikiwa na gari wanakuwa nawe hadi utakapopata msaada n.k;kwetu hata ukiharibikiwa na gari pale usawa wa kambi ya lugalo utaanza kujiharishia!!
 
Aisee siwapendi Polisi wa Tz mpaka basi ni watu wa hovyo sana tatizo lako ni mradi kwao sijui wapoje?
 
Hapo wanaostahili sifa ni jw tu polisi ni waovu wakuu hao usalama ndio wanaoteka watu kisa cccm hovyo kabisa
 
Mmmmh, kuhusu JWTZ hao sina la kuzungumza ila Polisi wale wanaovaa nguo za kaki Mungu nisamehe ila hawa si watu
 
Aisee siwapendi Polisi wa Tz mpaka basi ni watu wa hovyo sana tatizo lako ni mradi kwao sijui wapoje?
Siku zote huwez kumpenda jirani yako.
Lazima uwachukie polisi sababu ndo wako karibu na raia.
JWTZ wako zao mipakani ndo mana unawapenda.
 
Siku zote huwez kumpenda jirani yako.
Lazima uwachukie polisi sababu ndo wako karibu na raia.
JWTZ wako zao mipakani ndo mana unawapenda.
Sio defence hiyo sasa ujirani gani wa kubambikiana kesi nyie mapolisi mjitathimini sana mnaumiza sana raia kwa urafi wenu wa hela za masikini.MAPOLISI WA TZ HAWAPO JIRANI NA RAIA WAPO JIRANI NA HELA ZA RAIA
 
Back
Top Bottom