Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,546
2,000
Wanabodi,

Wakati tukijiandaa rasmi kuingia kwenye serikali 3, tutake tusitake, lazima tutarudi nyuma kuungazia muungano wetu, na kabla hatujaingia katika serikali tatu, lazima kwanza tuwe na Mkataba rasmi wa Muungano, ndipo zifuate hizo serikali 3. Hiki kilichopo, kinachoitwa Mkataba wa Muungano, "Articles of Union", kiukweli, nasema bila kumung'unya maneno, sio Mkataba wa Muungano (contract), bali ni Makubaliano ya Muungano (Agreement) tuu.

Kuna tofauti kubwa kati ya Mkataba na Makubaliano, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Yaani "Every contract is agreement, but not every agreement is a contract!".
Kama ilivyo kwa uraia wa Tanzania, kila Mzanzibari ni Mtanzania lakini sio kila Mtanzania ni Mzanzibari.

Ili makubaliano yaitwe mkataba, ni lazima makubaliano hayo yawe na sifa kuu nne za mkataba. Kwa bahati mbaya sana, Makubaliano ya Muungano wetu, yamekosa baadhi ya sifa hizo muhimu.

Ambatana nami katika kuyachambua haya makubaliano ya muungano kwa nini ni makubaliano tuu na sio mkataba, na ni kwa nini lazima kwanza tuwe na mkataba wa muungano ndipo tuweze kwenda kwenye serikali tatu.

Kwa wale wenye nafasi, mnaweza kuanza kuyapitia haya makubaliano ya muungano, kisha tutapelekana kidogo kidogo kwa lugha rahisi kwa kila mtu kulielewa hili.

NB. Mambo mengine, yako kisheria zaidi, ila bado I stand to be corrected na "the learned brothers and sisters"

Kwa wale ambao sio wanasheria, unaweza pia kuwa mwanasheria bila kusomea chuo chochote cha sheria, bali kwa kujisomea tuu mambo ya kisheria kama hapa.
kwa kuanzia jisomee mwenyewe
  1. What is a contract?
  2. What is an agreement?
  3. What are the differences between Contacts and Agreements?
  4. Why every contract is an agreement but not all agreements are contracts
  5. Baada ya kusoma hayo hapo juu, tunaweza kwenda pamoja kujua kwa nini makubaliano ya muungano sio mkataba!
NB. Japo makubaliano haya ya muungano sio mkataba, na japo hayakuridhiwa rasmi na upande wa Zanzibar (ratification), bado ni makubaliano halali, hivyo muungano wetu ni halali na nchi yetu Tanzania ni nchi halali (de facto) ila sio halali kisheria (de jure).

Happy New Year!
Pasco.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,586
2,000
Pasco utaandika maandishi mengi sana, na kwa kufanya hivyo walio na uwezo mdogo kusoma katikati ya mistari utakuwa umewapoteza kabisaaaa, watabaki wanakushangaa kama si kushangaa uandishi wako.

Mkataba ni makubaliano ya kutekeleza MAKUBALIANO.
HUO NDIO MKATABA usisubiri iwe imeandikwa kiyunani ndio ukubali.
 
Maishamapya

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,279
1,500
Wanabodi,

Kuna tofauti kubwa kati ya Mkataba na Makubaliano, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Yaani "Every agreement is a contract, but not every agreement is a contract!".

Ili makubaliano yaitwe mkataba, ni lazima makubaliano hayo yawe na sifa kuu nne za mkataba. Kwa bahati mbaya sana, Makubaliano ya Muungano wetu, yamekosa baadhi ya sifa hizo muhimu.

Ambatana nami katika kuyachambua haya makubaliano ya muungano kwa nini ni makubaliano tuu na sio mkataba, na niu kwa nini lazima kwanza tuwe na mkataba wa muungano ndipo tuweze kwenda kwenye serikali tatu

Pasco.

