Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Waungwana,
Chunguzeni leo hii nchi zote ambazo ni kinara wa mfumo wa Serikali za majimbo (federal government) duniani ni nchi ambazo zilikuwa zinakabiliwa Sana na tatizo la kukosa umoja wa Kitaifa kutokana na Vita, udini au Kukosa lugha ya kuwaunganisha.
Marekani walikuwa mataifa huru 50. Kuwaunganisha ni lazima uwaachie baadhi ya madaraka yao, hivyo mfumo wa Serikali ya Majimbo ni sahihi kwao.
Canada wanashida ya lugha. Kuna majimbo hawajui au hawaongei kabisa kiingereza, wenyewe wanaongea kifaransa. Hawa ni muhimu kuwa na majimbo ili wawe huru kutumia lugha waipendayo.
Ujerumani walitawanyika na kuwa nchi mbili tofauti na ukuta ukajengwa Kati ya Ujerumani ya Mashariki na ile ya magharibi. Hawa ili kuwaunganisha mfumo wa Serikali ya Majimbo ulikuwa lazima ila maeneo hayo yabaki na sehemu ya utawala wake wa awali.
Nigeria imepitia mengi sana sana Kati ya waislamu wa kaskazini na wakristo wa kusini. Waafrika kusini vilevile wamepitia mengi Kuhusu ukoloni na ukaburu. Wazungu wengi walibaki Afrika Kusini baada ya Uhuru kamili mwaka 1994. Kwa misingi hiyo, unaweza kabisa kuona Nigeria na Afrika kusini walihitaji utawala wa majimbo.
Sisi Tanzania tunahitaji utawala wa majimbo ili iweje? Je, changamoto za kiuchumi, utamaduni na kisiasa zinatokana na mazingira hayo niliyoyataja hapo juu?
Wazungu hawana makabila na karibu wote wana dini au imani sawa. Kuwawekea utawala wa majimbo sio mbaya. Hapa kwetu tunajadili sio to dini Bali hata dhehebu. Kuna baadhi ya watu walisema katika uchaguzi wa 2015, Sasa ni zamu ya M-KKKT kuwa wa -RC wametawala Sana. Sasa kwenye nchi Kama hii uanze umajimbo, tunategemea nini kitokee?
Majimbo yatatutenga zaidi badala ya kutuleta pamoja. Mfumo wa Serikali za mitaa kwa Tanzania ni mzuri na toshelevu. Kama Kuna changamoto basi ni Kuboresha tuu.
Ninawashangaa Sana wapinzani, sijui wamekunywa wanzuki ya wapi. Tasilimali za kila eneo husaidia eneo hilo na maeneo mengine. Hii ni kwasababu watu wanaingiliana na wanaweza kuishi popote. Mtoto wa Kagera anapangiwa kazi Tanga na maisha yanaenda. Mtu wa Mtwara anahamia Mbeya anakuwa mnyaki maisha yanaenda.
Watanzania tuukumbatie umoja, amani na mshikamano wetu kwa kuchagua mafiga matatu hapo 28 Oktoba, 2020. Tuwaadhibu wapinzani wanaotaka kutugawa kwa kuwanyima kura.
Amani Msumari
Tanga (kwasasa Kigamboni kumtafutia Rais Magufuli kura za bonus).