Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,431
Wanabodi,

Kuna vitu mimi huwa navisema humu just as hypothetical situation na watu humu wanavichukulia poa hivyo kunibeza, na wengine hata kunitukana!, ila siku vikija kutokea kweli ndipo wenye uelewa wanaanza kuelewa nilikuwa nazungumzia nini na kuheshimiana.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyovisema na nikabezwa sana humu, lakini vilipokuja kutokea kweli, ndipo tuka heshimiana.
  1. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
  2. Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
  3. Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums
  4. Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums
  5. Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums
Sasa ninachokisema leo humu, ni just à hypothetical situation ya kufikirika tuu, kwasababu sio ni kuwa sio wengi wanajua kuwa hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Wilfred Lwakatare kufuatia huyu ndiye Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema anayejua mambo yote ya Chadema ya kwenye mwanga na ya gizani!.

Story ya Ugali na Mboga.
Chadema imepakua ugali kwa kila mtu kupewa ugali kwenye sahani yake, Kamati Kuu ya Chadema, wakaamua kuipindua sahani ya ugali wa Lakwatare, na kuumwaga ugali ili Lwakatare asile, huku wengine wote wakiwa na sahani zao za ugali wao mikononi, wakisubiri bakuli la mboga litetwe, huku hakuna mwenye kumbukumbu ni nani aliyetumwa jikoni kwenda kuleta bakuli ya mboga, watu wapakuliwe ndipo wale!.

Mara aliyeibuka jikoni na bakuli ya mboga ni Mhe. Wilfred Lwakatare!, amelishika bakuli la chuma la mboga za moto kwa mikono yake, huku mikono yake inaungua lakini amestahimili na kuvumilia huku akitokwa machozi, jasho na damu, kwa ajili ya Chadema!.

Kabla hajalitua bakuli la mboga ili watu watu wapakue wote wale, akagundua kuwa ugali wake umemwagwa!.

Wakati wanamwaga ugali wake, hakuna aliyekumbuka kuwa anayesubiriwa kuleta mboga watu wale ni Lwakatare, hivyo sasa wote wamenyamaza kimya kusubiria Lwakatare, atafanya nini baada ya kubaini Chadema wamemwaga ugali wake, huku mwenye bakuli ya mboga ni yeye!, sasa hatima ya kama Chadema watakula ama hawali, iko mikononi mwa Wilfred Lwakatare, baada ya wao kumwaga ugali, Lwakarare akiamua na yeye kumwaga mboga, then, chakukula hakiliki, wanakosa wote!, yaani Chadema ndio inakuwa kwishney!.

Ili uelewa mimi nazungumza nini, ni lazima kwanza ukijue kisa, ambacho ndio bakuli ya mboga.
Ngoma ilianzia Star TV tarehe 30 Dec, 2012
On Star TV: Zitto, Nchemba na Mtatiro ktk mjadala wa kutathmini ya Siasa Tanzania 2012 - JamiiForums

Ndipo hatimaye movie ikapandishwa kwenye mtandao wa YouTube na hapa ukazungumziwa mwanzo mwisho
Chadema wafichua mtandao wa ugaidi - JamiiForums
Mwigulu Nchemba amekiri kuhusika na movie ya Lwekatare - ashikwe na kuunganishwa kesi hiyo - JamiiForums

Kisa chenyewe ni hiki.
Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare - JamiiForums
Japo mimi sio official authority, ila nimetazama ile video clip, nimejiridhisha its "bonafide genuine!", haijapitia doctoring yoyote!, japo ni kweli technolojia hizo zipo, kama lengo ni kuichafua Chadema, then of all the people, not Rwakatare!.
Pasco.
Chadema ni chama cha ajabu sana!, kinayo katiba yake ambayo ina ainisha taratibu zote za nidhamu ndani ya chama, kwanini hazifuatwi na badala yake kila siku kwenye timua timua ni mwendo wa a Kangaroo court?, mnakuja kuwatimua wanachama wenu kihuni huni tuu!, why?!. Kwanini CC ya Chadema inatoa maamuzi ya kihuni na kidikiteta bila kufuata sheria, taratibu na kanuni?. Why kwenye kutimuana always ni Kangaroo Court?.

Kuna watu unaweza kuwatimua kihuni huni tuu kwa kuwafukuza kama mbwa, lakini sio Lwakatare, na sababu ni moja tuu, huyu ameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!.

Chadema inapaswa kumyenyekea Lawakatare na kwasababu aliishatangaza kustaafu, Chadema walipaswa kumuacha tuu astaafu kwa amani, haswa kwa kuzingatia wamemfukuza wakati ambao Bunge hili limebakiza wiki3 tuu limalizike rasmi!.

Umuhimu wa Lwakatare kuachwa tuu hata afanye nini au aseme nini, ni kumzuia asije kufungua mdomo wake akamwaga mboga ugali ukashindwa kulika!

Ikitokea Lwakatare akaamua kufungua mdomo wake na kuyataja madudu ya ajabu Chadema inayoyafanya nyuma ya pazia, ikiwemo ile video mimi niliyoita hapo kuwa "bonafide genuine", Chadema Watakuwa mgeni wa nani?. Nani atabaki salama kwenye top brass ya Chadema ?

Mtu key kama Lwakatare anafukuzwaje?.

Kufuatia hiyo video niliyoitaja kule juu, nilipokutana na Msajili wa vyama alisema
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...! - JamiiForums

Sasa hiyo endapo katika bandiko hilo, ndilo bakuli la mboga, Lwakatare amelishikilia, licha ya yeye kumwagiwa ugali wake, anaweza kuamua yeye peke yake ndio akose kula na kulala njaa, hivyo atalitua tuu hilo bakuli la mboga mezani na wengine wote wale, na yeye tuu ndio akafie mbele, ila akiamua kuonyesheana ubabe, na mambo yanakuwa ni ubabe ubabe tuu, maadamu wamemwaka ugali, na yeye sasa anamwaga mboga...
yatakuwa mengine!.

Lets keep watching tukisubiria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.

Paskali

Update kuhusu angalizo la uchangiaji.

Japo jf was ment to be a home of great thinkers,
Lakini humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Mtu kuwa simple mind, ordinary mind na great minds ni the way one comprehend and thinking capacity, nimesema Lwakatare ameishika hatma ya Chadema mkononi mwake. Kwa vile Chadema wao wamemwaga ugali yeye akiamua Kumwaga mboga, Chadema keisha!.

Ma simple minds watamdiscus mleta mada, Pasco na Lwakatare, hivi na vile, sii lolote sii chochote, that is their level.

Ordinary mind wao wata discuss event ya Lwakatare kutimuliwa na atamwaga vipi mboga, atakakata tawi alilokalia etc.

Great minds wata discuss hiyo hatma ya Chadema, jee ni kweli ikijulikana Chadema kinakufa?, hiyo hatma yenyewe ya Chadema Lwakatare aliyo mayo ni nini haswa?, does have merits hadi Chadema ife, etc

Hivyo be free kujadili kwa kadri ya uwezo wako na kundi lako keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.

Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
Tuache kuongozwa na mahaba ya kitoto na wingi wa maandishi, Pascal nakuhehimu sana na ukweli unaujua, CHADEMA is there to stay, mark my word, hata akiondoka Mbowe, hakuna wa kuimaliza CHADEMA na unaujua ukweli.

Kuandika kwa kirefu sana na reference za thread ambazo mwandishi ni wewe mweyewe hakusaidii chochote kile ndugu yangu. aliondoka Zito mkaandika weeee, akaondoka Slaa mkachonga sana, lakini pata picha ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana, wote tunajua nini kilitokea. Tusijidanganye wala kujifariji kwa mambo ya kitoto. Tujadili issues muhimu. Chadema IFE huku mnamuogopa Mdude Chadema? Hahhahaahaha

Leo hii Wapinzani wametoka Bungeni, Bunge zima limewageuza kuwa mjadala! Why? kwasababu wako strong. kwasababu uwepo wao una mtetemo mkubwa. Tusijifungie Dar na kuandika tu
 
Hakuna kitu hapo bali propaganda kutafuta huruma kwa watawala. Kama CHADEMA haijafa baada ya Dk Slaa na haijafa miaka 5 bila siasa na haijafa kwa bunduki na mabomu na jela na mapanga na jela, ni nani wa kuipoteza CHADEMA? Lwakatare sisimizi ndo aipoteze CHADEMA? Kweli ww njaa imekupanda kichwani kama lilivo jina lako.


Chadema ni imani, chadema sio majengo...chadema iko sisiemu...chadema iko kwenye utawala.
 
