Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?.

Wanabodi,
Issue ya Kile Kishika Uchumba cha Dola Milioni 300/
Kwa vile Watanzania tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu, wala hatukuomba, naomba kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote, hatua ya kwanza ni huu mzigo wa dola milioni 300, uwekwe kwanza mezani, kuwapooza wajomba machungu ya binti yao kuzalishwa kwanza, ndipo kuposwa. Hii habari ya Acacia kuwa italipa baada ya kutoa madeni yake, iishie huko huko Acacia, maadam Prof wa Barrick aliahidi, then he must honour his promise!.

This is just a wake up call!, its not too late kuchukua tahadhari!.

Nawatakia Furahi Day Njema.
Paskali
Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.
Kitu muhimu sana ni Watanzania have the right to information the basis ya kumsamehe mwizi wetu!.

Kama deni hilo ni bonafide genuine, serikali inapoamua kusamehe, it got to give reasons. Na baada ya hapo TRA watoe taarifa kuwa wamelifuta deni hilo.

Haya mambo akina sisi tuliyasema sana humu, kama mwanzo tulizuia makinikia kwasababu tulihisi tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo!.

Tukafanya uchunguzi tutathibitisha ni kweli tumeibiwa!. Tukapiga hesabu tulichoibiwa, baba mtu mbio kaja na ahadi wamekubali kila kitu na ili kuonyeshea nia njema wakahidi kishika uchumba cha Dila milioni 300!.

Mwisho wa mazungumzo tukasamehe deni lote, na kuruhusu makinikia yaondoke huku mpaka leo mpaka kesho, bado hatujui kilichomo!.

Kama tulizuia makinikia kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukathibitisha tunaibiwa!, Tumeruhusuje makinikia bila kujua kilichomo?, kwanini tulizuia?!

More explanation on this is needed.
P
 
Back
Top Bottom