Kabla sijaandmaa nawe hebu nisaidie hapo kwenye BOLD
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,546
2,000
Pasco utaandika maandishi mengi sana, na kwa kufanya hivyo walio na uwezo mdogo kusoma katikati ya mistari utakuwa umewapoteza kabisaaaa, watabaki wanakushangaa kama si kushangaa uandishi wako.

Mkataba ni makubaliano ya kutekeleza MAKUBALIANO.
HUO NDIO MKATABA usisubiri iwe imeandikwa kiyunani ndio ukubali.
Yes kuna makubaliano mengi sana watu wanayaita ni mikataba, kumbe kiukweli sio mikataba bali ni makubaliano tuu, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Ili makubaliano yawe mkataba, lazima yakidhi vigezo fulani, makubaliano ya muungano, hayakidhi na ndio maana hati zile zimefichwa, na kule umoja wa mataifa imeandikwa zimepelekwa ila kiukweli hazikupelekwa na hazipo!.

Pasco
 
kyanaKyoMuhaya

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,953
2,000
Wanabodi,

Wakati tukijiandaa rasmi kuingia kwenye serikali 3, tutake tusitake, lazima tutarudi nyuma kuungazia muungano wetu, na kabla hatujaingia katika serikali tatu, lazima kwanza tuwe na Mkataba rasmi wa Muungano, ndipo zifuate hizo serikali 3. Hiki kilichopo, kinaichwa Mkataba wa Muungano, "Articles of Union", kiukweli, nasema bila kumung'unya maneno, sio Mkataba wa Muungano (contract), bali ni Makubaliano ya Muungano (Agreement) tuu.

Kuna tofauti kubwa kati ya Mkataba na Makubaliano, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Yaani "Every contract is agreement, but not every agreement is a contract!".

Ili makubaliano yaitwe mkataba, ni lazima makubaliano hayo yawe na sifa kuu nne za mkataba. Kwa bahati mbaya sana, Makubaliano ya Muungano wetu, yamekosa baadhi ya sifa hizo muhimu.

Ambatana nami katika kuyachambua haya makubaliano ya muungano kwa nini ni makubaliano tuu na sio mkataba, na niu kwa nini lazima kwanza tuwe na mkataba wa muungano ndipo tuweze kwenda kwenye serikali tatu.

Kwa wale wenye nafasi, mnaweza kuanza kuyapitia haya makubaliano ya muungano, kisha tutapelekana kidogo kidogo kwa lugha rahisi kwa kila mtu kulielewa hili.

NB. Mambo mengine, yako kisheria zaidi, ila bado I stand to be corrected na "the learned brothers and sisters"

Kwa wale ambao sio wanasheria, unaweza pia kuwa mwanasheria bila kusomea chuo chochote
kwa kuanzia jisemee mwenyewe
  1. What is a contract?
  2. What is an agreement?
  3. What are the differences between Contacts and Agreements?
  4. Why every contact is an agreement but not all agreements are not contacts
  5. Baada ya kusoma hayo hapo juu, tunaweza kwenda pamoja kujua kwa nini makubaliano ya muungano sio mkataba!
NB. Japo makubaliano haya ya muungano sio mkataba, na japo hayakuridhiwa rasmi Zanzibar (ratification), bado ni makubaliano halali, hivyo muungano wetu ni halali na nchi yatu Tanzania ni nchi halali (de facto) ila sio halali kisheria (de jure).

Karibu uandamane nami.

Pasco.

We! Pasco Muungano unautakia nini? kwani waliotakiwa kuridhia wengi wao mbona ni marehemu na ambao walikuwa "accountable by then"?..!?!.,???.

