Je Wajua Kuwa Kura ya "Hapana" Kwa Katiba Mpya! Ni Kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba Hii Iliyopo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,

Salaam.

Tuendelee kuelimishana kidogo kidogo kuhusu kura ya maoni ya kuikubali hii katiba mpya au kuikataa!. Nimenote kampeni za waziwazi kuikataa zimeanza kila upande kwa wapinzani, wana UKAWA na wana harakati, huku CCM na washirika wake wakipiga kampeni ya ndio.

Pamoja na malalamiko yote kuhusu hii katiba mpya, haswa upande wa mapungufu, lakini pia kuna kaukweli kidogo, kuwa ukiilinganisha na katiba iliyopo sasa, hii katiba mpya ni much much better kuliko katiba iliyopo!, hivyo nineshauri, wale wote wenye kuhamashisha kupiga kura ya "Hapana" kwa mara zote mbili, kwa Katiba Mpya!, pia wawaelimisha wafuasi wao kuwa ile kura yao ya "Hapana" maana yake sio tuu ni kuipinga katiba mpya, bali kura yao ya "Hapana" ikipigwa mara mbili, inahesabika kama ni kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba iliyopo sasa iendelee!.

Hii inamaanisha ni kuwapa CCM ule uhalali wa kuendelea na ule mtindo wa kuchakachua kura za urais, unaokubalika kisiasa duniani kote!, unaitwa "the end justifies the means!", haijalishi ni mbinu gani zimetumika, mtu akiishatangazwa ameshinda urais, ndiye rais na hakuna tena mjadala!. Huu ndio msimamo wa katiba iliyopo!. Hiki ndicho kilichofanyika kwenye kuipitisha katiba mpya kule ndani ya BMK na pia ndicho kitakachofanyika kuipitisha kwenye kura za maoni, "zisipotosha!, zinatosheshwa!".

Sasa kwenye katiba mpya angalau kuna kipengele kinaruhusu, mgombea urais mwenye ushahidi usiotia shaka kuwa "hazikutosha bali zimetosheshwa" anapewa fursa kutinga mahakamani, kuhoji matokeo ya urais!, waungwana wetu hili nalo hawalitaki!, wanaipinga katiba mpya yote kama ilivyo on its totality!.

Ushauri wangu mimi ni ule ule, "if you can't get what you want, just take what you get!", yaani usipopata kile ulichotaka, bora uchukue kile kilichopatikana" kwa minaajili ya "moja shika sii kumi nenda rudi!", Watanzania tulitaka "Katiba Bora!", hii tuliyoletewa ni "Bora Katiba!", bora tuikubali, tuipigie kura za ndio, ipite tupate katiba mpya kwa hoja ya "something is better than nothing!", Katiba ya zamani ni nothing!. Watanzania tukiikataa katiba mpya!, tutaendelea na katiba ya zamani!, hivyo uamuzi wa ama tuikubali katiba mpya ama tuikatae, utokane na kipi bora katika katiba mpya na katiba ya zamani!, na sio kuipitisha au kuikataa!.

Wengi wanaoipinga katiba mpya, wanatumia kigezo cha rasimu ya Warioba ilikuwa ni better kuliko katiba mpya ya CCM, wakidhani ukiipigia kura ya hapana katiba mpya, basi tutarudi kwenye ile rasimu ya Warioba!. No way!. Tukiikataa katiba mpya, tunarudi bach pili ya back to squire one!, kwa Bunge lili lile la Katiba, kupitia kwa watu wale wale, kujirudia kufanya yale yale, hivyo kuturejesha kwenye katiba hii hii iliyopo!, wanasheria wanaita "ab initio!" yaani haikuwahi kuwepo!, hivyo tuaendelea na katiba ya zamani as if nothing happened na hapa ndipo CCM itatawala milele ya kweli!.

Nawashauri wapinzani wote wa katiba mpya, tuipinge hii "Bora Katiba!" objectively, huku tukiwaeleza kinaga ubaga, watu tunaowashawishi, kuwa kupiga kura ya "Hapana!" na "Hapana" tena, kwa "katiba Mpya, kura hiyo ya "Hapana!" maana yake ni kura ya "Ndio!" kwa katiba hii mbovu iliyopo!.

Kwa msisitizo!,
Jee Wajua Kuwa Kura ya "Hapana" Kwa Katiba Mpya! Ni Kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba Iliyopo?!. Nikimaanisha jee mnajua kuwa katiba mpya ikikataliwa jumla, ni katiba ya zamani ndiyo inayoendelea?!.

Msingi wa hoja hii, ni kuna watu wanadhani, ukiikataa hii "Bora Katiba" ya CCM, basi ndio unaipata ile katiba ya kwenye rasimu ya Warioba!. No way!, tukiikataa hii katiba, na kuikataa tena!, tunarudishwa kwenye hii hii katiba mbovu iliyopo!.