Tumeshindwa kujenga hoja, tumerukia kwenye ushabiki. Well si lazima kila kitu kiende hivyo but sometimes kuna vitu inabidi tutumie akili ya kawaida.Cadema iliwajenga wananchi waka=feel ownership ya Chama hata pale kauli za Ukanda na Uchaga zilipopigiwa chapuo kamwe hazikfanikiwa, CCM wakajijenga kwenye maslahi. leo hii kila mwanachama aliyeko CCM yuko kwajili ya tumbo lake.....
 
Wanabodi,
Kuna vitu mimi huwa navisema humu na watu wanavichukulia poa, ila vikija kutokea ndipo wenye uelewa wanaanza kuelewa nilikuwa nazungumzia nini.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyovisema na kweli vikaja kutokea
  1. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
  2. Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
  3. Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums
  4. Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums
  5. Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums
Sasa ninachokisema leo ni kuwa sio wengi wanajua kuwa hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Wilfred Lwakatare?. Chadema imepakua ugali kwa kila mtu kupewa ugali kwenye sahani yake, Kamati Kuu ya Chadema, wakaamua kuipindua sahani ya ugali wa Lakwatare, na kuumwaga ugali ili Lwakatare asile, huku wengine wote wakiwa na ugali wao kwenye sahani zao, wakisubiri bakuli la mboga litetwe, huku haku mwenye kumbukumbu ni nani aliyetumwa jikoni kwenda kuleta bakuli ya mboga, watu wapakuliwe ndipo wale!. Mara aliyeibuka jikoni na bakuli ya mboga ni Mhe. Wilfred Lwakatare!, Amelishika bakuli la mboga za moto kwa mikono yake, huku mikono yake inaungua lakini amestahimili na kuvumilia huku akitokwa machozi, jasho na damu, kwa ajili ya Chadema!. Kabla hajalitua bakuli la mboga ili watu watu wapakue wote wale, akandua kuwa ugali wake umemwagwa!. Wakati wanamwaga ugali wake, hakuna aliyekumbuka kuwa anayesubiriwa kuleta mboga watu wale ni Lwakatare, hivyo sasa wote wamenyamaza kimya kusubiria Lwakatare, atafanya nini baada ya kubaini Chadema wamemwaga ugali wake, huku mwenye bakuli ya mboga ni yeye!, sasa hatima ya kama Chadema watakula ama hawali, ikomikononi mwa Lwakatare, baada ya wao kumwaga ugali, Lwakarare akiamua kumwaga mboga, then wanakosa wote!, Chadema ndio inakuwa kwishney!.

Ili uelewa mimi nazungumza nini, ni lazima kwanza ukijue kisa, ambacho ndio bakuli ya mboga.
Kisa chenyewe ni hiki.
Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare - JamiiForums

Chadema ni chama cha ajabu sana!, kuna watu unaweza kuwatimua lakini sio Lwakatare, na sababu ni moja tuu, ameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!.

Chadema inapaswa kumyenyekea Lawakatare na kwasababu aliishatangaza kustaafu, Chadema walipaswa kumuacha tuu astaafu kwa amani, haswa kwa kuzingatia wamemfukuza wakati ambao Bunge hili limebakiza wiki3 tuu limalizike rasmi.

Umuhimu wa Lwakatare kuachwa tuu hata afanye nini au aseme nini, ni kumzuia asije kufungua mdomo wake!.

Ikitokea Lwakatare akaamua kufungua mdomo wake na kuyataja madudu ya ajabu Chadema inayoyafanya nyuma ya pazia, ikiwemo ile video mimi niliyoita hapo kuwa "bonafide genuine", Chadema Watakuwa mgeni wa nani?.
Mtu kama Lwakatare anafukuzwaje?.

Kufuatia hiyo video niliyoitaja kule juu, nilipokuta na Msajili wa vyama alisema
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...! - JamiiForums

Sasa hiyo endapo katika bandiko hilo, ndilo bakuli la mboga, Lwakatare amelishikilia, licha ya yeye kunwagiwa ugali wake, anaweza kuamua yeye ndio akose na kulala njaa, hivyo atalitua tuu hilo bakuli la mboga na wengine wote wale, na yeye tuu ndio akafie mbele, ila akiamua kuonyesheana ubabe, na mambo yanakuwa ni ubabe ubabe tuu, maadamu wamemwaka ugali, na yeye anamwaga mboga...
yatakuwa mengine!.

Lets keep watching tukisubria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.

Paskali
P.
Ngonjera zako tumezizoea
 
Back
Top Bottom