Last edited by a moderator:

Kashishi

JF-Expert Member
Apr 11, 2010
1,126
2,000
Pasco nimekusoma kwa umakini hoja yako. Lakini naona kuwa unajichanganya mwenyewe na hao unaotaka waambatane na wewe pia unawachanganya hususani wale wasio na uelewa mpana katika masuala ya ulingo wa sheria;

Look my friend, "An Agreement is Contract" period! Na moja ya sifa za mkataba (Contract) ili uitwe mkabata "Ni lazima;
(a) Uwe Unaweza kutekelezeka (implementation)
(b) Uwe na nguvu zenye msukumo wa kisheria (law enforced agreement)

Na ili uweze kupata kitu kinachoweza kuitwa Mkataba (Contract), basi ni lazima kwanza kuwepo na list ya mambo ya kutekelezwa makubaliano, yaani (list of Agreement/s)

Hivyo mantiki yako ya kuwa "Not every Agreement is contract" DO NOT exist (Haipo)! Kwa maneno mengine if an agreement/s DO NOT FIT to be 'termed' under so called Contract, then; is NOT A CONTRACT. Period! You could just simply name it something el

Kwa lugha nyingine nyepesi pengine inaweza ku-apply pale tu ambapo labda kuwa mkataba (contract) wenyewe ni wa kuuziana bangi au mihadarati...kwa maana nyingine ni biashara ambayo haina UHALALI. Biashara isiyo tekekeleka kisheria. Na wala makubaliano (Agreements) yake hayawezi kubeba heshima ya kutambulika kisheria. Na wala kuweza kuwa na nguvu za msukumo wa kisheria (law enforcing agreement).

Lakini nikupe mfano mwingine; pale inapotekea umepangisha mtu chumba katika nyumba yako kwa makubaliano ya kulipwa mathalani Tshs.60,000.00 kila tarehe moja ya mwezi, kwa muda wa mkataba wa miaka miwili (including umeme na maji). Hayo ni makubaliano yenye uhalali na yenye kuweza kupata tiba, utetezi na msukumo wa kisheria endapo mkataba ama makubaliano (agreements) hayo yatakiukwa na upande mmoja wapo kati ya pande mbili zilizokuwa kwenye mkataba (contract).

Mwisho napenda kuhitimisha hoja / mada uliyoileta kwa kwa kuweka bayana pasipo shaka kuwa kilichopo Tanzania ni 'Mkataba halali wa Muungano' na si habari ya ati kuwa ni 'Makubaliano ya Muungano' tu. Kumbuka kwamba bila ya makubaliano means hakuna Mkataba (No Agreements means no Contract). Lakini si unaona mtiririko wa list ya Makubaliano (Agreements) yapo means Mkataba (Contract exist). Na yote ni mambo yanayotekelezeka kisheria. Na yote yanaweza kupata tiba na nguvu zenye msukumo wa kisheria.

Muulize Maalim Seif Sharif Hamadi kipindi fulani miaka ya nyuma alishapata kujitapa kuwa siku za mkataba feki wa Muungano zinahesabika kwani wamesha retains lawyers (Wanasheria) wazito na magwiji huko katika miji ya London na New York. Alidai wako tayari kusaidia ku challenge huo mkataba katika mahakama za kimataifa. Na waliiandikia hata ofisi za UN New York kushawishi wasiendelee kutambua hati hiyo ya Muungano.
Ni kitambo sijawasikia tena hata kutaja kuwa hiyo misheni yao iliishia wapi. Sasa hapo Pasco jiulize ndugu yangu na pia na ku challenge kuwa iwapo akina Maalim Seif walisha retain Wanasheria mashuhuri JE? unafikiri wao kiliwashinda nini? Je? hawakuona wepesi wa kutokea shimo hili (kuvunja muungano kiana na ki tekinikali) kuwa kilichomo humo ni makubaliano (agreement) tu na si MKATABA (Contract) kwa namna unayotuaminisha na kutusomesha hapa leo?

Mwisho, pengine wengi wetu hujiuliza kuwa Je? mkataba huo unaweza kutokea kuwa 'Challenge at the court of law" jibu ni jepesi nalo ni YES. Na nafikiri Zanzibar kuna jamaa kadhaa wamefungua kesi kwenye Mahakama ya Zanzibar tayari....lakini wacha niishie hapa pasipo kuchujua wala kupoteze hoja/mada.
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
2,000
Pasco rafiki yangu, Nimefuatilia sana article zako kuhusu hili. Tatizo ulilo nalo ndilo walilo nalo watanzani wengi ikibidi zaidi ya 95%.

Tatizo tulilojitakia sisi watanzania ni majina kuabadilibadili. Ukweli ni kwamba neno mkataba kwa kiswahili lina maana pana sana ukilitafsiri kwa kiingereza.

Kwa mfano, haya yote yana maana ya neno "mkataba": Contract, agreement, pact, memorandum of understandig, treaty nk. MKataba unapokuwa ni nchin na nchi, unaitwa TREATY.

Sasa sijui kwa nini huu wetu tulijikita sana kuuita ARTICLES OF UNION badala ya kuuita TREATY OF UNION OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR.

Kukosekana kwa neno TREATY ndiko kunakowafanya wazanzibari wakurupuke na kusema kwamba wanataka muungano wa mkataba kana kwamba ule wa 1964 haukuwa mkataba(Treaty)!!! Tuna watu wa akili za ajabu sana kule Unguja!!!!

Wenzetu Scotland na England waliungana 1707 na jina la mkataba wao kama wetu waliuita TREATY OF UNION na TREATY hiyo ikalipa taifa jipya jina GREATY BRITAIN.

Ukiiangalia ile Treaty of Union yao na yetu, hakuna tofauti sana isipokuwa wao walikuwa tayari wana zaidi ya miaka 100 wakitawaliwa na mtu mmoja tangu King James I alipozitawala kwa pamoja Scotland na England kama leo jinsi Elizabeth II alivyo kwa UK, Canada, Australia, New Zerland nk.

Tatizo lao halikuwa kama letu kwani sisi Rais mmoja angepoteza urais na hilo ndilo moja ya tatizo linalotusumua hadi leo.
 
Ben Mugashe

JF-Expert Member
Oct 9, 2008
998
1,000

Nina kigugumizi sana na hiz ID jinsi gani zinavyolandama kuanzia miandiko, mawazo, fikra na uelewa..labda nisaidie tu kaka Pasco..huyu mpwa wetu Nikupateje alipitia mafunzo kama yako?
 
crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
Pasco
Unaikumbuka ile picha maarufu ya karume na nyerere wakisaini ?
Inatajwa kuwa walikua wakisaini makubaliano ya kuungana . Hii ilikua zanzibar tarehe 22/04/1964
Na jee unaikumbuka ile picha nyengine maarufu karume na nyerere wote wakiwa wamepiga suti safi sana wakibadilisha kinacho semwa hati ya muungano.

Sasa cha kushangaza hizi hati zote 2 iile ya mwanzo iliyosainiwa zanzibat na ya pili walio saini dar es salaam na kubadilishana hazionekani. Yaani hatuna hati original walizo saini viongozi hawa hivyo muungano kisheria haupo . Huwezi kuwa na mkataba wa kisheria lakini hakuna uthibisho wa saini na official goverments seals.

Inawezekana makubaliano yalikuwa kwa masharti maalum ndio maana utaona wakati wa karume zanzibar ilikua inafanya mambo yake kivyake bila kufata mapenzi ya nyerere.
Mfano znz walianzisha TV lakini huku nyerere alikataa
Siasa ya ujamaa znz ilikua nadharria tu lakini watu wakiendelea kumiliki mali

Nyerere aliwahi kusema muungano huu ni tabu kueleweka na ni yeye na karume ndio wanaulewa.
Kuna fununu za hapa na pale kwamba nyerere alilazimishwa kuungana na znz ma CIA hivo hakua na nia ya dhati ya kuwa ndani ya muungano hivo waliwekeana mkataba wa miaka kumi na baadae waulizwe wananchi kama wanataka kuendelea ama la.
Na karume alikubali kuungana ili kujiimarisha ili baada ya miaka 10 atakuwa na uwezo wa kiulinzi pekee yake.
Wakati wa karume waliunda Navy iliuokua na zana za kisasa kabisa na haihusiani na mungano
Pia wanajeshi wa znz walikua wapo kwao yu hakuna mambo ya kuhamishiwa bara.

