Je, wajua kuwa kuna siku ya Wanaume Dunia?

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Kama kulivyo na siku ya Wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka mnamo Machi 8, Novemba 19 ni siku ya Wanaume duniani

Mataifa zaidi ya 70 hujumuika pamoja kuadhimisha siku hiyo duniani tangu ilipoanzishwa mwaka 1999

Huadhimishwa kuhamasisha utu ulimwenguni, kutilia mkazo hali ya afya kwa Wanaume, kuboresha mahusiano ya kijinsia, kukuza usawa wa kijinsia na kuwasihi Wanaume kuwa mfano wa kuigwa

Siku hii inalenga kupambana na aina zote za ubaguzi dhidi ya Wanaume na kusheherekea mafanikio na mchango wao katika familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom