Je, wajua kuwa Cold War (vita baridi) kati ya USSR na Capitalist bloc ni sababu ya Russia wako sahihi kuivamia

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,767
24,186
Baada ya vita vya pili vya dunia 1945, Dunia ilishuhudia uwepo wa mataifa mawili yenye nguvu kijeshi na kiuchumi. Ambayo ni USA na Russia iliyokuwa na nguvu chini ya rais Joseph Stalin.

Mataifa haya yalikuwa na itikadi mbili tofauti ambapo USA walitaka dunia nzima ifuate CAPITALISM (ubepari) kama ilivyosasa lakini USSR wao walitaka dunia ifuate SOCIALISM (ujamaa). Ingawa baadae mfumo huu uliprove failure.

Kutokana na uwepo wa ideology mbili kati ya mataifa haya mawili kulitokea uadui mkubwa baina yao ambapo neno COLD WAR lilizaliwa kipindi hiki,ikimaanisha Dunia ilikuwa kwny Tension ya vita vya tatu vya dunia.

Cold war kati ya Socialist block (USSR) na Capitalist block (USA) ilionekana katika nyanja mbalimbali kama ifuatavyo

1.Kuanzishwa kwa NATO (North Atlantic Treaty Organization mwaka 1949 hii ilikuwa ni jumuiya ya kujihami dhidi ya vitisho vya socialist block ambapo ilijumuisha USA, Canada na nchi Tisa za umoja wa ulaya. Lkn SOCIALIST BLOCK walijibu kwa kuanzisha WARSAW PACT ilikuwa inaundwa na nchi 13 ambazo ni Bulgaria, Hungary, na zingine ambayo ilikuwa na malengo sawa na ile waliyoanzisha marekan na washirika wake

Uundwaji wa mabomu ya nyuklia . USA Walikuwa wa kwanza kuunda Bomu la nyuklia mwaka 1945 ambapo Bomu hili lilipgwa japani, lakni kimsingi Bomu hili halikua bahati mbaya ila lilikuwa ni USA kujitangaza kuwa yeye ndo baba wa dunia. Likewise 1949 USSR walifanikiwa kutengeneza Bomu la nyuklia .....kitu ambacho kilifanya kuwe na ushindani katka nyanja za kivita mfano mwaka 1952 USSR waliunda INTERCONTINENTAL BALLISTIC MISSILES Pia USA waliunda Bomu kama hilo


Sababu za Russia kuivamia Ukraine

1.kulinda interest zake pale Ukraine , hapo kabla kipind cha USSR Ukraine ilikuwa ni moja ya state zilizounda USSR so asilimia kubwa kuna raia wengi wa urusi wanaishi ndani ya ukraine, hata hivyo lugha ya urusi inatumika sana nchini Ukraine So kutokana na choko choko za marekan na washirika wake wanasambaza propaganda mbaya kwa waukraine kama vile kupiga marufuku lugha ya urusi kutumika Ukraine , kwa sababu wanataka ijitenge na Urusi ..ndio maana kuna majimbo yalijitenga kama vile CRIMEA kwa sababu yanaona ni sehemu ya RUSSIA

2.sababu za kiulinzi. Marekani na washirika wake wanapambana Ukraine ijitenge na Russia ili kuwawezesha NATO Ku expand karibu na RUSSIA kitu ambacho Putin hataki kitokee
Anyway vita haiwez kutokea
Wazungu wanaogopa sana neno VITA

Nakaribisha maoni yenu
 
Lakini kwa Nini uwe na hofu ya kukosolewa,kwa Nini usikaribishe michango au maoni zaidi?
Kwanza umeandika ukweli halafu vizuri,haya Ni maoni yako Mimi nayaheshimu na Naamini wajumbe zaidi watakuja na maoni tofauti na hii ndio demokeasia ambayo Jiwe alikua anaiogopa Sana.
 
Lakini kwa Nini uwe na hofu ya kukosolewa,kwa Nini usikaribishe michango au maoni zaidi?
Kwanza umeandika ukweli halafu vizuri,haya Ni maoni yako Mimi nayaheshimu na Naamini wajumbe zaidi watakuja na maoni tofauti na hii ndio demokeasia ambayo Jiwe alikua anaiogopa Sana.
Itakua alikuwa muumini wa SOCIALIST IDEOLOGY coz hawa jamaa wanaamini kuwa single party system ina leta umoja na mshikamano kwny nchi

Pia wanaamini kuwa Multiparty system inaligawa Taifa ..through puppetism
 
Kwann vita yao wasipiganie kwenye nchi zao kuliko kwenda kupgania kwawatu wengne Ukraine
Mkuu wale vita vyao hutokea kutokana na interest zao ......haiwez kutokea wakapigana direct au face to face
Mfano 1950's kulizuka vita vingi sana ..,.vikihusisha haya mataifa mawili
Korean war 1953, ambapo vita ilikuwa kati ya north korea vs south korea .....kwenye hii vita USSR alikua upande wa north korea .....lkn USA alikua upande wa south korea

Vietnam war 1950's the same USSR aliisuport north lkn USSR alisuport sourthen

Pia current ...kwenye mgogoro wa Syria USA ana support waasi lkn RUSSIA ana support serikali ya Assad kwa sababu ana interest kubwa kwa Assad so USA nae anataka kumpindua Assad ili aweke puppet wake

SO THE ISSUE NI INTERESTS ZAO
 
Back
Top Bottom