Kwa kulizingatia hili, mimi naunga mkono juhudi zozote zinazofanywa ipite, hadi ule mpango mkakati kabambe wa "zisipotosha!, zinatosheshwa!"

[video=youtube_share;Wf6EtEmxSOw]http://youtu.be/Wf6EtEmxSOw[/video]
Wasalaam.

Pasco.
 
Hivi kwenye kura za maoni UTARATIBU WA MAWAKALA wa kambi za ndio na hapana utakuwepo? kama hawa jamaa bungeni wameiba kura sembuse vijijini?
 
Ukawa hawataki kusikia kuhusu katiba mpya. Wao wanaona kuwa katiba iliyopo ni bora iendelee kuliko hii mpya kwa vile haina mazuri yoyote kwao. Wao wananadi ubaya tu wa katiba mpya na sijasikia wakisifu mazuri yake
 
wewe pasco acha kupotosha jamii, kinachopigiwa kurahapa nikatiba mpya kwani hatakama kaendelea ya zamani kukatofauti gani na mliyotengeneza ninyi ccm, hatuoni umuhimu wa kutoa tairi chakavu kuweka chakavu zaidi.ngojeni siku ifike mtatuona.
 
Nimesoma heading tu, hivyo najibu hilo swali.
Yes najua, na pia kura ya hapana itafanya utokee mchakato mwingine wa kupata katiba in the near future kuliko kura ya ndio ya katiba ya ccm ambapo mchakato mwingine waweza chukua miaka mingine 50 kwa uchache.

So Mr Pasco sir, ni big HAPANA na katiba ya watawala.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma content, bado msimamo ni ule ule, twaweza kusubiri miaka mingine 10 au hata 20 ili tupate kitu kizuri. Hii ni system yangu ya maisha. Ni bora nikae bila tv kwa miezi 6 nikisave ili nije ninunue tv ya maana kuliko kununua chogo mchina nitumie halafu baada ya miaka 5 ndio nije ninunue flat screen
 
Pasco wenzio tuliandika hivyo, wahafidhina wakatutukana hapa.Huo ndio ukweli, Watanzania hasa Wazanzibari, tuchague moja. Mpya yenye maboreaho kibao au ya zamani. La katiba mpya tutasubori miaka 20 ijayo
 
Kaka Pasco, upo sahihi kabisa. Ila wahafidhina siku zote hawapendi kuambiwa ukweli. Hii tabia yako ya kusema ukweli inawakera wahafidhina wote
 
Pasco wenzio tuliandika hivyo, wahafidhina wakatutukana hapa. Huo ndio ukweli, Watanzania hasa Wazanzibari, tuchague moja. Mpya yenye maboreaho kibao au ya zamani
Kaka Kifaurongo, kwa vile UKAWA wameamua kufeli mtihani ili warudi kijijini wakachunge ng'ombe, wao watachagua ya zamani ili sisi watanzania tukose fursa zilizopo kwenye katiba mpya
 
Nimesoma content, bado msimamo ni ule ule, twaweza kusubiri miaka mingine 10 au hata 20 ili tupate kitu kizuri. Hii ni system yangu ya maisha. Ni bora nikae bila tv kwa miezi 6 nikisave ili nije ninunue tv ya maana kuliko kununua chogo mchina nitumie halafu baada ya miaka 5 ndio nije ninunue flat screen
Hahahahahaaaaaaa! Hicho kizuri kitatoka wapi shoga angu kama si kwa watu hawa hawa waliotuletea kizuri kupitia katiba hii mpya? Ni bora kuchukua hiki kizuri kuliko kuendelea na kibaya kwa zaidi ya miaka 20. Wewe huna tofauti na mtu ambaye yupo jirani na dispensary lakini anashindwa kwenda kutibiwa malaria eti anataka aende hospitali ya rufaa ambayo ipo mbali naye
 
The-Arab-Spring1.jpg
 
Subiri matusi kutoka kwa wana UKAWA

sio kwa wana ukawa peke yao,bali hata sisi ccm-asp hatukubaliani na katiba mpya huko dodoma tumenyamaza kwa kuogopa kutupata kilichompata mansour na kupoteza ufalme wetu znz,lkn sisi wazanzibar ki nje mtatuona tuna migogoro ila ukizama deep utaona kwamba hakuna mzanzibar anaetaka kupoteza heshma yke ktk muungano,dada yetu salma said amenipa taarifa kuwa pale bungeni baadhi ya vigogo vya ccm-znz waliwaomba wao waikatae kutokana na wao kushndwa kuufyata,ila kuna baadhi ya vigogo wa ccm kina Raza ,mheshimiwa Hamza,and the like washasema misimamo yao waziwazi dhidi ya hii katiba,kiukweli hasa nyinyi Tanganyika mumegain katiba hii ni bora kwenu kuliko ya zamani na hamna kitu mnapoteza,ila sisi wazanzibar whatever we are tuna poteza sana ukizingatia sisi katika katiba ya jamhuri hatuna tunachofuata zaid ya muungano sasa mkiuchakachua sisi tutawaeleza nini wapiga kura wetu ambao asilimia 90&more kwao ni koti?musifikiri wazanzibar ni wajinga kiasi cha kukubali kupoteza maslahi yake kijinga kiasi hichi pale bungeni wamemridhisha mkoloni mweusi,kazi ipo blw
 
Hilo likatiba la chenge huko huko lijadilini, sisi waznzibar tuna katiba yetu,

Ambayo haiwapi mamlaka ya kumiliki mali asili zenu wala uhuru wa nani awe rafiki yenu. Ikataeni hii msubiri miaka 20 ya uchumi wenu kuamliwa na koti.
 
Yawezekana Pasco unasema kweli lakini kwani hata kabla ya kufa si unaweza kukaa sana ICU yaani duniani hauko wala ahera hujafika??!!!

Au ukiwa bakery ni lazima ule mkate au andazi, si waweza pata chapati au hata visheti??!!!

Yaani ni kuwa kukubali ku "settle for less" ati kwa sababu kama vile "ataruhusiwa kwenda mahakamani" yaani hili nalo ni hoja ya wananchi wote???!! Au kambi yenu ina interest hapo tu katika katiba pendekezwa??!!!

Watu wanatakiwa wapate watakacho sio kilichopo, usiwekama wazee wachoyo wanaosema "mke wangu sina hela kabisa imebaki elfu hamsini ya bia tu" wqkati sukari na matumizi muhimu hakuna kabisa!!!!
 
Last edited by a moderator:
sio kwa wana ukawa peke yao,bali hata sisi ccm-asp hatukubaliani na katiba mpya huko dodoma tumenyamaza kwa kuogopa kutupata kilichompata mansour na kupoteza ufalme wetu znz,lkn sisi wazanzibar ki nje mtatuona tuna migogoro ila ukizama deep utaona kwamba hakuna mzanzibar anaetaka kupoteza heshma yke ktk muungano,dada yetu salma said amenipa taarifa kuwa pale bungeni baadhi ya vigogo vya ccm-znz waliwaomba wao waikatae kutokana na wao kushndwa kuufyata,ila kuna baadhi ya vigogo wa ccm kina Raza ,mheshimiwa Hamza,and the like washasema misimamo yao waziwazi dhidi ya hii katiba,kiukweli hasa nyinyi Tanganyika mumegain katiba hii ni bora kwenu kuliko ya zamani na hamna kitu mnapoteza,ila sisi wazanzibar whatever we are tuna poteza sana ukizingatia sisi katika katiba ya jamhuri hatuna tunachofuata zaid ya muungano sasa mkiuchakachua sisi tutawaeleza nini wapiga kura wetu ambao asilimia 90&more kwao ni koti?musifikiri wazanzibar ni wajinga kiasi cha kukubali kupoteza maslahi yake kijinga kiasi hichi pale bungeni wamemridhisha mkoloni mweusi,kazi ipo blw

Ni porojo nzuri, tunataka vitendo sisi. Sio unakubali kuaibishwa waziwazi tena ukishangilia kwa taarabu, halafu chumbani unadai hukutaka. Kwa hali yoyote Zanzibar ndio vinara, maana mmekubali hata kuchakachuliwa ili shamba la bibi Tanganyika liendelee kuvunwa.
 
Yawezekana Pasco unasema kweli lakini kwani hata kabla ya kufa si unaweza kukaa sana ICU yaani duniani hauko wala ahera hujafika??!!!

Au ukiwa bakery ni lazima ule mkate au andazi, si waweza pata chapati au hata visheti??!!!

Yaani ni kuwa kukubali ku "settle for less" ati kwa sababu kama vile "ataruhusiwa kwenda mahakamani" yaani hili nalo ni hoja ya wananchi wote???!! Au kambi yenu ina interest hapo tu katika katiba pendekezwa??!!!

Watu wanatakiwa wapate watakacho sio kilichopo, usiwekama wazee wachoyo wanaosema "mke wangu sina hela kabisa imebaki elfu hamsini ya bia tu" wqkati sukari na matumizi muhimu hakuna kabisa!!!!
Enheeeeee, mwambie mkuu. Kasahau Ariel Sharon amekaa miaka mingapi ICU na bado mwisho wake upo.
 
Back
Top Bottom