mukaruka mzee
JF-Expert Member
- Jan 22, 2020
- 970
- 483
Hamu na nia ya maendeleo ya mikoa ya Tanzania haina tofauti na haipishani sana. Huyo RC au DC anayeletwa huko mkoani au wilayani ni Mtanzania wa kawaida na anayajua mahitaji ya mkoa husika, kama hayajui basi asaidiwe na RCC au DCC yake. Mfumo huu wa akina Lissu na Amsterdam ni mtego wa kurudisha UKABILA na UTENGANO Tanzania.Tusiende huko Mbali, tuangalia County Government hapa Kenya zinavyofanya vizuri. Au hata tuwe na mfumo kama wa South Africa.
Mambo ya USA utatuambia litakapokuja swala la East Africa Federation sio leo.
Leo kwanini unatuletea mkuu wa Mkoa kama picha hana dira ya maendeleo hana uwezo wa kuamua chochote cha maendeleo, DC anawaza chama kishinde kwisha.
Sisi tunataka tujiamulie Vipaumbele vyetu wenyewe, mfano Kilimanjaro shule, umeme, Barabara, Hospital sio kipaumbele tena wao wanataka kwenda next leval wakati sisi Shinyanga Mabwawa ya maji ni kipaumbele chetu kwa ajili ya Mifugo na umwagiliaji