Je, wajua kuwa wanyama waweza kukupa taarifa kama kuna janga kubwa sana linakuja?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Kila alichokiumba Mwenyezi Mungu kina kazi yake maalumu ambayo binadamu mara ingine kuijua yaweza chukua karne.

Wanyama huwa wana uwezo wa kujua janga kubwa sana linapotaka kuja. Kwa mfano, kondoo kama kuna radi inataka kupiga chini, huwehuka na kuanza kukimbia huku na kule na kugonga miti kwa kichwa chake akikupa taarifa kuwa radi yaweza shuka eneo hilo chukua tahadhari upesi kama ulikaa chini ya mti mvua ikinyesha unatakiwa utoke haraka ukae sehemu ya wazi kujinusuru na radi ambayo hupenda kupiga kwenye miti.

Kukiweko joka kubwa karibu au mwanga Mchawi mbwa huwa wanabadilika tabia na kuanza kutoa milio fulani hivi isiyoeleweka kutoa taarifa kuwa kuna kitu cha kutisha tishio kiko karibu.

Mengine yasikilize kwenye hii video uone maajabu ya wanyama kupata taarifa za majanga makubwa mapema na kuziwakilisha kwa binadamu lakini kutokana na binadamu kuwa na uelewa mdogo taarifa hizo ambazo binadamu angezingatia maafa yangeweza kuepukika zinashindwa kumsaidia binadamu matokeo yake mamilioni ya watu kuangamia pasipo sababu.

 
NJIWA
Unajua kama njiwa ndio mfugo ambao hautaki kufugwa na mlevi, au watu wanaogombana sana mke na mume fuatilia kuhusu njiwa utayajua usiyoyajua.
msiba unakaribia nyumbani njiwa hawatoki kutwa mzima wanaweka kimya ata kelele hawatoi iyo siku na vikundi kwa uzuni hata kula yao haiyeleweki na mtu akishafariki tayari wakaja watu wengii nyumbani wakaleta fujo na kelele wanaeza kuhama wote na wasirudi tena kuepusha kuhama inataikiwa uwaambie kuwa leo kuna wageni wanakuja kuzika njiwa asubuhi sana wataondoka jioni watarudi.
 
Kuku wanaoishi karibu na makaburi husikia sauti ya marehemu akiwaita wakati mnaondoka baada ya kumzika. Inasemekana yale maji ya kibirika yakifika kwenye sikio la marehemu, marehemu huzinduka na kuanza kupokea adhabu za kaburi. Ukiwaangalia kuku wakati huo utaona wameinua shingo zao wanasikiliza
 
Kuku wanaoishi karibu na makaburi husikia sauti ya marehemu akiwaita wakati mnaondoka baada ya kumzika. Inasemekana yale maji ya kibirika yakifika kwenye sikio la marehemu, marehemu huzinduka na kuanza kupokea adhabu za kaburi. Ukiwaangalia kuku wakati huo utaona wameinua shingo zao wanasikiliza
nadharia tu hizo ..
 
Back
Top Bottom