Je wajua kuwa King Leopold ni wa kwanza kufanya mauaji ya halaiki?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3][/h]

thumbnail.aspx

Leo nimemkumbuka jambazi na mwanaharamu aliyeitwa mfalme Leopold II (1835-1909) wa wabelgiji ambaye ni binadamu wa kwanza kufanya mauji ya kimbari nchini DRC. Mwanaharamu huyu aliyepata malezi mabaya kiasi cha kuoa hata asiweze kufanya tendo la ndoa kwa mkewe, aliua zaidi ya wacongoman 15,000,000 akitaka kutimiza tamaa yake ya madaraka na utajiri. Wengi huwa hawajui kuwa jambazi huyu ndiye alifyatua tufe la mauaji ya kimbari na halaiki kwa muda wote aliokalia DRC. Sura yake hata mavazi yake yanaonyesha ukatili usio kifani. Huyu pamoja na majambazi wengine kama Dk. David Livingstone, Fredrick Lugard, Cecil Rhodes,Mungo Park, Henry Morton Stanley, Christopher Columbus, Fransico d'Almeida, Lord Kitchner aliyefika kwa kuiteka na kuikalia Sudan akitumia fuvu la binadamu mwafrika kama kidau cha wino na wengine ndiyo waliotusababisha haya masahibu ya umaskini tunayokumbana nayo. Wakati mwingine tunahitaji kujua historia yetu ili tujikomboe. Je ni wangapi wanalijua hili wakati kwa ujinga wao waliwaita majina watoto wao kwa kumbukumbu ya watesi wao?
 
inasemekana kabla ya wachina kuingia mikataba fulanifulani na DRC ya madini in exchange of silaha, walienda kutazama makabrasha Brussels kujua hazina iliyopo DRC. it seems DRC haina mwenyewe, ndo maana Rwanda na Uganda nao waliamua kwenda kujichotea huko vinavyochoteka.
 
Mkuu, what do you mean DRC haina mwenyewe? fafanua kidogo.
Kwa mtoa mada na all interested, for more about Leopold occupation of Congo and the long lasting impact, soma King Leopold's Ghost (Wiki link for overview). During that period alone, more than half of the nation population was executed.
 
Huyu pamoja na majambazi wengine kama Dk. David Livingstone, Fredrick Lugard, Cecil Rhodes,Mungo Park, Henry Morton Stanley, Christopher Columbus, Fransico d'Almeida, Lord Kitchner aliyefika kwa kuiteka na kuikalia Sudan akitumia fuvu la binadamu mwafrika kama kidau cha wino na wengine ndiyo waliotusababisha haya masahibu ya umaskini tunayokumbana nayo. Wakati mwingine tunahitaji kujua historia yetu ili tujikomboe. Je ni wangapi wanalijua hili wakati kwa ujinga wao waliwaita majina watoto wao kwa kumbukumbu ya watesi wao?

Hakuna nchi duniani ambayo haikukumbana na masahibu katika historia yake. Hata himaya ya urumi iliteketea. Sisemi kuwa yaliyotokea Congo ma Afrika kwa jumla hayakuwa mabaya. Yalikuwa mabaya sana tokea wakati wa utumwa, ukoloni na ukoloni mambo leo.

Kitu ambacho nchi zetu inabidi kiachane nacho ni kuwalaumu watu waliokufa miaka nenda rudi kwa matatizo yetu. Hicho ni kipimo tosha cha udhaifu wetu. Lets not forget but lets forge ahead.
 
Mkuu, what do you mean DRC haina mwenyewe? fafanua kidogo.
Kwa mtoa mada na all interested, for more about Leopold occupation of Congo and the long lasting impact, soma King Leopold's Ghost (Wiki link for overview). During that period alone, more than half of the nation population was executed.

HAINA mwenyewe in the sense that hakuna strong government yenye uezo wa kusimamia mipaka ya nchi hiyo zikiwemo rasilimali za asili za nchi hiyo zinazokadiriwa kuwa around $ 200 billion. Perhaps this is the richest country in the world, ukitizama definition halisi ya neno utajiri.
 
Hata Tz haina mwenyewe kwa mtaji huu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom