Je, Wajua Kuna Watu Wenye Bahati na Wasio na Bahati? - Kajaze Mafuta Kituo cha TotalEnergies Wiki Hii, Upime Bahati Yako Kwa "The Wheel of Fortune".

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,557
Wanabodi,
Haya ninayoandika ni kama utani vile lakini ndio ukweli wenyewe!,
Jee wajua ya kuwa, kuna watu wenye bahati na na wengine hawana bahati?. Wenye bahati, mambo yao yanakwenda vizuri na kusema ni bahati tuu, na wasio na bahati, mambo yao yanakwenda vibaya, na kuishia kusema ni bahati mbaya. Jee wewe umewahi kujipima kama una bahati au hauna bahati?.Kwa upande wa Waswahili wana msemo wao usemao , "Asiye na bahati, habahatishi", msemo huu ukimaanisha, wale wanaoonekana kuwa na bahati, sio kuwa wamebahatisha, bali ni watu wenye bahati zao.

Kipimo rahisi cha kwanza cha kujipima kama una bahati au laa, ni kwa kujaribu kucheza michezo ya kubahatisha, ikiwemo kucheza wa bahati nasibu.

Sasa kwa wiki yote hii, Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies inakuletea mchongo wa kwenda kupima bahati yako bure, kwa wenye magari, nenda kajaze mafuta kwenye kituo chochote cha mafuta cha TotalEnergies kilichokaribu nawe, kwa wiki hii yote, na kwa wasio na magari, nenda ukanunue bidhaa yoyote kwenye duka la Bonjou, ambalo lipo kwenye kila kituo cha TotalEnergy, utakutana na mtambo wa kupimia bahati, uitwao, "The Wheel of Fortune", utajaribisha bahati yako, kama una bahati, utapata zawadi, kama hauna bahati, utakosa zawadi.
Kwa wenye bahati, jishindie zawadi yako na uendelee na maisha yako, lakini wale wasio na bahati, nifuatena tukutane huku Bahati (luck) ni nini ?
tusemezane.

Wasome TotalEnergy wenyewe
Awamu ya tatu ya wiki ya huduma kwa wateja ya

TotalEnergies Marketing Tanzania Limited.

Dar es Salaam, Novemba 22, 2021

“Tuijenge kesho pamoja!"

Dar es Salaam, Novemba 22nd 2021:
Tahere 22 Novemba hadi 26 Novemba 2021 ni Wiki ya Huduma kwa Wateja ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd.

Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited ambayo awali ilijulikana kama Total Tanzania Limited imezindua wiki ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, yenye kaulimbiu: Tujienge kesho pamoja.

Hii ni awamu ya tatu ya wiki ya huduma kwa mteja ya TotalEnergies tangu ianzishwe mwaka 2019. TotalEnergies inaendelea kuonyesha dhamira yake kwa Tanzania kwa kuwakaribisha wateja wao ili kushiriki maono yao ya mustakabali wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited nchini. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni, Jean-Francois Schoepp alisema kuwa, "Kama baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa "Ikiwa maendeleo ya kweli yatatokea, ni lazima wananchi washirikishwe." Pia tunaamini kwamba TotalEnergies Marketing Tanzania Limited itaendelea kukuwa zaidi endapo tutawashirikisha wateja wetu wateja wetu na kuwa tayari kukidhi mahitaji kikamilifu.”

Wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wakiongozwa na mkurugenzi mkuu, Bw. Jean-Francois Schoepp walitoa huduma kwa wateja waliotembelea kituo cha TotalEnergies East Oysterbay siku ya Jumatatu na kupata fursa ya kusikiliza maoni ya wateja, kuboresha mahusiano na wateja wao kwa nia ya kuziba mapengo yoyote yaliwepo na kuweza kujenga TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa pamoja na wateja wao. Zaidi ya hayo, wateja walipata nafasi ya kucheza gurudumu la bahati katika kituo hicho na walijishindia zawadi kadhaa zikiwemo fulana, chupa za maji, kofia, bidhaa za kutunza magari kama vile baridi na air freshener, na vocha ya zawadi zilizowawezesha kununua bidhaa zozote katika duka la Cafe Bonjour lilipo kituoni hapo.

Bila shaka, TotalEnergies Marketing Tanzania Limited imekuja na taswira mpya na kuwa wabunifu zaidi, hii inaakisiwa kikamilifu na ushirikishwaji wa wateja wao kwa nia ya kuboresha ubora wa bidhaa na huduma zao ili kukidhi kila Mtanzania anayehitaji huduma za mafuta, vilainishi, pamoja na bidha zipatikanazo madukani.

Hakika, TotalEnergies Marketing Tanzania Limited imekuja na taswira mpya na kuendelea kuwa kampuni inayoongoza kwa ubora, hii inaonekana kikamilifu katika dhamira yake ya kutoa bidhaa na huduma bora kila mahali nchini Tanzania.

Contact TotalEnergies Marketing Tanzania Limited

Media Relations: Getrude Mpangile l +255784 670 582 l getrude.mpangile@totalenergies.co.tz

TotalEnergy Customer Week-Photo 1.jpg
TotalEnergy Customer Week-Photo 2.jpg
TotalEnergy Customer Week-Photo 3.jpg
TotalEnergy Customer Week-Photo 10.jpg
TotalEnergy Customer Week-Photo 13jpg.jpg


Paskali

Wakati wa uzinduzi, mimi nilikuwepo
 
Hapa sijaelewa maana kuna kujaza mafuta (full tank) na kuweka mafuta (mafuta ya buku 10).
Ebu fafanua kidogo maana Sisi wengine tunajaza mafuta tukiwa na Safar za mikoani Ila tukiwa hapa mjini tunatia mafuta ya buku 20 tu
 
Pasco ukumbuke tarehe 12 Novemba tuliambiwa yamebaki mafuta ya siku 15 tu na baadaye ikakanushwa vikali...mpaka sasa zimebaki siku 3 zitimie siku 15 ili tujue mbivu na mbichi...ngoja tuendelee na wheel of fortune😆
 
Pasco ukumbuke tarehe 12 Novemba tuliambiwa yamebaki mafuta ya siku 15 tu na baadaye ikakanushwa vikali...mpaka sasa zimebaki siku 3 zitimie siku 15 ili tujue mbivu na mbichi...ngoja tuendelee na wheel of fortune😆
Mkuu Cannabis , kwanza statement ile japo ni ukweli, lakini ilitolewa kimakosa kuwapanikisha tuu watu, kwasababu mtu mmoja ni user, na mwingine ni procurer.

Ni kama nyumbani kwako, mnakuwa mmempa maelekezo dada wa kazi, ikibaki sukari ya siku tatu, toa taarifa. Dada yeye ni user, anatoa taarifa kwa mama, wewe ndio the procurer. Mama baada ya kupokea taarifa hiyo, ana haki ya kupanic, kama ataambiwa sukari imeadimika. Ila wewe ambaye ndie procurer unazo taarifa malori ya Mtibwa yako njiani, kesho mzigo unashushwa hivyo kabla ya hizo siku tatu, sukari itakuwa imejaa madukani!.

TPDC ni user, procurer ni Ewura, ya serikali, anajua mimeli ya mafuta ilikuwa njiani saa hizi mafuta yameshushwa fulu fulu!, there was no need kuwapanikisha watu bure!.
Nenda ka roll lile wheel of fortune ujaribu bahati yako.
Pasco
 
Braza Kinjekitile hakushindwa, ila nyie mmemezeshwa hadithi za mkoloni. Je unafahamu kwamba Kinjekitile alikuwa ni nusu mtu na nusu mamba?
Mkuu Bujibuji Simba Nyanaume , hii ya Kinjekitile kuwa nusu mtu nusu mamba ndio naisikia kwako leo, na kusema ukweli kama ni kweli, then hii ni kali kuliko!.

Hawa watu wa aina hii niliwasoma tuu kwenye Greeks mythology, Kaironi alikuwa nusu mtu nusu simba. Pia niliwahi kusikia kuhusu nguvu ni nusu mtu, nusu samaki!, hii ya nusu mtu nusu mamba...ndio nasikia kwako leo!. Hii ni kubwa kuliko!.
Mimi ni Tomaso, siamini mpaka angalau nipate collaborative evidence
P
 
Back
Top Bottom