Karume alishi only kwa miaka 8 ya muungano hivyo walo kubaliana yakapotea na ndio ikaanza mbinu ya kuimeza znz .

Muhimu cha kujiuliza zipo wapi hati za mkataba zenye saini za Karme na nyerer
?

Kwanini zimepotezwa?

Labda kabla ya kuongeza na kupunguza mambo ya muungano kama rasimu mpya inavosema basi hati hizi zipatikane otherwise muungano huu si halili kisheria na akitokea mjuaji kuzipandisha serikali mahakama ya kimataifa muungano unaweza kupindiliwa
 
Mkuu wewe ni wa ajabu kweli. Huamini picha na makabidhiano ya mkataba lakini unaamini fununu kwamba kuna mkataba mwingine waliosaini wa kukaa miaka kumi halafu uitishwe uchaguzi wananchi wachague kuendelea au kuusitisha muungano!

Wakati Karume alitamka wazi kuwa hakutakuwa na uchaguzi wowote Zanzibar ndani ya miaka 50. Karume alikuwa sahihi maana uchaguzi wake alioona unafaa ni hiyo referenduma tunayopiga mwaka huu kuchagua katiba mpya maana ni miaka 50 kamili ya Karume tangu Mapinduzi.

Cc: Pasco
 
mwanzo wa moto ni moshi....fununu unaweza kuziamini kwa kuangalia mazingira yenyewe...Karume hakufa aliuliwa....na wanajeshi . na katika watu walo husika na kutakiwa kushtakiwa ni SALIM,Babu, Kanal Ali Mahfoudh hawa wote walikingwa na Nyerere, Ali MAHFOUDH AKapewa cheo kikubwa Msumbiji kwa ushauri wa nyerere!!! jeee hiii ni zawadi kwake kwa job well done ?
hizo ni fununu lakin zina ukweli wa wazi kwa kwa vile haileweki kisa halisi cha kupotea mikataba hii yenye saini na seal za serikali...
jee copy ya upande wa zanzibar ilipotea lini ? baada ya karume kuuliwa.
karume mdogo Amani yeye alijisemea hajawahi kuiona, mwanasheria wa znz naye akasema haipo na mwanasheria wa znz nae alithibitisha haipo imeibwa
suala zima ni lime zungukwa na conspiracy theory kwa sababu sio halali
 
sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
939
500

tumeshaungana sasa haijalishi historia yetu ya kuungana ipoje, ni kama ukijua kuwa ulizaliwa baada ya baba ako kumbaka mama yako, tusonge mbele tuweke makubaliano mapya katika katiba mpya tuimarishe muungano wetu unaoendana na kizazi chetu, tusiendelee kuwa watumwa wa historia
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,443
2,000
Mkuu Pasco hivi na wewe unapataga client wa kuwatetea Mahakaman.
Nadhan watakuwa wote wameshindwa kesi na pengine kuswekwa Lupango kabisa
 
Last edited by a moderator:

Bobwe

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,239
0
Yes kuna makubaliano mengi sana watu wanayaita ni mikataba, kumbe kiukweli sio mikataba bali ni makubaliano tuu, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Ili makubaliano yawe mkataba, lazima yakidhi vigezo fulani, makubaliano ya muungano, hayakidhi na ndio maana hati zile zimefichwa, na kule umoja wa mataifa imeandikwa zimepelekwa ila kiukweli hazikupelekwa na hazipo!.

Pasco

Kama hazipo,huo uhalali wa muungano upo wp?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom